Watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ikiwemo wakuu wa idara na vitengo, wakuu wa shule na watendaji wa kata wapigwa msasa juu ya mfumo wa PEPMIS katika mafunzo yaliyofanyika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo Mei 22, 2024.
Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ndugu Robert Masunya amesisitiza umakini wakati wa ujifunzaji ili mwisho wa siku watumishi wote waende na njia moja “Ni vizuri wote tukawa vinara ili kama wizara inatafuta vinara basi wote tuibuke vinara” amesema.
Mafunzo yaliyotolewa yamelenga namna ya kuandaa mpango mpya wa utendaji wa taasisi, Idara, vitengo na watumishi kwa mwaka wa fedha ujao wa 2024/2025 na kwa mwaka wa kalenda 2025. Pia mafunzo yamelenga kukumbusha namna ya ujazaji wa taarifa za utendaji za kila siku za watumishi, changamoto na utatuzi wake sanjari na madirisha mengine kama uhamisho, mikopo, likizo na taarifa binafsi za mtumishi.
Mafunzo yamehudhuriwa na Mkurugenzi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Zainab Juma Kutengeza na wawezeshaji wengine ambao ni Bi. Mariam Mussa kutoka OR – Utumishi, ndg. Simon Nganyanyuka na George Sangai kutoka Ofisi ya RC Iringa
Kauli mbiu katika mafunzo haya, “Tuujenge Utumishi wa Umma Kidigitali”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa