Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego pamoja na Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na baadhi ya Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa amefanya ziara katika tarafa ya Pawaga Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa sikuya tatu 18.01.2024 ambapo ameendelea kusikiliza na kutatua kero za wananchi na kuzungumza na makundi mbalimbali ya kijamii.
Pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi pia Mhe. Dendego amekutana na kuongea na viongozi wa dini mbalimbali katika tarafa ambapo amepokea maoni na kujibu baadhi ya masuala ya kijamii.
Mhe. Dendego pia ametembelea shule ya sekondari William Lukuvi na kukagua ujenzi wa nyumba za walimu, ujenzi wa vyumba vya maabara nakuweza kuongea na wanagunzi shuleni hapo. Akionge na wanafunzi Mhe. Dendego amewaasa wanafunzi kujitunza ili kuwezakufikia malengo yao ya masomo kwani serikali imeshafanya mambo mengi na makubwa kuimarisha miundombinu.
Kwa kazi kubwa zilizofanyika shuleni hapo Mhe. Dendego amewahakikishia wanafunzi pamoja na viongozi wengine kuwa shule ya sekondari William Lukuvi itapandishwa hadhi ili kuwa na kidato cha tano na cha sita.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja amesema kuwa serikali ipo tayari kufanya maboresho ikiwa ni pamoja na kukamilisha maboma ya nyumba za walimu na hata kama jamii itaamua kuanzisha maboma mengine serikali itakuwa tayari kuyapokea na kumalizia.
Kwa upande wa tarafa ya pawaga ziara hii imehitimishwa na itaendelea kwenye maeneo mengine hasa yale ya pembezoni ambayo kwa sehemu kubwa huwa hayafikiwi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa