Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alifanya ziara ya siku tatu Mkoani Iringa, na kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Wakati wa hotuba yake aliyotoa katika Uwanja wa Samora uliopo Manispaa ya Iringa alisisitiza mambo mbalimbali ikiwemo; kutambua maeneo ya malisho na kuyapima ili kupunguza migogoro ya ardhi. Kuwapatia Maafisa Ugani vitendea kazi kama pikipiki, ili kuwasaidia kuwafikia wakulima kwa urahisi.
Aidha Mh. Rais amesema, ni muhimu kuimarisha kilimo cha umwagiliaji mfano ujenzi wa skimu ili wakulima wapate kulima misimu miwili mfululizo.
Pia kwa upande wa ufugaji amesema, wananchi wananchi wafuge kwa kuzingatia kanuni za ugaji bora ili kujipatia kipato.
Kwenye suala la Utalii Mh. Rais amesema, ujenzi wa barabara kutoka Iringa kwenda Mbuga ya Ruaha itajengwa kwa kiwango cha lami ili kurahisisha wa watalii kuja kwa wingi.
Mh. Rais ameongeza kuwa, Awamu ya Pili ya Royal Tour itajikita katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Iringa ikiwemo.
Kwa upande wa Afya Mh. Raisi amesisitiza kuendelea kuboresha Hospitali ya Rufaa na ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya katika maeneo mbalimbali, bila kusahau ununuzi wa vifaa tiba.
Mh. Rais ameipongeza Mkoa wa Iringa kwa ufaulu wa Kidato cha Nne cha Kidato cha Sita. Pia amewata wanafunzi waendelee kuweka jitihada katika masomo kwa nafasi za mafunzo zipo wazi na mikopo ya elimu ya juu itatolewa kwa wakati ili kutokwamisha jitihada za wanafunzi.
Vilevile upande wa Misitu, Maliasili na Mazingira Mh. Rais ametaka Wilaya zote kuendelea kutunza misitu na kuitunza na kuzingatia upandaji miti. Pia kuanzisha kwa viwanda hasa maeneo yanayolimwa mazao ya misitu. Pia ametoa pongezi kwa Mkoa wa Iringa kwa utunzaji wa mazingira.
Aidha Mh. Rais amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya maji katika maeneo ya Ismani na Migoli, pia kutunza vyanzo mbalimbali vya maji kama Bwawa la Mtera.
Mh. Rais amesema, suala la ajira kwa vijana litaendelea kutatuliwa taratibu na kwa kusisitiza Sekta binafsi kuendelea kutoa ajira kwa vijana. Pia Serikali itaendelea kuwapa nguvu Machinga kwa kuwajengea masoko yenye miundombinu rafiki.
Pamoja na mengine yote Mh. Rais amesisitiza wananchi wajitokeze kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya watu na makazi litakaloanza tarehe 23/08/2022, kwani ni muhimu kwa maendeleo yetu.
Pia Mh. Rais ameendelea kusisitiza wananchi wote kuendelea kujikinga dhidi ya UVIKO 19.
Mwisho ametoa shukurani kwa Wanahabari kwa kuwa naye toka siku ya kwanza ya ziara hadi alipoondoka Mkoani Iringa, pia na Watumishi na wananchi wote kwa kujitokeza kumpokea na kusikiliza hotuba yake.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa