Ukanda huu una mwinuko wa meta 900 – 1,200 kutoka usawa wa bahari, hupata mvua chache kiasi cha mm 500 – 600 kwa mwaka na kiwngo cha joto ni kati ya 20 °c – 30 °c.
Ukanda huu unajumuisha maeneo ya Tarafa za Pawaga, Idodi na Isimani. Mazao yanayoliwa ni pamoja na mahindi, mpunga, vitunguu, nyanya, ndizi, karanga, pamba, mtama, mhogo, maembe, machungwa, korosho, mapapai, ufuta na viazi vitamu.
2.2. UKANDA WA KATI:
Ukanda huu una mwinuko wa meta 1,200 – 1,600 kutoka usawa wa bahari, hupata mvua za wastani na juu ya wastani mm 600 – 1,000 kwa mwaka na kiwango cha joto ni kati ya 15 °c – 20 °c.
Ukanda huu unajumuisha maeneo ya Tarafa za Mlolo, Kalenga, Kiponzelo na Kata za Kising’a na Kihorogota katika Tarafa ya Isimani. Mazao yanayolimwa ni tumbaku, alizeti, kabeji, ngano, soya, mahindi, pamba nyanya, viazi vitamu, viazi mviringo, maharage, ufuta, mboga na matunda. Mazao mengine yanayoweza kustawi ni kahawa, pareto na njegere.