Wizara ya Afya kupitia Ofisi ya Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Taasisi ga USAID Afya Yangu, imetoa mwongozo wa Uundaji wa Kamati za Kudhibiti UKIMWI.
Tukio hilo limefanyika Agosti 05, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri uliopo Ihemi.
Akifungua kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Hlamashauri ya Wilaya ya Iringa Ndugu Robert Masunya amesema, "mwongozo huu unakubalika hivyo ufanyiwe kazi kwa kadri inavyotakiwa, ili Wanakamati waweze kutekeleza majukumu yao kwa namna inavyotakiwa".
Akitoa na kuelezea Uundwaji wa Kamati Afisa Maendeleo Bi. Keshia Witete, ambaye amemuwakilisha Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa amesisitiza na kusema "Pamoja na mambo mengine Kamati zinatakiwa kuweka agenda za kudumu katika vikao vyao, ili kuendelea kutoa elimu na hamasa.
Naye Mwakilishi wa USAID Afya Yangu Ndugu Francis Makulla Mshauri Mabadiliko ya Tabia Katika Jamii amewashukuru Wajumbe kwa kuhudhuria kikao na kujifunza namna Kamati zinavyotakiwa kuwa.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa