Historia Yaandikwa Barabara ya Kwenda Hidadhi ya Ruaha – Zaidi ya Bilion 142 Kukamilisha Mradi Huo
Mamia ya wakazi wa Mkoa wa Iringa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Peter Serukamba Septemba 21, 2024 wameshuhudia tukio la kihistoria la utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya lami yneye urefu wa k. 104 kutoka Iringa mjini hadi Hifadhi ya Ruaha.
Barabara hiyo itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami ikiwa ni mchakato uliochukua takribani miaka 60 hadi utekelzaji wake.
Mkataba huo imewekwa kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Kampuni ya China Henan International Company Limited (CHICO), ambapo umefanyika katika viwanja vya Samora, Manispaa ya Iringa.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) amesema kuwa, mkataba huo wa ujenzi wa barabara ni mafanikio makubwa kwa Tanzania hasa katika kuinua Sekta ya Utalii na Uchumi Mkoani Iringa.
Aidha Mhe. Bashugwa amewahakikishia wananchi wanaodai fidia ya kupisha ujenzi huo kuwa watalipwa stahiki zao kwa wakati baada ya tathimini kumalizika.
Akitoa maelezo ya barabara hiyo Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohamed Besta amesema kuwa, ujenzi huo utachukua miezi 24 ukigharmu kiasi cha Shilingi Bilioni 142.56.
Akitoa salamu za Mkoa Mhe. Serukamba ametoa shukrani kwa Serikali huku akiiomba Wizara hiyo kushghulikia kwa haraka suala la fidia.
Kusainiwa kwa mkataba huo kumepongezwa na Wabunge wa Mkoa wa Iringa waliohudhuria katika hafla hiyo akiwemo William Lukuvi (Isimani), Jesca Msambatavangu (Iringa Mjini), Jackson Kiswaga (Kalenga), na Wabunge Viti Maalum Nancy Nyalusi na Rose Tweve ambao wataja kama historia kwa Mkoa huo na kusema kuwa Serikali imelipa deni kubwa kwa wananchi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa