WAZIRI MKUU AHIMIZA KILIMO CHA PARACHICHI IRINGA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaasa wananchi wa Iringa kufanya kilimo cha zao la parachichi kwani kwa sasa kuna fursa nzuri ya soko na soko kubwa linapatikana nchini China na India. Mhe. Majaliwa ameyasema haya alipokuwa akizungumza na wananchi katika viwanja vya Mwembetogwa Iringa Mjini Julai 08, 2024.
Mhe. Majaliwa amesisitiza kuwa uridhi mzuri kwa watoto ni kuwaachia shamba la parachichi kwani mparachichi huvunwa kwa muda wa miaka 45 hadi 50 zitamsaidia mtoto kwenye ngazi mbalimbali za kielimu hadi anapokuwa mtu mzima, hivyo wananchi wa Iringa wanapaswa kuendelea kulima zao hilo.
Aidha Mhe. Amesema kutokana na uwepo wa ndege za shirika la ATCL ni rahisi kupakia mzigo na kwenda moja kwa moja kwenye soko la parachichi bila kupata changamoto.
“Wana Iringa limeni Parachichi, soko llipo bei nzuri, usafirishaji ni bei rahisi kwa sababu tayari Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta ndege ya kubeba mizigo mnapakia mzigo wa parachichi, mnauza na kurudi nandege hiyo hiyo” amesema.
Kwa upande wa barabara Mhe. Majaliwa amesema serikali imeshakamilisha taratibu zote zinazohusu ujenzi wa barabara ya inayoenda kwenye hifadhi ya Taifa ya Ruaha (Iringa – Msembe) ikiwemo upatikanaji wa mkandarasi, barabara ambayo itajengwa kwa fedha kutoka benki ya Dunia. Wakishakagua wataalamu kutoka benki ya Dunia kazi itaanza.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amehitimisha ziara yake Mkoani Iringa ambapo amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo, kuongoza mbio za Marathoni 2024 zilizofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, kuzindua Hospitali Teule ya Tosamaganga kuwa Hospitali ya Rufaa na kuongea na wananchi katika maeneo mbalimbali.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa