Watendaji Kata/Vijiji, Maafisa Tarafa Wanolewa Kiutendaji Kazi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Wakili Bashir Muhoja amewapongeza Watendaji wa Kata na vijiji wa Halmashauri hiyo kwa kuchochea maendeleo katika maeneo yao waliyopangiwa na Serikali.
Wakili Muhoja amesema hayo wakati wa kikao kazi cha watendaji wa vijiji, kata na Maafisa Tarafa kilichofanyika tarehe 01/04/2023 kwenye Ukumbi wa Siasa ni Kilimo, kuwa pamoja na changamoto mbalimbali wanazopitia kwenye maeneo yao ya kazi lakini wameonesha kuwa wana ali na kazi za utumishi wa serikali.
Kwa upande wake Afisa utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi. Beatrice Augustine kupitia wasilisho lake la mada ya Maadili ya kazi, amewahimiza viongozi kuwa mfano kwa wote, akitahadharisha juu ya unywaji holela wa pombe jambo linaloweza kuchafua taswira ya kiongozi.
Pia amewakumbusha viongozi wa vijiji, kata na tarafa kutotumia nafasi zao vibaya bali watekeleze majukumu yao kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria zilizowekwa na serikali.
Kwa niaba ya watendaji, mtendaji wa kijiji cha Migoli ndugu Majeshi Ndambo amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kwa kuitisha kikao hicho ambacho kimetoa dira ya na mustakabali mzima wa ufanyaji kazi kwa watendaji wote.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa