Wakazi wa Pawaga Wahofia Baa la Njaa
Wananchi na wakazi wa Tarafa ya Pawaga Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, wahofia kupatwa na baa la njaa kutokana na uwepo wa ndege washambuliao mpunga shambani, baada ya kuona ndege wanaosemekana huwa wanashambulia mpunga shambani ukiwa kwenye hatua ya kukomaa.
Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Kilimo Kanda ya Mbeya na Arusha na Wataalamu wa Halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ambaye pia amekaimu nafasi ya Ukuu wa Wilaya Ndugu Robert Masunya, wameweza kutembelea eneo hilo Aprili 18, 2024 na kuonana na wanaanchi na kutoa ushauri ya nini kifanyike mara wakulima hao watakapoona ndege hao wakiingia shambani.
Awali taarifa za uwepo wa ndege hao ilitolea kwa Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Komredi Kheri James alipokuwa ziara katika Tarafa hiyo ya kwenda kujitambulisha kwa wananchi na kujua eneo la utawala wake.
Pamoja na ushauri uliotolewa na Wataalam hao, waliomba kupewa ushirikiano wa kutambua maeneo ambayo ndege hao huweka makazi ili wajue namna ya kutibu au kutatua changamoto hiyo.
Wanachi wameomba Wataalam hao ikiwa na Serikali kwa ujumla kufanya jitihada za haraka kuwaondoa ndege hao kwani wana hofu ya kukosa chakula na biashara kwa msimu huu wa kilimo.
Aidha Ndugu Masunya ameweza aliweza kumuongoza Katibu Tawala wa Mkoa Bi. Doris Ntuli Kalasa kutembelea Hospitali ya Wilaya iliyopo Kata ya Itunundu Kijiji cha Mbuyuni Kitongoji cha Igodikafu na kujionea huduma zitolewazo na muendelezo wa ujenzi wa baadhi ya majengo.
Pia Ndugu Masunya aliweza kutembelea Shule ya Msingi mpya ya Mseke iliyopo Kijiji cha Itunundu kujionea maendeleo ya shule hiyo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa