Dkt. Kalemani aagiza wanaochaji gharama ya nguzo Vijijini washughulikiwe.
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano -Iringa DC)
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amesisitiza kuwa bei elekezi ya kupata nishati ya Umeme kwa vijijini ni Shilingi elfu Ishirini na saba tu (27,000),na kuwa ni kinyume na maagizo ya Serikali kuwaambia wananchi wagharamie nguzo.
Hayo aliyasema alipokuwa katika ziara ya Kikazi katika Kijiji cha Mtera kilichopo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa ambapo alikuwa ameongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira Mh Mussa Azzan Zungu wakikagua athari za mazingira katika kituo cha kufua Umeme cha Mtera kufuatia mvua kubwa zilizonyesha mwaka huu.
Mh .Dkt Kalemani alisema “tutakuwa tunajikanyaga , na hili naagiza kwa viongozi wa Tanesco wa Mkoa na Wilaya kuhakikisha mafundi na vibarua hawafanyi hivi iwapo watakiuka wafukuzeni kazi , lakini nikuombe Mkuu wa Wilaya ya Iringa usiwavumilie watumishi wanamna hii ukiwasikia wafikishe Mahakamani kwani kufanya hivi ni kuuchumu uchumi ’’alisema.
Na kuongeza “ viongozi wa serikali za vijiji suala la uingizwaji wa umeme katika Taasisi zilizopo katika maeneo yenu ni jukumu lenu kama kuna Ofisi,Shule na Zahanati simamieni suala hilo maana najua swali hili nitaulizwa’’ .
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa