Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango imefanya ziara Juni 19 kwa kukagua miradi. Mradi uliokagulia ni Bomalang’ombe Village Company (BVC) uliopo Wilaya ya Kilolo, ambao ulianzishwa na Shirika la CEFA kutoka Italy mwaka 1994, na kwamba wakati huo bado Wilaya ya Kilolo haijaanzishwa.
Kamati imetembelea mradi huo na kubaini mambo mbalimbali hayajakaa sawa hivyo kutoa maagizo kwa Mkurugenzi Mtendaji kuyafanyia kazi haraka ili mradi uweze kufanya tena kazi, kwani ulisimama uzalishaji baada ya kugawanywa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na Kilolo, na Taasisi ya CEFA kukabidhi mradi kwa Kijiji cha Bomalang’ombe .
Baadhi ya mali zilizokabidhiwa katika Kijiji cha Bomalang’ombe ni pamoja na shule ya chekechea, mradi wa uzalishaji umeme, mifumo ya maji, jengo la ukumbi, pia kuna karakana ya utengenezaji wa magari, kiwanda cha kusindika soseji, mabanda ya ufugaji wa ng’mbe na nguruwe, jengo la Utawala, baadhi ya magari japo ni mabovu na shamba la miti lenye ukubwa wa ekari 432.
Kamati imeagiza mambo yafuatayo; mali zilizopo ziendelee kusimamiwa vizuri na Meneja aliyekuwepo tangu kiwanda kinaanza, isitoke mali yoyote bila taarifa na kwamba mali zilizopo zibaki kama zilivyo hadi pale maamuzi yatakapotolewa, kwani bado mazungumzo yanafanyika kwa Kilolo na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa juu ya uboreshaji wa mradi huo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa