CAMFED ni shirika linashughulika na watoto wanaoishi katika mazingira magumu shuleni kwa kuwasaidia kulipia gharama mbalimbali. Pia husaidia kwa watoto waliacha shule kwa matatizo mbalimbali na kuwarejesha shule waweze kuendelea na masomo.
Pamoja na juhudi zinazofanywa na Shirika hili, pia wameweza kutoa vishikwambi kwa Wakuu wa Shule Ishirini na Tano ili kurahisha utoaji taarifa za watoto hao. Vishikwambi hivi watatumia Wakuu wa Shule au Walezi wanaosimamia watoto hawa.
Ester Sanga Mratibu wa Mradi CAMFED amesema, pamoja na kutoa huduma za kuwasaidia watoto hawa pia tunatoa program nyingi zinazohusiana na makuzi ili mtoto aweze kujitambua.
“Progaram hizi zinasaidia kuwaelimisha watoto hasa walioacha shule na kuwarejesha shule, pia vikundi vya wazazi ili waweze kutoa changamoto zao ambazo zimesababisha kushindwa kutunza watoto na kupelekea mtoto kuacha shule”, amesema.
Ameongeza kusema kuwa, Program hizi kwa kushirikiana na Serikali zinawawezesha watoto hawa kuwa katika mazingira bora ya kujifunzia”. Ameongeza kusema kuwa, Program hizi zinazotelewa na CAMFED zinafanyikia shule na siyo mtaani, kwa mfano Program ya ‘Dunia Yangu Bora’ inafunza kwa upana zaidi jinsi ya kumuelimisha mtoto aliyekata tamaa na kumrejeshea furaha”.
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Bwana Sylvester Mwenekitete amesema, “nashukuru kwa kutupatia vishikwambi hivi ambavyo vitawasidia Wakuu wa Shule/Walezi hawa kutoa taarifa kwa wakati na kwa usahihi. Halmashauri ina shule za sekondari nyingi lakini kwa Shule hizi Ishirini na Tano si haba na kwamba wataweza kufanya kazi kwa haraka zaidi kuliko walivyokuwa wanaandika kwenye makaratasi”. Pia naomba Shirika la CAMFED liendelee kuwaangazia watoto wengine wenye mazingira magumu ili kuwaokoa katika ulimwengu huu wa sasa ambapo watoto wanapotea kwa kukatishwa tamaa” amesema.
Naye Afisa Elimu Taaluma Mkoa Ndugu Gervas Simbeye ametoa shukrani za dhati kwa shirika la CAMFED kwa wito walionao wa kuwasaidia watoto wenye mazingira magumu. Ameomba wadau wengine kujitolea kutoa huduma kama hii ili kuokoa kizazi hiki kinachoangamia kwa changamoto mbalimbali.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa