Wajumbe wa ALAT Mkoa wa Iringa wakiongozwa na Mwenyekiti wa ALAT Mkoa Mhe. Steven Mhapa wamepongeza utekelezaji wa miradi unaofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa walipotembelea na kukagua miradi hiyo April 17, 2024.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa ALAT Mkoa Mhe. Regnant Kivinge ametoa pongezi kwa usimamizi na utekelezaji wa miradi na kuweza kuzitatua changamoto wakati wa utekelezaji. Aidha Mhe Kivinge amepongeza hali nzuri ya ufaulu kwa shule ya Sekondari Ifunda na kusema kuwa sifa hiyo ni kwa Mkoa wote.
Miradi iliyotembelewa na wajumbe wa ALAT ni Jengo la Ofisi Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa lililopo katika kijiji cha Ihemi, Jengo la Upasuaji katika kituo cha Afya cha Wenda ambapo tayari limeshaanza kutoa huduma hiyo na bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya ufundi Ifunda.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa