Kamati ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Ndugu Yahya Kiliwasha, imefanya ziara kukagua miradi ya maendeleo kwa Robo ya Nne kwa mwaka wa Fedha 2024/2025.
Ziara hiyo imefanyika siku ya Jumamosi Juni 15, kwa kukaguliwa ni pamoja na shamba la maparachichi na mabwa ya samaki vyote vikiwa katika Kata ya Mgama Kijiji.
Miradi hiyo iliksudiwa kufanyika kwa tija ili kuipatia Halmashauri mapato japo kumekuwa na changamoto chache katika miradi hiyo.
Changomoto za kuchelewa kukamilisha miradi ikiwa ni ufinyu wa bajeti imepelekea kutofikia lengo katika miradi hiyo hasa upande wa mabwawa kwa kuchelewa kumaliza ujenzi wa mabwawa hayo. Pia kutosafisha chamba la maparachichi kwa wakati kupelekea miti hiyo kutostawi vizuri.
Kamati imetoa maagizo ya kuwa, bajeti ijayo ya mwaka wa Fedha 2025/2026 iongeizwe kwa ajili ya umaliziaji wa mabwawa na usafishaji wa shamba hilo kubwa lenye maparachichi
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa