Baraza la Wafanyakazi Iringa – DC la kumbushwa Wajibu wake.
Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa -DC)
Afisa Kazi wa Mkoa wa Iringa Bi.Leonida Kibiki amewakumbusha wajumbe wa baraza la wafanyakazi wajibu na majukumu yao ni pamoja na kutimiza malengo ya taasisi ikiwemo kutoa michngo mizuri kwa kuzingatia taaluma zao.
Bi.Kibiki ameyazungumza hayo jana katika kikao cha kwanza cha baraza la wafanyakazi kwa mwaka wa fedha 2021-2022 huku akiwataka wawakilishi kuwa sauti ya watumishi wote na sio kutazama tu maeneo wanayotoka.
Aidha,katika kikao hiko kulifanyika uchaguzi kwa nafasi ya Ukatibu na Bw.Robin Gama aliibuka mshindi kwa kura 29 kati ya 57 zilizopita huku Bi.Gloria Tawa akipata kura 28 nakufanya idadi yote ya kura halali kuwa 57 na hakukuwa na kura iliyoharibika.
Baada ya uchaguzi huo Kaimu Mkurugeni Mtendaji ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Dkt.Samwel Marwa aliendelea na kikao na wajumbe waliibua hoja mbalimbali zikiwemo za upandaji wa madaraja,kutolipwa nauli za likizo na pesa za kujikimu kwa baadhi ya Watumishi na kutotembelewa na kusikilizwa kero wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao.
Bi.Merania Mwinuka aliomba kwa Mwenyekiti na Afisa Utumishi wawe na ziara za kuwatembelea watumishi na kusikiliza kero zao kwani kitendo hiko kitaleta utulivu na amani n ahata utekelezaji wa wajumuku utakuwa mzuri.
“Kutokuwa na amani na kutokuwa na taarifa ama majibu sahihi ya maswali yako kama mtumushi kunapunguza ari na weledi katika kutekeleza majukumu ya kila siu ya kiutumishi”Alisema Bi.Merania Mwinuka Muuguzi Hospitali teule ya Tosamaganga.
Akitoa ufafanuzi wa hoja hizo Afisa Utumishi Wilaya Bi.Beatrice Augustine alisema kuchelewa kwa masuala ya upandishwaji na ubadilishwaji wa muundo vilicheleweshwa na zoezi la uhakiki Watumishi hewa lililofanyika kuanzia mwezi Mei 2016 na baada ya zoezi hilo kukamilika taratibu za kiutumishi ziliendelea mpaka mwaka huu Mh.Rais alipoagiza Watumishi wanaostahili kupanda madaraja na kupata nyongeza ya mshahara ambalo limefanyika na tayari watumishi wameshaanza kuona nyengeza hizo.
Kuhusu watumishi kulipwa likizo alifafanua kwamba mtumishi unapokwenda likizo ambayo unastahili kulipwa nauli unatakiwa kuambatanisha fomu ya likizo na barua ya kuomba kulipwa fedha hizo na sio kweli kuwa Watumishi waliozaliwa ndani ya Mko,Wilaya ama Kijiji ambapo taasisi ipo haustahili kulipwa nauli.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa