IDARA YA ARDHI MALIASILI
Idara ya Ardhi na Maliasili ni mojawapo ya Idara za Halmashauri za Wilaya ya Iringa. Idara hii inaundwa na jumla ya vitengo vidogo saba (7) chini ya sekta za Ardhi na Maliasili ambavyo ni: (i) Mipango Miji (ii) Usimamizi wa Ardhi (iii) Upimaji na Ramani (iv) Uthamini wa mali (v) Misitu (vi) Wanyamapori (vii) UtaliiIdara ya Ardhi na Maliasili ina jumla ya Watumishi 22.
MAJUKUMU YA IDARA YA ARDHI NA MALIASILI
Kwa ujumla majukumu ya Idara ya Ardhi na Maliasili ni ya kutoa huduma za kitaalam na ushauri kwa wakazi wa eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, wananchi wengine wa Tanzania na wawekezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Majukumu hayo ni kama ifuatavyo:
WANYAMAPORI NA UTALII KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA
Katika Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ni maarufu kwa wanyamapori na vivutio mbalimbali vya utalii kama ifutavyo;
VIVUTIO MBALIMBALI VYA UTALII KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA
Makumbusho ya Mtwa Mkwawa Tarafa ya Kalenga.
Hili ni jengo la Makumbusho ya Mtwa Mkwawa lililopo katika kijiji cha Kalenga. Eneo hili linalopatikana umbali wa Km 15 kutoka Iringa mjini. Eneo .Kalenga ndiyo asili ya MAisha ya Kiutawala ya Mtwa Mkwawa. Katika jengo hili kichwa cha Mtwa mkwawa aliyetawala 1855-1898 kimehifadhiwa. Pia Mtalii utapata historia ya utawala wa Mtwa Mkwawa na Kabila la Wahehe.
Kielelezo Na 1.Makumbusho ya Kalenga katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Pango la Masalia ya Binadamu Magubike
Kielelezo Na 2 Eneo la Mapango ya Magubike eneo lenye masalia ya binadamu wa kale na zana za chuma
Magubike ni pango lililopo katika Kilima katika kijiji cha Mugabike Halmashauri ya Iringa .Kuna sehemu mbili ambazo zimetapakaa masalia ya muhula wa chuma ,zana za mawe zinazoonekana katika maeneo yenye mmonyoko wa ardhi zana za muhula wa kati zinaonekana wazi katika mteremko chini ya pango kwenye shamba la tumbaku.
Pango la Magubike yamepatikana masalia ya muhula wa chuma,, kulikuwa na masalia ya zana za muhula wa chuma na masalia ya zana za Miuhula wa kati. na masalia ya mifupa ya wanyama mbalimbali, konokono ( Genus Achatina), na vipande 6.5 vya meno ya binadamu wa kale ( Homo sapiens) aliyeishi kipindi cha miaka 50,000 hadi 200,000 iliyopita Umri halisi wa masalia ya binadamu na masalia mengine utapatikana baada ya kukamilisha utafiti .Meno haya ni ya binadamu wa mwanzo aliyefanana kimaumbile kama binadamu wa sasa.
Mapango ya Mlambalasi (Mlambalasi Rockshelter)
Mlambalasi ipo umbali wa km 50 magharibi mwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Njia iendayo Hifadhi ya Ruaha. Mlambalasi ni eneo alilozikwa Mtwa Mkwawa, Mtemi wa kabila la Wahehe katika karne ya 19. Pango hili lipo juu ya eneo la makaburi na lina sehemu kuu 2. Katika sehemu zote mbili kuna mtawanyiko mkubwa wa zana za muhula wa chuma na za kihistoria. Sehemu ya kwanza,yalipatikana masalia ya kihistoria ya muhula wa chuma, vyungu na zana za mawe za muhula wa mwisho zilichanganyikana na masalia ya chuma.
Kielelezo Na 3 Pango la Mlambalasi ambalo lilitumiwa na Mtwa MKwawa Kiongozi wa Kabila la Wahehe
Chemchemi ya Maji moto Kikongoma
Hili ni eneo lililopo km 16 kutoka mji mdogo wa Kalenga katika kijiji cha Kalenga. Eneo hili hutembelewa na watalii wengi kwa ajili ya kunawa maji ya moto. Maji haya huaminika kuwa ni maji ya Baraka, ambayo mtu akiyatumia mikosi na matatizo mbalimbali katika maisha yanaisha. Waganga Mbalimbali wa tiba za asili hutumia maji haya kwa ajili ya tiba. Hiii ni chemchem ambayo maji yake hayaongezeki wala kukauka.
Kielelezo Na 2 Sehemu ya Majimoto KIkongoma katika kijiji cha Mangalali sehemu ambayo hutembelewa na watalii Wengi
Daraja la Mungu Kikongoma – Mangalali
Hili ni eneo ambalo ni mojawapo ya vivutio vya utalii katika Halmashauri kivutio cha utalii. Katika eneo hili Mto Raha Ndogo hupotea na mita baada ya mita 53 kuibuka. Daraja linalofunika mto huu ni mawe yenye rangi mbalimbali za kuvutia ambayo yamepangwa kwa asili na kufanya sauti nzuri za maporomoko ya maji ya Mto ruaha ndogo. Eneo hili ndiko alikofia Mama yake na Mkwawa akipinga kutoa siri ya nguvu ya utawala utawala wa mwanae Mtwa Mkwawa.
Kielelezo Na 5 Daraja la Mungu Kikongoma katika kijiji cha Mangalali
Maeneo kwa ajili ya Utalii wa Kutembea
Halmashauri ya wilaya ya Iringa imejaliwaa kuwa na utajiri wa mazingira mazuri yenye mvuto na salama kwa ajili ya utalii wa kutembea kama vile kutembelea milima, Mawe na misitu mbalimbali ya asili. Hili ni eneo la Igangidungu Katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Hili ni jiwe kubwa lenye mvuto wa rangi mbalimbali ambalo huvutia wageni wengi kutembelea na kupiga picha
Kielelezo 6 Jiwe lililopo katika kijiji cha Igangidung’u kwa utalii wa kutembea
Utalii wa kuona Wanyama
Utalii wa wanyama katika maeneo ya mapori ya Jumuia za wanyamapori zinazozunguka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha. Utalii unaofanyika katika maeneo haya ni utalii wa kuona, kutembea na Utalii wa picha. Hifadhi ya RAha ipo umbali wa Km 146 kutoka Iringa Mjini .
Kielelezo7 Wamyama aina ya swala wanapatikana katika Hifadhi ya Ruaha na jumuiya za wanyamapori MBOMIPA- Iringa
IDARA YA ARDHI,NA MIPANGO MIJI
Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ni mojawapo ya Idara za Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Idara hii inaundwa na jumla ya vitengo vidogo nane (7) chini ya sekta za Ardhi na Maliasili ambavyo ni: (i) Mipango Miji (ii) Usimamizi wa Ardhi (iii) Upimaji na Ramani (iv) Uthamini wa mali (v) Misitu (vi) Wanyamapori (vii) Utalii
Idara ya Ardhi na Maliasili ina jumla ya Watumishi 27.
MAJUKUMU YA IDARA YA ARDHI NA MALIASILI
Kwa ujumla majukumu ya Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ni ya kutoa huduma za kitaalam na ushauri kwa wakazi wa eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, wananchi wengine wa Tanzania na wawekezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Majukumu hayo ni kama ifuatavyo:
Kudhibiti uvunaji holela wa maliasili mbalimbali kama vile misitu na wanyamapori.
WANYAMAPORI NA UTALII KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA
Katika Ukanda ya Nyanda za Juu Kusini, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ni maarufu kwa wanyamapori na vivutio mbalimbali vya utalii kama ifutavyo;
PICHA ZA WANYAMA NA NDEGE MBALIMBALI
Tembo (Elephant -Loxodonta africana) wa Iringa ni wakubwa na wanapatikana kwa wingi katika eneo moja kuliko eneo lingine lolote la Afrika Mashariki.
Mbwa mwitu (Wild dog), ni mnyamapori aliyehatarini kutoweka pia anapatikana katika maeneo yetu ya Hifadhi. Hatari hii ya kutoweka inatokana na ujangili na kupungua kwa maeneo ya hifadhi kwa kuwa wanaishi kwenye kundi kubwa, hivyo wanahitaji wanahitaji eneo kubwa la hifadhi. Pia wanauawa na simba, fisi na wafugaji)
Tandala wakubwa dume na jike Tandala mdogo jike na watoto
Korongo (Roan Antelope) Palahala/Mbalapi (Sable antelope)
Maeneo ya hifadhi ya Iringa ni maeneo pekee kwa kuwa na wingi wa Tandala wakubwa (Greater Kudu), Tandala wadogo (Lesser Kudu), Palahala/Mbalapi (sable Antelope) na Korongo (Roan antelope).
Simba dume wakinywa maji
Simba jike na watoto wake kama walivyoonekana kwenye eneo la MBOMIPA
Chui wanaopatikana katika Hifadhi ya Ruaha
Viboko wanapatikana katika bwawa la Mtera
Ramani ya Hifadhi za wanyama katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa
VIVUTIO MBALIMBALI VYA UTALII KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA
Pamoja na wanyamapori, vipo vivutio mbalimbali vya utalii kama vile Nguzo za Asili (Natural Pillars) za Isimila, Daraja la Mungu na Maji ya Moto ya Kikongoma, Mapango ya Mlambalasi alikojificha Chifu Mkwawa wakati alipopambana na Wajerumani, Zana za Kale katika eneo la Isimila, Jengo la Makumbusho ya Mtwa Mkwawa Kalenga, Ngome ya Chifu Mkwawa katika eneo la Kalenga nk.
PICHA ZA VIVUTIO VYA UTALII
Daraja la Mungu la Kikongoma,
Eneo hili linalojulikana kama jiwe jeusi linapatikana kwenye kijiji cha Mangalali Kata ya Ulanda katika barabara kuu itokayo Iringa mjini kuelekea hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Ni eneo ambalo mama yake Chifu Mkwawa aliyeitwa Sengimba alijiua baada ya kupata taarifa kuwa mwanawe Mkwawa amekamatwa na wajerumani.
Katika eneo hili mto Ruaha mdogo unazama ardhini umbali wa mita zaidi ya 100 na kutengeneza daraja la asili linalojulikana kama daraja la Mungu. Jirani na eneo hili kuna chemi chem ya maji moto na eneo la matambiko.
Eneo hili linafaa kwa utalii wa picha na ujenzi wa kambi za muda, changamoto iliyopo ni kutofikika kwa urahisi kutokana na ubovu wa barabara
Pillars za Ismila
Minara hii inapatikana nje kidogo ya kituo cha kihistoria cha Isimila.
Minara hii ni kivutio kizuri cha utalii.
Katika eneo hili zama za kati na za mwisho zinapatikana.
Eneo hili linahitaji kutangazwa zaidi kama kivutio cha utalii cha kihistoria
Fuvu la Mkwawa
Mkwawa alizaliwa mwaka 1855 na kufa mwaka 1898, Fuvu la mtwa Mkwawa lilipelekwa Ujerumani mwaka 1898 lilirudishwa na Wajerumani mwaka 17/06/1954 na kuwekwa kwenye Kituo cha Makumbusho Kalenga kilichopo kijiji cha Kalenga kata ya Ulanda umbali wa kilometa 10 toka Iringa Mjini.
Kituo hiki kinamilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii - Idara ya mambo kale.
Katika Kijiji hiki Halmashauri imeanzisha kikundi cha utalii wa kiutamaduni wa wahehe.
Ngoma za kimila kama mbayaya, mangala na kiduo pia zinapatikana.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa