WASTAAFU WAASWA KUENDELEA KUTOA UZOEFU WAO KATIKA KUJENGA JAMII BORA
Wapongezwa kwa kazi nzuri na ya kizalendo waliyoifanya wakati wa utumishi wao
Wastaafu waaswa kuendelea kutoa mchango wa uzoefu wao walioupata walipokuwa watumishi wa umma ili kuendelea kuijenga jamii bora na endelevu. Hayo yamezungumzwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ndugu Christian Ndenga wakati wa Hafla ya kuwaaga wastaafu wa Idara ya Kilimo Februari 08, 2025 iliyofanyka katika ukumbi wa Gentle Hills Mjini Iringa.
“Mlihitimu kutoka kwenye kazi rasmi, nafasi yenu katika jamii haipungui. Uzoefu wenu ni rasilimali ambayo inapaswa kuhifadhiwa na kushirikiwa. Tunawahimiza kushiriki katika shughuli za kijamii, kuendelea kutoa ushauri na kuwa washauri wa busara kwa wale walio kwenye hatua za mwanzo za utumishi” Amesema ndugu Ndenga.
Aidha ndugu Ndenga amewapongeza wastaafu kwa utumishi wao walioutoa kwenye Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kutoa masuluhisho kwenye masuala mbalimbali na kutoa wito kwa watumishi wanaobaki kuendelea kuwa mfano wa uadilifu na usimamizi bora ili kuifanya Iringa kuwa mahali pa maendeleo na fursa kwa wote.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa