Ujenzi wa vyoo matundu saba Zahanati ya Mikongwi Kijiji chaMokongwi Kata ya Kihorogota. Ujenzi ulianza tarehe 5/08/2022. Jumla ya fedhailiyotolewa ya ujenzi wa vyoo ni Milioni 24.2, nguvu ya wananchi ni Tshs.Milioni 4.2 na kufanya jumla kuwa Tshs. Milioni 28.4.
Ujenzi wa Zahanati ya Kinywang'anga iliyopo Kata ya Kising'a ujenzi umehusisha jengo la zahanati, vyoo na nguzo za kuwekea tenki la maji, ujenzi umekamilika kwa asilimia tisini na tisa 99%.
Ujenzi wa Kituo cha Afya Kiwele, ujenzi huu umehusisha majengo ya wazazi na upasuaji, jengo la kufulia, jengo la kuchomea taka na jengo la OPD. Ujenzi umefikia 60%. na ujenzi unategemewa kukamilika tarehe 2/11/2022.
Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Igodikafu uliohusisha jengola kuhifadhia maiti, jengo la dharura, Nyumba ya Mtumishi na jengo la upasuaji.
Ujenzi wa shule ya sekondari Mlenge kiasi cha Tshs milioni 470 zimepokelewa, jumla ya fedha zilizotumika ni Tshs milioni 450, ujenzi bado unaendelea na umefikia 75%.
Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa unaotekelezwa katika Katika Kata ya Ifunda Kijiji cha Mgama, ambao utagharimu kiasi cha Bilioni 3 (3bin). mpaka sasa jumla ya fedha za mradi zilizopokelewa ni bilioni 2 (2bn) na Mradi umekamilika kwa asilimia 80. (80%).
Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kibena unaotekelezwa katika Kata ya Kibena, Gharama za mradi ni Milioni 700 (700 Mln). Jumla ya fedha zilizopokelewa ni Milioni 500 (500Mln) na Mradi umekamilika kwa asilimia 95 (95%).
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa