MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA ATETA NA WATUMISHI
Aonya juu ya suala la rushwa kwa watumishi wa umma
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ndugu Robert Masunya azungumza na watumishi wa Halmashauri kupitia kikao cha robo ya pili cha watumishi kilichofanyika Februari 12, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri uliopo makao makuu Ihemi.
Ndugu Robert Masunya amewatahadharisha watumishi wa umma wanaofanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kujiepusha na masuala yote ya rushwa kwani sio tu rushwa ina madhara kwa mtumishi bali pia kwa watu wengine amba oni tegemezi kwa mtumishi husika.
Aidha ndugu Masunya amesisitiza juu ya ushirikiano wa watumishi katika utendaji na kuwataka kufanya kazi kama timu huku kila mtumishi akilenga kutimiza wajibu wake kwa uaminifu na kwamba kila mmoja aone kwamba ana mchango kwenye taasisi na hatimaye Iringa DC kuwa kimbilio la wengi.
“Niombe na kusisitiza kwamba kila mtu atimize wajibu wake, tukitimiza wajibu wetu kila mmoja atamheshimu mwenzake, team work itakuja na hatimaye kutoa mafanikio ambayo yanaonesha elimu ya msingi imebadilika na sasa inaelekea inakotakiwa Kwenda”
Katika kikao hiki watumishi wamepata fursa ya kupitishwa kwenye maada mbalimbali ikiwa ni Pamoja na madhara na kujikinga na ugojwa wa kisukari, UKIMWI, mapitio ya sheria ya Utumishi wa Umma, Maadili na masuala ya kiutumishi sanyari na maada ya rushwa
Lengo la kikao hiki cha watumishi ni kuongeza uwajibikaji kupitia taarifa muhimu wanazopatiwa watumishi na fursa ya kukumbushwa masuala muhimu ya kuzingatika katika utumishi wa umma.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa