ZAIDI YA MADAWATI 162 YATOLEWA KWA SHULE SEKONDARI YA KIDAMALI NA SHAFA AGRO COMPANY LIMITED
Shule ya sekondari Kidamali iliyopo katika Halmashuri ya Wilaya ya Iringa, mkoani Iringa, imepewa msaada wa madawati zaidi ya 162, na kampuni ya Shafa Agro Company Limited ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii inayowazunguka katika uwekezaji wao.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa madawati hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Mh. Stephen Mhapa amesema kuwa, wanathamini misaada inayotolewa na wawekezaji kwakuwa wanaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha elimu nchini.
“Tunathamini misaada mikubwa na mingi inayotolewa na kampuni hii ya Shafa Agro Limited, na ninyi mnaona kampuni hii ni ya kwenu lakini sisi kwa pamoja wananchi, wanafunzi, wazazi, na viongozi wote tunaamini kabisa kampuni hii inatuhusu kwa sababu na sisi tunafaidi matunda yake”
Aidha, Mh. Mhapa ameongeza kuwa, uwezekezaji wenye tija katika Halmashauri lazima ulindwe ili kuhakikisha unakuwa faida kwa Taifa na jamii nzima kwa ujumla ikwia ni pamoja na wanafunzi ambao wamepata madawati hayo kusoma kwa bidii.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi. Lucy Nyalu, amewashukuru na kuwapongeza wadau wa maendeleo Shafa Agro Company Limited kwa misaada yao kwani kasi waliyoanza nayo ni kubwa sana, na kuahidi kuendelea kutambua mchango wao.
Naye Mkuuu wa shule ya sekondari Kidamali amesema kuwa, mbali na kupewa viti na meza 162 vyenye thamani ya Tsh. Milioni 9,720,000/-, kampuni hiyo imefadhili walimu watano (5) wa masomo ya sayansi kwa muda wa miezi 8 sawa na Tshs. 8,000,000/-, aidha wamejenga jiko dogo la kuandalia chakula cha wanafunzi kwa Tsh. 2,500,000/- ikiwa ni pamoja na kujenga magoli ya uwanja wa mpira wa kikapu na kuahidi kufanyia kazi ombi la kufadhili miundombinu ya maji shuleni hapo.
Kwa upande mwingine viongozi wa vijiji vya Kata ya Nzihi, wanafunzi, na jamii kwa ujumla wamepokea kwa mikono miwili msaada huo na kuongeza kuwa watoto wao watakuwa katika mazingira mazuri ya kujifunzia.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa