Waziri Ummy atoa rai kwa Jamii kuheshimu na kutambua kazi za huduma ya afya zinazofanywa na wauuguzi nchini.
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa-DC)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu ametoa rai kwa jamii kutambua thamani ya kazi inayofanywa na wauguzi kote nchini.
Kauli hiyo aliitoa katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani ambayo yamefanyika kitaifa kwenye viwanja vya Kwaraa, mjini Babati, mkoani Manyara. Ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Wauguzi, Sauti inayoongoza Dira ya Huduma ya Afya.’
Waziri Ummy Mwalimu amesema ni budi kuthamini kazi ya wauguzi kwa sababu inakusisha uokoaji wa maisha ya binadamu bila kujali itikadi wala matakaba, uuguzi ni fani muhimu ambayo inapaswa kuheshimiwa na jamii.
“Nimeongea na wauguzi wa Muhimbili, MOI, JKCI na wale wa hospitali za rufaa, wote wamenieleza shida kubwa inayowakabili ni maumivu ya mgogo kutokana na kazi kubwa wanayofanya, hivyo natambua changamoto zenu na nitazifanyia kazi,” amesema Waziri Mwalimu.
Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Maadhimisho hayo yalifanyika katika Kata ya Ifunda yakiongozwa na Muuguzi Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi.Sara Mtweve ambapo wauguzi walikula kiapo cha kujikumbuha weledi katik utekelezaji wa majukumu yao ya kuhudumia jamii.
Aidha katika maadhimisho hayo Wauguzi wawili walitunukiwa vyeti ambao ni Dwilfina Ngowi ambaye alipata cheti cha pongezi kwa kusimamia na kutoa huduma znzuri za uuguzi na ukunga kwa kipindi cha mwaka 2020 na Gcecy Sembiu alipata cheti cha Nursing Ward Round.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa