Idara ya ujenzi katika halmashauri ya wilaya ya Iringa ina mtandao wa barabara wenye jumla ya Km 1323.93. Kati ya hizo barabara kuna Km 7 ni barabara za lami sawa na 0.5%, Km 986.33 sawa na 74.5% ni za changarawe na jumla ya Km 330.60 sawa na 25% ni za udongo. Barabara za changarawe na lami hupitika vizuri karibu kwa 90% katika vipindi vyote vya mwaka lakini barabara za udongo hupitika kwa shida katika wakati wa mvua.
Pia idara inahusika moja kwa moja katika ujenzi na ukarabati wa majengo mbalimbali ya idara mbalimbali kaika halmashauri kwa kuhakikisha majengo hayo hayahatarishi maisha ya watumiaji.
Majukumu makuu ya idara ya ujenzi ni kuhakikisha barabara zote zinapitika mwaka mzima kwa kufanya matengenezo ya barabara hizo kulingana na bajeti. Katika hilo idara inajukumu kuu la kuhakikisha kuwa wakandarasi wanaoshinda zabuni za barabara na majengo wanatekeleza kazi husika kwa ubora na viwango kulingana na mikataba yao.
Ili kuweza kutekeleza majukumu ya kila siku ya Idara ya ujenzi, idara ina muundo halisi wa idara unaoundwa na watumishi mbalimbali. Muundo wa idara ya ujenzi upo kama hivi, Kiongozi mkuu ni mkuu wa idara na chiniyake kuna vitengo vikuu viwili ambavyo ni Kitengo cha Barabara na Kitengo cha Majengo. Kila kitengo kina mkuu wa kitengo na kuwa na wahandisi pamoja na mafundi sanifu ili kuweza kutekeleza kazi katika vitengo hivyo. Idara ina jumla ya wahandisi watatu akiwemo mkuu wa idara, mkadiriaji majengo (QS) mmoja, mafundi sanifu saba. Pia idara ina katibu muktasi mmoja na muhudumu mmoja. Timu hii ya wataalamu kwa pamoja ndio wanaowezasha idara kuweza kutimiza majukumu ya idara ya kila siku na kuleta jija katika mkoa na taifa kwa ujumla.
Ujenzi wa barabara hii katika kiwango cha lami unatoka na ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya (EU) katika halmashauri yetu. Mradi huu upo katika utekelezaji kwa sasa na kuwa na unagharimu (є): 5,919,667.85 ambazo ni sawa karibu na TZS: 14,799,169,625.00.
Barabara hii inajengwa na kuwekwa lami njia moja yaani (single lane) kutokana na idadi ya watumiaji wa barabara hii. Barabara hii ikikamilika itawawezesha wananchi kusafirisha mazao yao na bidhaaa zinginezo kwa urahisi zaidi katika kipindi chote cha mwaka tofauti na hapo awali ambapo ikifika wakati wa mfua barabara hii ilikuwa ikipitika kwa shida. Ujengwaji wa barabara hii itapunguza pia gharama za usafirishaji na pia kuviinua vijiji vilivyo kandokando ya barabara hii. Vilevile barabara hii itawafanya wananchi waweze kufikia huduma muhimu kirahisi kwa jamii husika hasa za afya na elimu kwa watoto.
Ujenzi wa barabara hii katika kiwango cha changalawe unatoka katika mfuko wa barabara wa Taifa. Mradi huu upo katika utekelezaji kwa sasa na kuwa na unagharimu TZS: 668,022,300.00 utakapokamilika.
Barabara hii inajengwa kwa kiwango cha changalawe lakini ni barabara ambayo imechokwa kwa kilomita 7 mfululizo na kuinua kuinuwa tuta lake. Barabara hii ikikamilika itawawezesha wananchi kusafirisha mazao yao na bidhaaa zinginezo kwa urahisi zaidi kutoka kijiji cha Kisanga na kupeleka katika kijiji cha Itunundu na hatimaye mjini katika kipindi chote cha mwaka tofauti na hapo awali ambapo ikifika wakati wa mfua barabara hii ilikuwa ikipitika kwa shida na wananchi walikua wakizunguka na kupita njia ya Kinyika ambayo ni ndefu. Ujengwaji wa barabara hii itapunguza pia gharama za usafirishaji na pia kuwezesha barabara ya kuingia katika gereza la Itunundu kuwa nzuri na yenye kupitika mwaka mzimz. Vilevile barabara hii itawafanya wananchi waweze kufikia huduma muhimu kirahisi kwa jamii husika hasa za afya katika hospitali ya pawaga na elimu kwa watoto.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa