• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe Za Watumishi |
Iringa District Council
Iringa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu sekondari
      • Elimu Msingi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo umwagiliaji na ushirika
      • Mazingira na Usafishaji
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA NA Uhusiano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipango,Utawala na Uchumi
      • UKIMWI
      • Afya Elimu na Maji
      • UMazingira, uchumi na Ujenzi
      • Maadili
    • Ratiba Ya Vikao mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Hudumakwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video za Shughuli Mbalimbali za kiofisi na za Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Idara ya Maendeleo ya Jamii

1.0 UTANGULIZI WA IDARA 

Idara ya maendeleo ya jamii ni mojawapo ya Idara 11 zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.  Idara ngazi ya wilaya ina Madawati 4 ambayo ni (i)Utafiti, mipango na Takwimu (ii) Jinsia (iii) Watoto (iv) Ufundi na ujenzi.vilevile katika ngazi ya Halmashauri  Pia Idara inaratibu miradi ya Mfuko wa maendeleo ya jamii ( TASAF), Mapambano dhidi   UKIMWI, UNICEF– Malezi na mkuzi ya mtoto (Parenting) na Watoto walio katika mazingira Hatarishi.  Mfuko wa afya ya jamii (CHF). Uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kupitia Mfuko wa vijana (YDF) na Mfuko wa Wanawake (WDF) na Uratibu wa asasi za kiraia (CBOs/NGOs/FBOs). idadi ya watumishi waliopo ni 40 ambapo makao makuu ya willaya kuna watumishi  8(me 3 ke 5) kati yao watumishi wawili wako shule, upungufu wa mtaalam 1 wa ufundi na ujenzi, ngazi ya kata watumishi 29 (me 7 ke 22) kati yao watumishi 4 wako shule, ngazi ya vijiji ina watumishi wa 4 (ke 4, me 0).

2,0 TAFSIRI YA MAENDELEO YA JAMII.

Maendeleo ya Jamii hutafsiriwa na makundi tofauti kutegemea na mahali walipo na maana zote ni sahihi. Tofauti katika Tafsiri hutokana na hatua za maendeleo zilizofikiwa na maelezo yanayotolewa na wataalam kulingana na desturi, wanachopendelea na falsafa yao. Ili kujenga uelewa wa dhana ya maendeleo ya jamii katika maelezo yanayotolewa katika kipeperushi hiki, Maendeleo ya Jamii ni  hatua zinazowawezesha  watu kutambua uwezo walio nao wa kubaini matatizo na uwezo wao  wa kutumia rasilimali zilizopo kujipatia na kujiongezea kipato cha kujiletea maisha bora.

3.0 TOFAUTI KATI YA MAENDELEO YA JAMII NA USTAWI WA JAMII 

Maendeleo ya Jamii ni hatua zinazowawezesha   watu kutambua uwezo walio nao wa kubaini matatizo na uwezo wao wa kutumia rasilimali zilizopo kujipatia na kujiongezea kipato cha kujiletea maisha bora.

Ustawi wa jamii mchakato wa kuwasaidia watu ambao wanauhitaji wa huduma za kijamii, kiuchumi na kisaikolojia.

4.0 HISTORIA YA MAENDELEO YA JAMII (HISTORY OF COMMUNITY DEVELOPMENT)

Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini Tanzania imekuwa ikibadilika kutokana na mabadiliko yaliyojitokeza duniani kama ifuatavyo:

  • Ilianzishwa mwaka 1945 ikiitwa ustawi wa Jamii ili kuwasaidia wahanga wa vita kuu ya pili ili wawe sehemu ya Jamii.
  • Mwaka 1952 ilibadilika kuwa Maendeleo ya Kijamii (social development) iliendelea kuwasaidia wahanga wa vita na utoaji wa huduma za jamii mijini.
  • Mwaka 1961 ilibadilika kuwa Maendeleo ya Jamii na Utamaduni ambapo iliendelea kutoa huduma za jamii na kusaidia Jamii kurejesha utamaduni wa kitanzania ulioingiliwa na tamaduni za kigeni.
  • Mwaka 1967 ilibadilika kuwa maendeleo vijijini msisitizo ukiwa ni kupeleka huduma za jamii maeneo ya vijijini yaliyosahaulika.
  • Mwaka 1974 ilibadilika kuwa Ujamaa na Ushirika msitizo ikiwa kuishi pamoja na kujitegemea.
  • Mwaka 1981 ilibadilika na kuwa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto, msisitizo maendeleo ya jamii kwa watu maskini na makundi tete ya wanawake na watoto.
  • Mwaka 2005  - 2010 ilimebadilika na kuwa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, msisitizo maendeleo kwa watu maskini yenye uwiano wa ushiriki wa wanawake na wanaume
  • Mwaka 2016 imebadilika na kuwa wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia  wazee na watoto

5.0 FALSAFA

Maendeleo endelevu ni yale yanayoletwa na watu wenyewe kwa njia ya kujitegemea na kushirikiana. Msisitizo upo kwenye ushirikishwaji jamii katika masuala yanayogusa maisha yao.

6.0 WALENGWA WA SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII

 

Walengwa wa sekta ya Maendeleo ya Jamii ni maskini wa Maskini (Poor of poor) na Makundi yaliyosahaulika katika jamii wanawake, watoto, vijana, wazee, na walemavu

Communty development Beneficiaries is the poorest of the poor and disadvantaged groups in society such as women, children, youth, elderly, and disabled.

7.0 MAJUKUMU YA IDARA:

Jukumu Kuu

Ni kusaidia watu kubadili fikra, imani, utamaduni, mila na desturi kutoka zile za zamani zilizopitwa na wakati kuwa zile zenye mwelekeo wa maendeleo.

Majukumu Mahsusi

Majukumu mahsusi yatahusisha:

  • Kuziwezesha jamii kuondokana na fikra, imani, desturi na utamaduni unaokinzana na maendeleo.
  • Kuziwezesha jamii kutambua fursa walizonazo ili kutatua vikwazo vya maendeleo (mipango shirikishi).
  • Kuwezesha jamii kuibua, kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathimini miradi ya maendeleo na shughuli za kujitegemea.
  • Kujenga uwezo wa Halmashauri na vijiji juu ya utawala bora, upangaji mipango shirikishi na bajeti.
  • Kuwezesha Halmashauri na vijiji kuingiza masuala ya jinsia katika mipango na bajeti na kutekeleza.
  • Kutambua, kuunda na kutoa mafunzo kwa vikosi vya ujenzi ili waweze kujiajiri na kuanzisha shughuli za kuongeza kipato.
  • Kuwezesha uanzishaji na kujenga uwezo wa vikundi vya uzalishaji mali kwenye ngazi ya jamii ili kujiajiri na kuongeza kipato.
  • Kufanya tafiti na tafiti shirikishi ili kubaini vikwazo vya maendeleo katika Halmashauri na matokeo yake kutumika katika maamuzi ya maendeleo
  • Kueleimisha jamii kuingiza masuala mtambuka katika mipango na shughuli za maendeleo kama usafi wa mazingira, mapambano dhidi ya UKIMWI, Mapambano dhidi ya rushwa na Jinsia.
  • Kutafsiri na kuelimisha jamii sera mbali mbali na mikakati

Matokeo Muhimu (Key Results)

  • Jamii kuwajibika na masuala yanayogusa maisha yao kwa kutambua changamoto zinazowakabili, kupendekeza suluhisho na kutekeleza (Mipango shirikishi)
  • Uwepo wa viongozi wa vijiji na kata wanaofanya kazi zao kwa kuzingatia utawala bora.

 8.0 MADAWATI YALIYOPO NGAZI YA WILAYA 

8.1 Dawati la Jinsia (Gender desk)

Idara imenzisha dawati la jinsia kwa mujibu wa mwongozo Wizara ya  afya maendeleo ya jamii jinsia  wazee and  na watoto  unalekeza kila taasisi au sekta kuwa na dawati la Jinsia. Kwa Halmashauri ya Iringa dawati la jinsia limeanzishwa mwaka 2008 baada ya mabadiliko ya lililokuwa dawati la wanawake na watoto. Mabadiliko haya yanaenda sambamba na msisitizo wa mkakati na mpango ujulikanao kama “Wanawake katika Maendeleo” (WID) wa kuwawezsha wanawake kushiriki katika shughuli za maendeleo uliokuwepo 1970 hadi 1992 na kubadilika kuwa  “Jinsia na Maendeleo” (GAD)

Malengo ya Dawati

  • Kuhakikisha kuwa masuala ya jinsia katika Halmashauri yanatambuliwa kwa kufanya uchambuzi wa jinsia (gender analysis).
  • Kuhakikisha masuala ya jinsia yanaingizwa katika mipango ya vijiji na Halmashauri  (gender mainstreaming) kwa Ujumla na kutekelezwa
  • Kujenga uelewa miongoni mwa wakuu  wa idara, wakuu wa vitengo na madiwani juu ya umuhimu wa kufanyia kazi mapengo ya jinsia ili kuleta haki na usawa wa kijinsi

Majukumu ya Dawati

  • Kuratibu ukusanyaji wa takwimu za mchanganuo wa kijinsia (Gender Disaggregated Data)
  • Kuwezesha zoezi la uchambuzi wa masuala ya jinsia
  • Kuratibu utapatikanaji wa wawakilishi wa jinsia wa sekta
  • Kuratibu uingizwaji wa masuala ya jinsia katika mpango na bajeti ya Halmashauri
  • kuwezesha mafunzo mbali mbali ya jinsia kwa kadriri ya mahitaji
  • Kutoa rufaa kwa wahanga wa ukatili wa jinsia (ustawi wa jamii, polisi, wanasheria na hospitali).
  • Kufanya ukaguzi shirikishi wa masuala ya jinsia (participatory gender audit)
  • Kuratibu kazi zinazofanywa na wadau wa masuala ya Jinsia

Afua (Interventions)

  • Uchambuzi na ukusanyaji wa takwimu za kijinsia
  • Mijadala ya kijinsia (warsha, makongamano, mafunzo na mikutano)
  • Uanzishwaji wa vikundi vya ujasiarimali
  • Uwezeshwaji wa mitaji (VICOBA, Mikopo ya Wanawake na Vijana)
  • Uanzishwaji na uendelezaji wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana ili kumpa fursa mwanamke kufanya kazi za uzalishaji na uongozi.
  • Uenezaji wa teknolojia rahisi na sahihi za kurahisisha mzigo wa kazi (mf. Majiko sanifu, mashine  za kukausha mboga, mashine za kupukuchua mahindi, mikokoteni na wanyamakazi).

 Matokeo Muhimu (Key Results)

  • Uwepo wa Takwimu za mchanganuo wa Jinsia
  • Uwepo wa wawakilishi wa madawati ya jinsia ya sekta
  • Uwepo wa taarifa za ukaguzi wa jinsia (gender audit)
  • Uwepo wa mikakati ya jinsia itakayowezesha upatikanaji wa haki na usawa wa jinsia
  • Uwepo wa mfumo endelevu wa Kutoa rufaa kwa wahanga wa ukatili wa  jinsia

Mikakati

  • Mafunzo endelevu ya uingizwaji wa masuala ya jinsia katika mipango na bajeti kwa ngazi zote
  • Kuwa na mfumo endelevu wa kukusanya na kutumia takwimu za mchanganuo wa kijinsia
  • Kuwa na mfumo wa endelevu wa utoaji elimu ya jinsia
  • Kubuni, kukusanya na kusambaza teknolojia rahisi na sahihi ya kupunguza mzigo wa kazi kwa wanawake na Kutoa fursa ya kushiriki katika shughuli za maendeleo na uongozi.
  • Kupanua fursa ya upatikanaji wa mitaji (Maandiko ya miradi, VICOBA na utoaji wa taarifa za taasisi za kifedha kwa jamii

Mfumo wa rufaa kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia na uvunjifu wa haki za watoto.

8.2 Dawati la Watoto (Children desk)

Dawati hili lilianzishwa ili kutoa uzito kwa masuala ya watoto yanayohusu haki za watoto ambazo ni Haki ya kuishi, kuendelezwa, kulindwa, kuishi na kutobaguliwa.   Lengo kuu la kuanzishwa dawati la watoto  ni kutekeleza  mkataba wa  kimataifa  wa  haki za watoto  uliosainiwa mwaka  1989  na serikali ya Tanzania,  na kutungwa kwa sera ya mendeleo ya mtoto ya mwaka 1996  na kufanyiwa marekebisho 2008.

Malengo ya Dawati

  • Kuhakikisha haki za watoto zinazingatiwa na kutekelezwa na familia na jamii kwa ujumla.
  • Kuhakikisha takwimu za makundi mbali mbali ya watoto walio katika mazingira hatarishi zinakuwepo, zinahuishwa na kusambazwa kwa wadau.
  • Kuwa kiungo kwa wadau wanaoshughulikia masuala ya watoto ikiwa ni sekta za serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Majukumu ya Dawati

  • Kuratibu ukusanyaji , uhuishwaji, uchambuzi na usambazaji wa takwimu zihusuzo watoto
  • Kuratibu na kusimamia masuala yanayohusu haki za watoto
  • ·Kutambua, kuratibu na kusimamia uendeshaji wa vituo vya kulelea watoto mchana na makazi ya watoto yatima.
  • Kuwezesha uanzishwaji na uendelezaji wa mabaraza ya watoto ya kata na wilaya.
  • ·Uanzishwaji na uendelezaji wa kamati za watoto walio katika mazingira hatarishi.

Afua (Interventions)

  • Uanzishwaji na matumizi ya mfumo endelevu wa kukusanya na kuhuisha takwimu za watoto za jumla na za watoto walio katika mazingira hatarishi.
  • Kuendesha mijadala inayohusu haki za watoto (warsha, makongamano, mafunzo na mikutano).
  • Uanzishwaji na uendelezaji wa mabaraza ya watoto yanayofanya kazi.
  • Uanzishwaji na matumizi ya rejesta ya uvunjifu wa haki za watoto inayotumika katika kutoa rufaa (ustawi wa jamii, polisi, hospitali)

Matokeo Muhimu (Key Results)

  • Uwepo wa takwimu za jumla za watoto na za watoto walio katika mazingira hatarishi.
  • Uwepo wa mfumo endelevu wa kiieletronik wa kuchambua, kuandaa na kutunza takwimu za watoto.
  • Uwepo wa mabaraza ya watoto ya kata na wilaya yanayofanya kazi.
  • Uwepo wa mfumo endelevu wa kutoa rufaa kwa watoto waliovunjiwa haki zao ulibuniwa na Idara (Rejesta za Haki za watoto na mimba mashuleni).
  • Uwepo wa vituo vya kulelea watoto mchana vinavyofanya kazi.
  • Uwepo wa mifuko ya kusaidia watoto walio katika mazingira hatarishi ya vijiji inayofanya kazi.

Changamoto

  • Bado kuna idadi kubwa ya watoto walio katika mazingira hatarishi ambao hawajapata usaidizi kulingana na ufinyu wa rasilimali.
  • Mila na desturi bado ni kikwazo katika uvunjifu wa haki za watoto (ukeketaji, unyanyasaji wa watoto)
  • Ugumu katika uendelezaji wa mabaraza ya watoto ngazi ya kata kutokana na ufinyu wa bajeti.

Mikakati

  • Kuanzisha jukwaa la wadau wanaoshughulikia masuala ya watoto ili kuchukua hatua endelevu za kusaidia watoto wenye uhitaji.
  • Kuimarisha mifuko ya kusaidia watoto ya vijiji ili kuwasaidia watoto walio wengi.
  • Kujenga uelewa miongoni mwa wanajamii kuwajibika kuwalea watoto yatima badala ya kuwapeleka kwenye vituo vya watoto yatima.
  • ·Kujenga uelewa miongoni mwa wanajamii kuondokana na mila potofu zinazosababisha uvunjifu wa haki za watoto.
  • Kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa haki za watoto
  •  

8.3 Dawati la Utafiti, Mipango na Takwimu (Research, planning and statisticts)

Idara imeanzisha dawati la Utafiti, Mipango na Takwimu dawati hili lilianzishwa ili kutoa uzito kwa masuala la Upangaji wa mipango, Utafiti na ukusanyaji wa takwimu mbalimbali kwa matumizi ya wadau mbalimbali.

Malengo ya Dawati

  • Kushirikisha jamii kutambua vikwazo na fursa kwa maendeleo ili kupendekeza njia sahihi ya kutatua kwa kufanya utafiti wa kawaida na utafiti shirikishi.
  • Kuhakikisha Idara na Halmashauri kwa ujumla inakuwa na takwimu za uchumi na kijamii na za mchanganuo wa jinsia zitakazotumika wakati wakutoa maamuzi na upangaji mipango na bajeti, ufuatiliaji na tathmini.
  • Kuwezesha jamii kuandaa au kuhuisha mipango shirikishi na bajeti ya mwaka kwa kuzingitia vipaumbele.
  • Kujenga uwezo wa Halmashauri za vijiji katika utawala bora, maandalizi ya mipango shirikishi na bajeti.
  • Kuhakikisha kuwa jamii inaandaliwa ipasavyo kuanzisha, kutekeleza na kusimamia miradi ya jamiii na shughuli za kujitegemea

Majukumu ya Dawati

  • Kuandaa maandiko ya utatifi wa kawaida na utafiti shirikishi  yanayotumika kufanyia utafiti
  • kuratibu ukusanyaji , Uhuishwaji, uchambuzi na kugawa  takwimu za uchumi na kijamii na za mchanganuo wa kijinsia (Gender Disaggregated Data)

Kwa kushirikiana na sekta ya mipango ya Halmashauri dawati linaratibu uibuaji na mapitio ya mipango shirikishi ya fursa na vikwazo vijijini (O&OD)

  • Kwa kushirikiana na sekta ya mipango dawati linaunganisha mipango ya O&OD ya vijiji na kutengeneza mpango wa wilaya.
  • Kuandaa mpango na bajeti ya idara wa kati (MTEF) ili kuunganishwa na mpango wa Halmashauri ya Wilaya.
  • Kuandaa mpango kazi wa  Idara, mpango wa manunuzi na mtiririko wa fedha kwa mujibu wa mpango na bajeti.
  • Kuratibu mafunzo ya halmashuri za vijjji juu ya utawala bora na upangaji mipango shirikishi na bajeti za vijiji.
  • Kuratibu uhamasishaji wa uibuaji , upangaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya jamii na shughuli za  kujitegemea.
  • Kuandaa miongozo ya mipango, bajeti, taarifa, uhamasishaji na utatifi
  • Kuratibu Maandalizi ya  taarifa mbali mbali za idara na kuziwasilisha kwa mkurugennzi, RAS na Wiza

Afua (Interventions)

  • Ukusanyaji , uchambuzi na uhuishwaji wa takwimu za kiuchumi na kijamii na kijinsia
  • Mijadala (warsha, makongamano, mafunzo na mikutano)
  • ·Ushirikishwaji Jamii katika mipango na utekelezaji wa shughuli za kujitegemea
  • Ufuatiliaji na tathmini

Tafiti, na ukusanyaji takwimu

Matokeo Muhimu (Key Results)

  • Uwepo wa Takwimu za Kiuchumi na Jamii na za  mchanganuo wa Jinsia
  • Uwepo Mipango shirikishi na Bajeti  ya vijiji na wilaya
  • Uwepo wa Maandiko ya utafiti na miradi
  • Uwepo wa Miongozo mbali mbali
  • Uwepo wa taarifa inayoonyesha wajumbe waliopewa mafunzo ya Halmashauri za vijiji
  • Uwepo wa taarifa mbali mbali zilizoaandaliwa na kuwasilishwa
  • Uwepo wa taarifa zinazooonyesha hali halisi ya uhamasishaji  na ushiriki wa wananchi wa katika  shughuli za kujitegemea.

Changamoto

  • Migogoro kwenye ngazi ya jamii inayopelekea kuvunjwa uongozi uliopewa mafunzo

Mikakati

  • Kubuni utaratibu wa kutatua migogoro inayojitokeza ili kupunguza matukio ya kuondolewa viongozi.

8.4 Dawati la Ufundi na Ujenzi  (Technical and construction desk )

Idara imeanzisha dawati kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujenga nyumba bora , na kuanzisha vikosi vya ujenzi kati vijiji.

Malengo ya Dawati

  • Kuwezesha Jamii kuwa na vikosi vya ufundi na ujenzi ili kujiajiri katika shughuli za ufundi na ujenzi.
  • Kuwezesha Jamii kujenga nyumba bora zenye gharama nafuu
  • Kutafiti, kukusanya na kusambaza teknolojia rahisi na sahihi zitakazorahisisha utendaji kazi, ujenzi, na ufundi.
  • Kujenga uwezo katika kupanga na kukusanya vifaa vya ujenzi kulingana na makadilrio ya kitaalam

Majukumu ya Dawati

  • Kuratibu uanzishwaji wa vikosi vya ufundi na ujenzi vijijini
  • Kubuni na kutafiti teknolojia rahisi na sahihi na kuzisambaza
  • Kuwezesha ubunifu, utafiti, ukusanyaji, matumizi na Kutoa taarifa juu ya teknolojia mbali mbali rahisi na sahihi kwa jamii na wadau.
  • Kuwezesha uhamasishaji juu ya umuhimu wa ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu vijijini.
  • Kuwezesha wananchi kupanga na kuandaa rasimali na vifaa vinavyohitajika kwa ajiri ya ujenzi wa miradi ya kujitegemea mf madarasa, hosteli,maabara, nyumba za walimu, zahanati na vituo vya afya nk

Kutoa mafunzo kwa vikosi vya ufundi na ujenzi vijijini

  • Kubuni, kuandaa na kusambaza vijijini ramani za nyumba bora za gharama nafuu

Afua (Interventions)

  • Mafunzo kwa vikosi vya ufundi na ujenzi (nadharia na vitendo)
  • Utafiti na ubunifu wa teknolojia rahisi na sahihi
  • Uelimishaji wa jamii juu ya ujenzi wa nyumba bora na uwepo wa teknolojia mbali mbali kwenye jamii.
  • Uwezeshwaji wa mitaji (VICOBA na Mikopo ya  Vijana)
  • Kiviunganisha vikosi na taasisi za kifedha ili kupata mitaji
  • Uenezaji wa teknolojia rahisi na sahihi ili kupunguza mzigo wa kazi (mf. Majiko sanifu,mashine za kukausha mboga, mashine za kupukuchua mahindi, mikokoteni ya wanyamakazi).
  • Kushiriki katika maonyesho ya bidhaa na sughuli  ili kueneza teknolojia zilizopo.

Matokeo Muhimu (Key Results)

  • Uwepo wa vikosi vya ufundi na ujenzi vinavyofanya kazi kwa kujiajiri.
  • Uwepo wa taarifa zinazoonyesha teknolojia rahisi na sahihi zinazofaa kutumika vijijini.
  • Uwepo wa ramani za nyumba zilizochorwa kwa kutumia programmu ya computer (ArchCAD na AutoCAD).
  • Uwepo wa aina mbalimbali za ramani za nyumba bora za gharama nafuu.

Uwepo wa mfumo endelevu wa ukusanyaji, uuishwaji, uchambuzi na usambazaji wa takwimu za vikosi vya ufundi na ujenzi, teknolojia rahisi na sahihi.

  • Uwepo wa program endelevu ya uelimishwaji wa jamii kuona umuhimu wa kuwa na nyumba bora na matumizi ya teknojia rahisi na sahihi
  • Wajumbe wa kamati za maendeleo za kata,kamati za ujenzi za kata waliopewa mafunzo ya maandalizi ya rasilimali na vifaa vinavyohitajika kwa ujenzi.

Changamoto

  • Mitaji midogo na uhaba wa vifaa vya kisasa  kwa vikosi vya ufundi na ujenzi.

Mikakati

  • Kupanua fursa ya upatikanaji wa mitaji (Maandiko ya miradi, uanzishwaji wa VICOBA na kuviunganisha vikundi na taasisis za kifedha.
  • Kubuni mkakati wa Kutoa motisha za kufanya wataalam wa ufundi na ujenzi kubaki idarani.

9.0 MTAALAM WA MAENDELEO YA JAMII NGAZI YA KATA NA MAJUKUMU YAKE 

Watalaam wa maendeleo ya jamii wanalenga kuleta ustawi wa jamii, mabadiliko ya jamii na haki katika jamii. Kimsingi wanajenga uwezo wa makundi ya watu maskini, makundi yaliyosahaulika na jamii kwa ujumla kutambua matatizo yao, kuchambua na kupendekeza njia za kutatua kwa kuanzisha miradi au program za kutatua masuala ya kijamii, kiuchumi, kimazingira na kisiasa.

Wajibu wa Mtaalam wa Maendeleo ya Jamii (roles)

  • Wakala wa Mabadiliko (Agent of change )– Jamii inahitaji mabadiliko, wapo tayari kubadilika, ni wajibu wa Mtalaam wa maendeleo ya jamii kuwawezesha wakubali mabadiliko ya kimfumo na wao wenyewe.
  • Chachu ya Mbadiliko– Mtalaam wa maendeleo ya jamii ni chachu ya mabadiliko anawafanya watu watamani mabadiliko ya maisha yao.
  • Anajenga Uwezo (Build capacity to community) – kwa kuifanya jamii itambue mahitaji yake, watamani kujifunza , kujenga uwezo wa kiuchumi na kuchukua hatua kutatua matatizo yao.
  • Ni Mtafiti– (Researcher) ana uwezo wa kutambua sababu na madhara ya matatizo yaliyopo katika jamii, ana uwezo wa kuchambua takwimu na kuwezesha jamii kupendekeza ufumbuzi wa matatizo yao.
  • Ni Mwezeshaji– (Facilitator) inawawezesha jamii kufanya maamuzi sahihi na kushiriki katika masuala yanayohusu maendeleo yao.
  • Ni Kiongozi– anaelekeza jamii kufikia malengo yao waliojipangia.
  • Ni Mshauri– anatoa ushauri kwa jamii juu ya masuala ya sekta mbali mbali zinazoweza kuwasaidia wananchi na anatoa habari muhimu zinazosaidia jamii kutatua changamoto zao.
  • Ni Mtaalam wa Mipango (Planning expert) – anawezesha jamii kutambua matatizo, kupendekeza njia za kutatua.
  • Ni Mratibu– anaratibu mchango wa sekta mbali mbali katika kutatua changamoto zinazokabili jamii.

Majukumu ya Afisa Maendeleo ya Jamii ya Kata 

Kufanya mikutano ya uhamasishaji ya ushiriki wa jamii kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini miradi ya maendeleo na shughuli za kujitegemea vijijini.

  • Kutoa mafunzo kwa wajumbe wa kamati za ujenzi za kata na halmashauri za vijiji juu ya upangaji na upatikanaji na rasimali na vifaa vya ujenzi wa miradi  ya miundo mbinu
  • Kushiriki katika tafiti shirikishi zinazofanyika katika maeneo ya kata zao.
  • Kukusanya takwimu mbali mbali za kijamii na kiuchumi na za mchanganuo wa jinsia katika vijiji na kata.
  • Kuwezesha jamii kutumia takwimu katika upangaji mipango shirikishi na bajeti za vijiji na kata.
  • Kuwezesha uibuaji au mapitio  ya mipango shirikishi ya fursa na vikwazo kwa maendeleo ya vijiji na kata.
  • Kukusanya na kutoa taarifa juu ya vikwazo vya maendeleo kwenye ngazi ya jamii
  • Kufuatilia utekelezaji wa mipango ya fursa na vikwazo kwa maendeleo ya vijiji.
  • Kuwezesha vijiji kufanya tathmini ya utekelezaji wa mipango ya fursa na vikwazo kwa maendeleo.
  • Kuwezesha uanzishwaji na uendelezaji wa mabaraza ya watoto ya kata.
  • Kuwezesha uanzishwaji na ufuatiliaji wa vituo vya kulelea watoto mchana vilivyopo kwenye vijiji vya kata husika.
  • Kutoa mafunzo ya walezi wa vituo vya kulelea watoto mchana wa vijiji

Kutambua na kuisha takwimu za watoto kwa ujumla na zile za watoto walio katika mazingira hatarishi za vijiji.

  • Kuwezesha na uendelezaji wa mifuko ya kusaidia watoto walio katika mazingira hatarishi ya vijiji.
  • Kuwezesha utatuzi wa migogoro
  • Kukusanya na kuwasilisha takwimu za mafundi, majiko sanifu na nyumba bora.
  • Kukusanya taarifa juu ya teknolojia za kurahisiha kazi zilizopo vijijini.
  • Kuhamasisha ujenzi wa nyumba bora, majiko sanifu na vyoo bora vijijini.
  • Kuhakikisha ramani za nyumba zenye gharama nafuu zinapatikana kwenye kata yake kwa ajili ya kuwapatia wananchi wenye uhitaji.
  • Kuhamasisha uanzishwaji na kutoa mafunzo kwa vikundi vya ujasiriamali vya mchanganyiko, wanawake, vijana na Benki za kijamii vijijini (VICOBA)..
  • Kutambua na kuwezesha maandalizi ya mchanganuo wa miradi kwa vikundi vinavyoomba mikopo kwa wanawake na vijana

Vitendea Kazi na Miongozo

Mtaalam wa Maendeleo ya Jamii ngazi ya kata katika kutekeleza kazi zake anahitajika kuwa miongozo na vitendea kazi vifuatavyo:

  • Sera ya Maendeleo ya Jamii ya Mwaka 1996, Sera ya Jinsia na Wanawake ya Mwaka 2003, Sera ya Mtoto ya mwaka 2000,
  • Dira ya Halmashauri ya wilaya, Dhima ya Halmashauri, Malengo ya Halmashauri na malengo madogo ya Sekta ya Maendeleo ya Jamii.
  • Miongozo ya mwezeshaji na mshiriki wa mbinu shirikishi PRA, O&OD.

Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Malengo ya Millenia na MKUKUTA

  • Miongozo wa kuandaa mpango na taarifa  ya mtumishi wa idara.
  • Mwongozo wa kuanzisha Benki za Kijamii Vijijini.
  • Mwongozo wa uundaji wa mabaraza ya watoto wa kata
  • Mwongozo wa kukusanyia takwimu za kiuchumi na kijamii, takwimu za jinsia na watoto.
  • Rejesta za unyanyasaji wa kijinsia, mimba mashuleni na ukiukwaji wa haki za watoto.
  • Mwongozo wa kuanzisha na kuendesha vituo vya kulelea watoto mchana.
  • Mwongozo wa kufundishia walezi wa vituo vya watoto wadogo.
  • Mwongozo wa mafunzo ya utawala bora, upangaji mipango shirikishi na bajeti kwa Halmashauri za vijiji.
  • Mwongozo uingizwaji wa masuala ya jinsia kwenye bajeti za halmashauri za vijiji

10.0   USTAWI WA JAMII

Ni mchakato wa kuwasaidia watu ambao watu wanuhitaji wa huduma za kijamii,kiuchumi na kisaikolojia.

Kitengo cha Ustawi wa jamii ni Kitengo kilichopo chini ya Idara  ya afya  na kimekuwa kikishirikiana na idara ya maendeleo ya jamii katika kutekeleza shughuli zake . Kitengo hiki kinashughulikia masuala ya wazee, watu wenye ulemavu,familia na watoto (WWKMH,Vituo vya kulelea watoto wadogo mchana na makao ya watoto yatima/wenye shida).

Historia

Kazi za ustawi wa jamii zilianza karne zilizopita katika nchi za Afrika Mashariki ambapo watu walianza kufanya kazi ya kutoa huduma kwenye makao ya watoto yatima,wazee na watu maskini.

Karne ya 19 kilikuwa ni kipindi cha mapinduzi ya viwanda,kipindi kilipelekea kuwepo kwa matatizo ya kijamii (social problems) ukiwemo umaskini,magonjwa,wagonjwa wa akili.

Hivyo serikali na mashirika ya dini yalichukua jukumu la kuanzisha miundo mizuri na sheria zilizoweza kusaidia kutoa huduma ya ustawi wa jamii na kuwasaidia watu wenye uhitaji,hivyo vikundi vingi viliundwa na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii.matatizo yalipoongezeka katika jamii,ndipo umuhimu wa kazi za ustawi ulioonekana,hivyo watumishi walipewa mafunzo zaidi ili kuisaidia jamii kutatua matatizo yao walionayo.

 

Kazi za ustawi wa jamii

  • Kitengo  kinapokea malalamiko ya ndoa zenye mifarakano,na kufanya vikao vya pamoja kwa lengo la kutoa ushauri nasaha   ili kupata suluhu ya matatizo katika familia.
  • Kitengo  kinatoa suluhu juu ya matunzo ya watoto waliozaliwa nje ya ndoa.
  • Kitengo  kinatoa suluhu juu ya matunzo ya watoto walio kwenye ndoa zenye mfarakano.
  • Kitengo  kinasimamia,kufuatilia na kutoa ushauri kwenye makao ya watoto yatima wenye shida.
  • Kitengo kinahamasisha jamii na tasisi mbalimbali juu ya uanzishaji wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana.
  • Kitengo kinafanya utambuzi wa watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi na kutoa misaada,ushauri nasaha na kubuni na kuweka mikakati kushirikiana na jamii husika.
  • Kitengo  kinaelimisha  jamii juu ya  sheria/sera na taratibu za usajili wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana na vituo vya makao - ya watoto yatima/wenye shida.   
  • Kitengo kinafanya utambuzi wa watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi na kutoa misaada,ushauri nasaha na kubuni na kuweka mikakati kushirikiana na jamii husika.
  • Kitengo kinakusanya takwimu za  watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi
  • Kitengo kinasimamia/kufanya uangalizi wa wavunja sheria  wa makosa ya jinai kulingana na muda uliopangwa na hakimu. 
  • Kitengo  kinashauri  na kutoa taratibu na miongozo kwa watu wenye ulemavu na wazee.
  • Kitengo  kinawaunganisha   wahitaji  (clients – disabled,aged people mvc,s) na taasisi husika.

Malengo

  • Kuwezesha Halmashauri kuwa na takwimu za watoto yatima na watoto waishio katika mazingira hatarishi ili wasaidiwe.
  • Kuwezesha jamii kuanzisha vituo vya kulelea watoto wadogo mchana.
  • Kupunguza ndoa zenye mifarakano katika jamii na kuwa na ndoa zinazoishi kwa amani na upendo.
  • Kuwa na takwimu za watoto yatima na watoto waishio katoka mazingira hatarishi.

Matokeo (key results)

  • Ongezeko la vituo vya kulelea watoto wadogo mchana vilivyo sajiliwa.
  • Uwepo wa walimu wenye ujuzi juu ya vituo vya kulelea watoto wadogo mchana.
  • Kuwa na takwimu za watoto yatima na watoto waishio katoka mazingira hatarishi.

Afua (Intervations)

  • Kutoa mafunzo juu ya  sheria/sera na taratibu za usajili wa vituo vya watoto kwa jamii.
  • Ukusanyaji wa takwimu za watoto yatima na watoto waishio Atoka mazingira hatarishi.
  • Kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kusajili vituo vya watoto wadogo mchana.
  • Kushirikiana na wadau wengine kuwapatia walemavu na wazee,mitaji na vifaa vinavyohitajika kulingana na mahitaji yao.

Majukumu ya Maafisa ustawi wa jamii.

  • Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kusajili vituo vya kulelela watoto wadogo mchana
  • Ukusanyaji wa takwimu za WWKMH na watoto Yatima.
  • Ukusanyaji wa takwimu za wazee na watu wenye ulemavu.

 

11.0 KUWEZESHA KUNDI LA VIJANA NA WANAWAKE 

 

11.1 KUNDI LA VIJANA 

Halmashauri  ya Wilaya ya Iringa  kulingana na matokeo ya sensa ya  Idadi ya watu ya mwaka 2012 ina  jumla ya  vijana  58,628 (wanaume 28,217 na wanawake 30,411) wenye umri kati ya 18 hadi 35 .Kati ya Vijana hao  , vijana   1,356 ( ME 825, KE 531)   wamejiunga na vikundi 177 vya vijana vilivyopo katika Halmashauri.   Kati ya vikundi 177 vikundi 122 vimesajiliwa sawa na asilimia 59  . Pia kuna mitanda 5 iliyoungana kwa  lengo la kufanya kazi kwa pamoja. Mitandao hii na jumla ya wanachama. 219, Me 133 Ke 86.

11.2 MFUKO WA VIJANA (YDF)

Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDC) umeanzishwa kwa ajili ya kuwawezesha vijana wenye kipato duni au wasio na kipato ili kupata mtaji wa kuendesha miradi midogo midogo ya kiuchumi na kuwawezesha kuondokana na umasikini uliokithiri. Mfuko huu ulianza kutoa mikopo mwaka 2003/2004 ukiwa na mtaji wa Tshs 3,089,756.00. Mfuko umeendelea kukua na hadi kufikia tarehe 8 Novemba 2016 mfuko una jumla ya fedha kiasi cha Tshs 148,909,462.00 ni fedha zile zilizopo kwenye mzunguko, madeni yaliyopo kwenye vikundi ambapo kati ya hizo kiasi cha, Ili kuweza kufanya usimamizi na ufuatiliaji wa utendaji wa mfuko wa vijana, asilimia 10% hutengwa kutokana na fedha za mfuko kuwezesha wataalamu kuyafikia maeneo yote yenye vikundi na kuvishauri namna bora ya kunufaika na miradi inayoendeshwa

Vikundi  viliundwa kwa mujibu wa maelekezo ya Wizara ya Habari Vijana utamaduni na Michezo, Utaratibu unaoruhusu kuwa na kikundi cha  vijana  chenye  vijana kati ya 5 hadi 10  na kuendelea

Shughuli zinazofanywa  na  vijana shughuli zinazofanywa na vijana katika halmashauri ya wilaya ya iringa ni pamoja na ;-Kilimo,Ufugaji wa mifugo mbalimbali ,Utengenezaji wa vigae vya kuezekea,Migahawa,Biashara,Useremala (utengenezaji wa samani),Ufyatuaji wa Matofali  ya kuuza ,Ufugaji wa samaki ,Kuweka na kukopa (VICOBA),Ufugaji wa nyuki

11.3 Ushiriki wa vijana katika shughuli mbalimbali. (Participation of young people in various activities)

Baadhi Vijana wanaojishughulisha na kilimo wao humiliki maeneo yao katika mabonde ya  Pawaga , na Idodi ambako huzalisha zao la mpunga, eneo la Tarafa za Kiponzelo Mlolo,Kalenga na Ismani  vina hujishughulisha kilimo cha Mahindi, alizeti   na upandaji miti ya mbao, maeneo haya humilikiwa na  baadhi ya vijana wenyewe na wengine hurithi kutoka kwa wazazi wao.

11.4 MAFANIKIO

 

  • Tangu  Mwaka  2004 hadi 2017    Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imeweza kutoa mikopo kwa vikundi vya  vijana  93  vyenye  jumla ya wanachama  442 wakiwemo  wanaume  244 wanawake 198.
  • Vijana wamepata hamasa zaidi ya kuomba mikopo kutoka Halmashauri ya Wilaya na Taasisi za Fedha na Makampuni Mbalimbali
  • Halmashauri   imeendelea  kutenga fedha  kwaajili  ya  kutoa mikopo kwa vijana

11.5 MKAKATI ULIOPO

  • Kuwahamasisha vijana kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali na uzalishaji mali ili kuwawezesha vijana kutambuliwa, kupata elimu ya mbalimbali  na kupata dhamana ya  mikopo.
  • Kuwaunganisha vijana kuunda mitandao inayotokana na shughuli zinazofanana mfano:Mtandao wa wafuga nyuki

Mtandao wa wakulima wanaolima mazao ya kufanana, Mtandao wa wafugaji ,Umoja wa wafyatuaji tofari na  Umoja wa mafundi seremala  ili kurahisisha utafutaji wa masoko kwa bidhaa wanazozizalisha

  • Kuhamasisha vijana kutumia fursa zilizopo za kilimo cha umwagiliaji kwa kuwawezesha mikopo yenye riba nafuu kupitia mfuko wa vijana (YDF).
  • Kuunganisha  mitandao ya    vijana na VICOBA ili  kuanzisha SACCOS ya vijana  kwa ngazi ya Halmshauri  ili kuwawezesha kupata  mikopo kutoka wizara ya vijana, utamaduni na michezo
  • Kuwaunganisha vijana na taasisi za kifedha  zilizopo katika maeneo yao  kama  FINCA, PRIDE, IDYDC, MAMA BAHATI FOUNDATION, NMB, CRDB, BACKLAYS na  MUCOBA ili waweze kupata mikopo ya   kuendesha shughuli za kiuchumi.
  • Kuhamasisha vijana kushiriki katika michezo mbalimbali (Mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa wavu na mpira wa mikono ) ili   kuimarisha afya zao kufahamiana ,kuwajengea umoja  na kupunguza athari za kujihusisha na tabia hatarishi zinazoweza kuwapelekea kupata maambukizi ya VVU/UKIMWI.

Kufanya matamasha na /au mashindano yanayowezesha vijana kuonyesha vipaji, ujuzi na bidhaa wanazozalisha katika wiki ya vijana na kumbukumbu ya baba wa Taifa tarehe 8-13, Oktoba, kila mwaka. Maonesho yatajikita katika mambo yafuatayo:-Bidhaa wanazozalisha, Shughuli wanazofanya, Manufaa ya shughuli wanazofanya na Kuwaunganisha vijana na wanunuzi/watoa huduma mbalimbali.

  • Kuhamasisha vijana kuanzisha  vikundi vya sanaa  kwa lengo la kudumisha mila na desturi nzuri , kuelimisha jamii juu ya masuala mbalimbali ya kijamii na kuvitumia katika maadhimisho mbalimbali ya kitaifa
  • Kuandaa utaratibu wa ziara za ndani na nje ya wilaya   kwa  wanakikundi ili kubadilishana uzoefu katika   uendeshaji wa shughuli za  kilimo bora ,ufugaji wa nyuki,ufugaji samaki na  utunzaji wa mazingira

 

11.2 KUNDI LA WANAWAKE

11.2.1 MFUKO WA WANAWAKE (WDF)

Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) umeanzishwa kwa ajili ya kuwawezesha Wanawake wenye kipato duni au wasio na kipato ili kupata mtaji wa kuendesha miradi midogo midogo ya kiuchumi na kuwawezesha kuondokana na umasikini uliokithiri. Mfuko huu ulianza kutoa mikopo mwaka 1994 ukiwa na mtaji wa Tshs 1,350,000 Mfuko umeendelea kukua na hadi kufikia tarehe 8 Novemba 2016 mfuko una jumla ya fedha kiasi cha Tshs 169,284,526.57 fedha hizi ni zile zilizopo kwenye mzunguko, madeni yaliyopo kwenye vikundi na mchango wa halmashauri ya wilaya

Ili kuweza kufanya usimamizi na ufuatiliaji wa utendaji wa mfuko wa wanawake, asilimia 10% hutengwa kutokana na fedha za mfuko kuwezesha wataalamu kuyafikia maeneo yote yenye vikundi na kuvishauri namna bora ya kunufaika na miradi

Halmashauri  Imefanikiwa   kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa vikundi vya wanawake toka vikundi 9 vya mwaka 1995 hadi vikundi  100 vya mwaka 2016/2017

Shughuli zinazofanywa   na wanawake.

Shughuli zinazofanywa na vijana katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ni pamoja na Kilimo  cha  mpunga, Mahindi, Ufuta , mbogamboga , karanga, Njegere, Nyanya.Ufugaji wa mifugo mbalimbali ,Migahawa, Biashara ya Ufyatuaji wa Matofali, Ufugaji wa samaki, Kuweka na kukopa (VICOBA), Ufugaji wa nyuki.

SHUGHULI WANAZOZIFANYA WANAWAKE 

Wanawake wanaojishughulisha na;-Kilimo,Ufugaji wa mifugo mbalimbali ,Utengenezaji wa vigae vya kuezekea,Migahawa,Biashara,Useremala (utengenezaji wa samani),Ufyatuaji wa Matofali  ya kuuza ,Uuzaji wa samaki  ,Kuweka na kukopa (VICOBA),Ufugaji wa nyuki

MAFANIKIO.

  • Halmashauri  Imefanikiwa  kutekeleza Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa vikundi vya wanawake toka vikundi 9 vya mwaka 1995 hadi vikundi 100 vya mwaka 2016/2017.
  • Wanawake  waliobahatika kupata mkopo wameweza kuendesha miradi yao  katika Nyanja za kilimo, biashara ndogondogo na  ufugaji
  • Katika  baadhi ya maeneo vikundi vidogo vidogo vimeungana na kuanzisha benki za kijamii (VICOBA) ambapo hadi sasa kuna VICOBA
  • Kutokana na shuhuda  za wakopaji wameweza kuongeza kipato na kuweze kumudu mahitaji ya muhimu kama vile kulipa ada za watoto, sare za shule, kujenga nyumba  na mahitaji madogo madogo  ya nyumbani
  • Maombi ya mkopo kwa upande wa wanawake  kwa sasa yanapungua kulingana na mwaka jana na mwaka juzi kutokana na uanzishwaji wa benki za kijamii (VICOBA).

MKAKATI ULIOPO

  • Kuwahamasisha wanawake kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali na uzalishaji mali ili kuwawezesha vijana kutambuliwa, kupata elimu ya mbalimbali  na kupata dhamana ya  mikopo.
  • Kuwaunganisha wanawake kuunda mitandao inayotokana na shughuli zinazofanana mfano:Mtandao wa wafuga nyuki Mtandao wa wakulima wanaolima mazao ya kufanana, Mtandao wa wafugaji ,na Umoja wa wafyatuaji tofari  ili kurahisisha utafutaji wa masoko kwa bidhaa wanazozizalisha.
  • Kuhamasisha wanawake kutumia fursa zilizopo za kilimo cha umwagiliaji kwa kuwawezesha mikopo yenye riba nafuu kupitia mfuko wanawake.
  • Kuunganisha  mitandao ya    wanawake na VICOBA ili  kuanzisha SACCOS  ya wanawake   katika ngazi ya Halmshauri  ili kuwawezesha kupata  mikopo kutoka  Benki ya wanawake .
  • Kuwaunganisha wanawake  na taasisi za kifedha  zilizopo katika maeneo yaokama  FINCA, PRIDE, IDYDC, MAMA BAHATI FOUNDATION, NMB, CRDB, BACKLAYS na  MUCOBA BANK  ili waweze kupata mikopo ya   kuendesha shughuli za kiuchumi.

CHANGAMOTO

 

  • Wanawake wengi kuendesha shughuli za kilimo zaidi kuliko biashara nyingine ndogondogo
  • Woga wa kufanya biashara tofauti na kilimo kwa sababu ya ukosefu wa soko la kutosha la bidhaa tofauti  na kilimo mfano batiki,sabuni, na Dawa za choo.
  • Hali ya hewa (Ukame ) kwa maeneo ya Ismani huathiri uzalishaji na kukwamisha maendeleo ya baadhi ya vikundi vinavyojishughulisha na kilimo cha mahindi na alizeti

MIKAKATI

  • Kuendelea kutoa elimu ya ujasiliamali kwa vitendo  kwa vikundi vya wanawake ili  waweze kubuni biashara mpya na nzuri zaidi.
  • Kuendelea kutoa hamasa kwa wanawake kujiunga katika vikundi iliwaweze kukopesheka   na kukuza  mitaji yao.
  • Kuendelea kuhamasisha na kuwezesha uundwaji wa benki za kijamii (VICOBA) ili  kupunguza Idadi kubwa ya wanawake wanaotegemea mikopo toka mfuko wa maendeleo ya wanawake (WDF)

12.0 URATIBU WA ASASI ZA KIRAIA (CBOS/NGOS/FBOS)

Usajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Tanzania Bara imegawanyika katika ngazi ya Wilaya, Mkoa, Kitaifa na Kimataifa kwa lengo la kuwezesha na kurahisisha zoezi la utoaji wa huduma hii muhimu katika ngazi hizo. Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24/2002 kifungu 22 (1) (2) natoa mamlaka kwa Msajili kuteua Maafisa wa Umma ambao watakuwa na jukumu la kuwezesha usajili wa wa Mashirika haya katika ngazi ya Wilaya na Mkoa.

Mwaka 2005 baada ya Sheria hii kuanza kutumika, serikali iliwateua Makatibu Tawala (W) na Maafisa Mipango (M) kuwezesha usajili katika maeneo yao kwa maana ya Wilaya na Mikoa, kabla ya kuwasilisha rasmi maomb hayo kwa Msajili kwa ajili ya kupatiwa cheti.  Kwa sasa taratibu za usajili wa NGOs zinaelekeza kuwa majukumu ya Maafisa Maendeleo ya Jamii kama Wasajili Wasaidizi ni kuwezesha usajili wa NGOs katika ngazi za Wilaya na Mikoa kulingana na maeneo yao ya kazi.

TARATIBU ZA USAJILI WA NGOs

Msingi wa taratibu za usajili wa NGOs ni:Kanuni za NGOS za mwaka 2004 Taratibu za kisheria

KANUNI ZA NGOs:

Kanuni ya 7 ya Kanuni za NGO inaelezea utaratibu wa usajili chini ya Wasajili Wasaidizi kama ifuatavyo: Wasajili Wasaidizi katika ngazi za Mkoa na Wilaya watapokea na kupitisha/kukubali maombi au kukataa maombi ya usajili.Endapo watapitisha/kukubali maombi wanatakiwa kuandaa na kuwasilisha taarifa/maoni kwa Msajili kuhusu kupitisha maombi hayo. Endapo watakataa kupitisha maombi wanatakiwa kumjulisha muombaji wakitoa sababu za kukataa maombi, pia watoe taarifa ya kukataa maombi hayo na kuwasilisha kwa Msajili.

Kanunuzi ya 8 inatoa ufafanuzi kuwa mwenye mamlaka ya mwisho kuhusu usajili ni Msajili Mkuu kwani ana mamlaka ya kukubali taarifa ya Msajili Msaidizi, kurekebisha au kuomba taarifa zaidi toka kwa muombaji au Msajili Msaidizi.

 

 

Taratibu za Kisheria:

Maombi ya usajili wa NGOs yaambatanishwe:

  • Nakala tatu (3) za Katiba.
  • Muhtasari wa kikao kilichofanyika kabla.
  • Maelezo binafsi ya viongozi (Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina 

            na picha 2 kila    kiongozi

  • Anuani na sehemu yalipo makao makuu ya NGO.
  • Ada ya usajili.
  • Maelezo mengine kama yatakavyohitajika na Msajili.

Maombi ya usajili yatatumwa kutumia Fomu Na. 1na maombi ya cheti cha ukubalifu yatatumwa kutumia Fomu Na. 3.Maombi ya NGOs za Kitaifa na Kimataifa yatawasilishwa moja kwa moja Ofisi ya Msajili Mkuu na maombi ya Wilaya na Mkoa yatapitia kwa Wasajili Wasaidizi watoe maoni yao kabla ya kuwasilisha kwa Msajili Mkuu.

Maombi ya Cheti cha Ukubalifu

(ii) Maombi ya cheti cha Ukubalifu yaambatanishwe na vifuatavyo:-

  • Nakala 3 za Katibu ya NGO zilizojaladiwa.
  • Nakala ya Cheti cha Usajili wa awali.
  • Taarifa ya kikao kilichopitisha Katiba.
  • Maelezo binafsi ya viongozi (Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina na picha 2 kila kiongozi).
  • Anuani na sehemu yalipo makao makuu ya NGO.
  • Maelezo mengine kama yatakavyohitajika na Msajili.

ADA ZA USAJILI

Ngazi za Wilaya:

  • Ada ya usajili ngazi ya wilaya ni Shs. 41,500

 Mchanganuo 

  • Ada ya usajili                        Shs. 40,000
  • Stempu                                 Shs. 1,500

            (Stempu iambatishwe kwenye fomu ya maombi Na. 1)

Ngazi ya Taifa

Ada ya usajili ngazi ya Taifa ni Shs. 66,500/=

Mchanganuo 

  • Ada ya usajili                     -   Shs. 65,000
  • Stempu                              - Shs.   1,500

(Stempu iambatishwe kwenye fomu ya maombi).

Ngazi ya Kimataifa:

Ada ya usajili ngazi ya Kimataifa ni dola 267.

  • Ada ya usajili                 -        USD  267
  • Stempu                           -        USD  2

(Stempu iambatishwe kwenye fomu ya maombi)

 

 

MALIPO YA ADA YA MWAKA      

  • Kila NGO iliyosajiliwa inatakiwa kulipa ada ya mwaka ya Shs. 50,000/= au dola za Marekani 60 kwa NGOs za Kimataifa.
  • ·NGOs zote zinazopatiwa Cheti cha Ukubalifu zinatakiwa pia kulipa ada ya mwaka kila baada ya mwaka mmoja ya kiasi hicho hicho cha fedha.

TARATIBU ZA KULIPA ADA

  • Malipo yote ya ada za usajili na ada za mwaka yatalipwa kama ifuatavyo:
  • NGOs zitafanya malipo husika moja kwa moja kwenye idara ya uhasibu.  Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.  Stakabadhi halali kwa malipo hayo itatolewa
  • Hakutakuwa na ada ya usajili kwa Mashirika yanayoomba Cheti cha Uiubalifu.

 TAARIFA YA KAZI

  • Kila NGO iliyosajiliwa inatakiwa kuwasilisha kwa Msajili taarifa ya kazi ya mwaka na mahesabu iliyohakikiwa na Wakaguzi wa hesabu waliosajiliwa.
  • Taarifa hizi zipatiekwa Wasajili Wasaidizi (W) na (M) kabla ya kuwasilishwa kwa Msajili Mkuu kufanyiwa uchambuzi na kuhifadhiwa kwenye Benki ya taarifa.
  • Taarifa hizi zitakuwa kwenye Fomu Na. 10.
  • Kwa ujumla taratibu za usajili wa NGOs zinaelekeza kuwa majukumu ya Maafisa Maendeleo ya Jamii kama Wasajili Wasaidizi ni kuwezesha usajili wa NGOs katika ngazi za Wilaya na Mikoa kulingana na maeneo yao ya kazi.
  • Wasajili Wasaidizi watahakiki Katiba za NGOs na kuzitolea maoni.
  • Watahakiki uwepo wa Ofisi kwa kila NGO inayoomba usajili.
  • Watahakiki Fomu mbalimbali na kutoa ushauri wa kisekta kusajili chini ya Sheria ya NGOs Na. 24/2002 na kuhakiki NGOs zinalipa ada za mwaka kwa wakati.
  • Endapo Msajili Msaidizi atapokea maombi ya NGO inayojihusisha na Vituo vya Malezi ya Watoto walio katika Mazingira Magumu ni muhimu kuwaelekeza wahusika kuambatisha maoni kutoka idara ya Ustawi wa Jamii na ndipo Msajili atatoa maoni yake na kupitisha maombi kwa Msajili Mkuu.
  • Kutuma makabrasha kwa Msajili kwa ajili ya kutengenezewa Vyeti na kuhakikisha yanatumwa kwa wakati.
  • Kutoa maelekezo ya jinsi ya kufanya malipo ya usajili sambamba na kutoa weledi kuhusu taratibu za usajili kuzingatia sheria ya NGOs 24/2002.
  • Kutoa taarifa kuhusu asasi zilizosajiliwa katika ngazi zao.

 

T ARATIBU ZA USAJILI WA VIKUNDI VYA KIUCHUMI 

 

  • Kuongeza mtaji katika mfuko wamaendeleo ya wanawake na vijana (itatunisha mfuko wa wanawake na vijana) hivyo kutoa fursa kwa vikundi vingi zaidi kukopa.
  • Ni utaratibu ambao Halmashauri zote Tanzania   wanafanya ili kuweza  kumudu gharama za kutoa vyeti kwa kuwa  sasa kinachotolewa ni cheti na siyo barua kama ilivyokuwa zamani:
  • Kujenga  tabia ya  kutunza na kuthamini vyeti vya usajili wanavyopewa,kwa kuwa inaonekana wanapotambuliwa hawatunzi wanapoteza na kurudi mara kwa mara pale wanapohitajika kutumia cheti cha utambulisho:

Maombi ya usajili wa yaambatanishwe

  • Nakala tatu (3) za Katiba.
  • Muhtasari wa kikao kilichofanyika kabla.
  • Maelezo binafsi ya viongozi (Mwenyekiti, Katibu na Mweka
  • Hazina na picha 2 kila    kiongozi.
  • Anuani na sehemu yalipo makao makuu ya  kikundi/CBO
  • Ada ya usajili.
  • Maelezo mengine kama yatakavyohitajika na Msajili.

Taratibu za kulipa gharama za usajiri na ada ya mwaka.

Aina ya vikundi na ada ya usajili 

  • Vikundi vya wanawake (Women Economic Group (WEG) ( ada ya Usajili ni 3000)
  •  Benk za kijamii - Village Community Bank (VICOBA)  5000
  • Vikundi vya vijana (Youth Economic Group (YEG)  (Ada ya usajili  3000)
  • Vikundi vya mchanganiko(Income Generating Activities (IGA)  (ada ya usajili 5000)
  • Taasisi za kijamii (Community Based Organizatio ) (ada ya usajili 15,000)
  • Faith Based Organization (FBO)
  • Vikundi vya ufundi na ujenzi (Technical and Construction Group )  (Ada  ya usajili 5000)
  • Mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali (Non government organizations )

Vikundi ambavyo  vipo chini ya Ushirika 

  • Vyama vya kuweka na kukopa (Saving and credit cooperative society) usajili ni ushirika ( SACCOS)
  • Vikundi vya kuweka na kukopa (Saving and credit cooperative Group (usajili ni ushirika ) (SACCOS)

 

    Mfumo wa uanzishaji wa vikundi 

                          

 MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII   (TASAF)

Kulingana na sensa ya mwaka 2002 Halmashauri ina jumla ya watu 254,032 wanaume 123,243 na wanawake 130,789 na kaya 60,160.TASAF awamu ya Tatu hapa wilayani Iringa ilianza Januari 2015. Katika awamu hii TASAF imeweza kufikia jumla ya vijiji 82 kati ya133 sawa na asilimia 66. Lengo ilikuwa ni kutambua Kaya 7,540 zilizotambuliwa 8,554.

Mfuko wa  Maendeleo ya jamii (TASAF katika   Halmashauri ya wilaya ya Iringa  Unatekeleza Mpango  wa kunusuru  Kaya  Maskini  unawezesha  kaya  maskini  kupata mahitaji ya msingi, kulinda rasilimali   zao na kuweka  akiba  kwa ajili  ya kujiletea  maendeleo  na hatimaye kujitoa kwenye  umaskini.

 

 MADHUMUNI YA MPANGO

Madhumuni ya TASAF awamu ya Tatu - Mpango  wa Kunusuru Kaya Maskini  ni  kuziwezesha  kaya maskini  kupata mahitaji ya msingi  na fursa  za kujiongezea  kipato.

 

WALENGWA WA MPANGO

Walengwa wa mpango ni kaya maskini katika jamii katika maeneo   yaliyoainishwa.

WALENGWA WAMPANGO WALIVYOPATIKANA.

Walengwa wa Mpango huu wanapatikana  kupitia utaratibu ufuatao:-Maeneo ya utekelezaji  yalichaguliwa  kutokana na takwimu  za viwango  vya umaskini   katika maeneo   yote  nchini  na kupewa fedha za utekelezaji.Jamii katika  maeneo husika zilichagua  kaya maskini sana ambazo  zinakidhi  vigezo vya kusaidiwa, Njia  mfumo wa kompyuta ilitumika  kupitia   na kuchuja majina ya walengwa walioorodheshwa ili kubaki  na wale tu  wenye sifa kuwa kwenye Mpango.Majina  ya walengwa   yaliyopatikana   kupitia mfumo wa kompyuta  yalitafanyiwa  uhakiki  wa mwisho  na jamii husika  ili kupata  walengwa  wanaostahili  kuwepo  kwenye  mpango  chini ya usimamizi  wa Halmashauri  za vijiji.

 

4.0 MAENEO YANAYOTILIWA MKAZO.

TASAF awamu ya Tatu   - Mpango   wa kunusuru  Kaya  Maskini zilizo

katika Mazingira   Hatarishi  unatilia  mkazo  maeneo   makuu  yafuatayo:-

Kunusuru  kaya  maskini  kwa kuzipatia  fedha  ambazo  zitasaidia  kwenye  uzalishaji mali  ili wapate  manufaa  ya muda mrefu.

Kutoa ajira   ya muda mfupi kwa walengwa wenye   uwezo wa kufanya kazi kutoka kwenye  kaya maskini  na kuzipatia stadi  mbalimbali.

Kutoa  ajira  ya muda mfupi  kwa walengwa  wenye  uwezo wa kufanya kazi  kutoka  kwenye kaya maskini  na kuzipatia stadi  mbalimbali.

Kukuza na kuchochea  utamaduni  wa kaya maskini  kujiwekea  akiba na kuzipa  elimu  ya masuala ya  fedha na uendeshaji  wa biashara ndogo ndogo.

Kuziwezesha  jamii maskini  kujenga / kuboresha  miundombinu  ya maji, elimu na  afya  katika maeneo ambayo  hayana  huduma hizi  ili walengwa  wapate kutumia  huduma hizi  ikiwa kigezo  cha kutimiza  masharti  ya Mpango.

Mpango  utasisitiza  ushiriki wa Walengwa  ili watoke  kwenye Mpango  wakiwa na  uwezo  wa kujikimu, kupata  chakula na kujikita  katika shughuli  za uzalishaji  na kuwekeza.

5.0 SEHEMU ZA MPANGO

 

TASAF awamu ya Tatu – Mpango  wa Kunusuru  Kaya  Maskini  zilizo katika Mazingira hatarishi  una  sehemu  kuu nne.  Sehemu hizo ni:-

Kunusuru kaya Maskini na zilizo katika mazingira hatarishi.

Walengwa kutoka kwenye kaya  maskini  watapatiwa  ruzuku  ili kuziwezesha  kupata  huduma  za elimu  na afya.  Aidha, sehemu   hii itakuwa  inatoa ajira  kwa kaya  maskini  zenye watu wenye  uwezo  wa kufanya  kazi  wakati  wa majanga mbalimbali  kwa mfano ukame na mafuriko.

Kuinua  hali  ya maisha  na kuongeza kipato

Watu wenye  kuonyesha jitihada  katika kuboresha kipato  na kuinua  hali za maisha kwa kuweka  akiba na kuwekeza, watapatiwa mafunzo ya utunzaji wa fedha  na kuendesha  biashara  ili makundi  haya yaweze kujiimarisha  kiuchumi.

Ujenzi  wa miundombinu katika  maeneo  maalumu

Vijiji  ambavyo  havina miundombinu  au huduma  hizo  ziko mbali vitawezeshwa kujenga  miundombinu ambayo  itasaidia  walengwa  kutimiza  masharti  ya mpango.  Miundombinu itakayojengwa ni  sekta ya afya, maji na elimu.

Kujenga uwezo

Wadau katika ngazi  zote za Taifa, Mkoa na Wilaya, Kata, Vijiji na  Shehia watapewa  mafunzo  yatatolewa  ili  utekelezaji  wa Mpango  ufanyike kwa mujibu  wa taratibu  na hivyo kufanikisha  malengo yaliyowekwa.



Utoaji wa  misaada kwa vituo vya kulelea watoto yatima


Baadhi ya watumishi wanawake wakitoa zawadi kwenye kituo chakulelea wototo yatima Nyumba Yetu Ismani wakati wa maadhimisho ya siku ya mwanamke 

 



Ni mabinti wa jamii ya wafugaji kutoka kijiji cha Malinzanga  wakitumbuiza wakati wa madhiimisho ya sikun ya wanawake

 



 

 



Mratibu wa dawati la jinsia la  halmashauri  ya wilaya akiwa  ofisini akitekeleza moja ya majukumu yake



Wataalamu wakijadiliana na wananchi  juu ya upangaji wa mipango





Wataalamu wakiwezesha wananchi upangaji wa mipango ngazi ya kijiji





Wataalamu wakijadiliana na wananchi 




ramani za nyumba bora zenye gharama nafuu ambazo hutolewa na mtaalam wa kitengo cha ufundi na ujenzi






Mfano wa nyumba bora iliyokamilika ya gharama nafuu






Watumishi wa idara ya maendeleo ya jamii wakishiriki kuhamasisha shughuli za kujitegemea katika kijiji cha Ikengeza


Maonyesho ya idara ya maendeleo ya jamii ngazi ya kata



 





 




Utengenezaji wa majiko banifu na sanifu katika maonesho ya nane nane mbeya

 

 

 

 


Mmoja wa watumishi akikabidhi msaada kwa Mzee katika kijiji cha Mangalali .

 

 

 

 

 

 

Wototo wanaoishi katika mazingira magumu  kijiji cha Mlanda

Watoto hawa wamenunuliwa sare za shule na wazazi wao wanaopata ruzuku ya fedha za Mpango wa kunusuru kaya maskini.  Picha wakati

 

IDARA YA MAENDELEO YA JAMII

AINA YA TEKNOLOJIA ZINAZO WEZA KUTUMIWA KATIKA MAENEO MBALIMBALI VIJIJINI

     Na.

Aina ya Teknolojia

Picha ya Teknolojia husika

Asili ya Teknolojia

Maelezo ya Teknolojia Husika


Jiko sanifu(Rocket Stove)


Chuo kikuu cha Dar es salaam(Pro BEC)

  • Hupika vyakula vya aina mbalimbali haraka zaidi
  • Linatumia kuni na mkaa kidogo sana
  • Huhifadhi mazingira
  • Gharama za ujenzi ni nafuu

Jiko sanifu(Ndani hujengwa kwa chungu)


Njombe

  • Hupika vyakula vya aina mbalimbali
  • Linatumia kuni na mkaa kidogo
  • Lina hamishika
  • Hujengwa kwa simenti na wavu

Jikosanifu(Hutengenezwa kwa bati na chuma cha cast iron)


VETA-Mbeya

  • Hupika vyakula vya aina mbalimbali
  • Huoka mikate
  • Kuchemsha maji
  • Halitoi moshi
  • Linahamishika

Kaushio la mbogamboga na matunda


Japan-JAICA

  • Kukausha matunda na mbogamboga
  • Hutengenezwa kwa mbao,bati na wavu
  • Gharama za ujenzi hutegemea mahitaji

Jiko la Maranda


Sumbawanga
  • Hupika vyakula vya aina mbalimbali
  • Hutumia maranda na ukuni mmoja
  • Hutengezwa kwa bati na nondol(6mm)
  • Linafaa kwa mapishi ya biashara

Jiko la kuchemsha maji kwa kutumia mkaa kidogo


Sumbawanga

  • Kuchemsha maji
  • Hutumia mkaa kidogo sana
  • Hutengenezwa kwa bati gumu
  • Hufaa kwa matumizi ya nyumbani na biashara

Jiko la maranda(Hupika na kuchemsha maji)


Sumbawanga

  • Hupika vyakula vya aina mbalimbali na kuchemsha maji kwa wakati mmoja
  • Hutumia maranda ya mbao

Jiko la mionzi ya Jua


Pawaga Iringa

  • Kuchemsha maji
  • Kuyeyusha nta
  • Kupikia vyakula
  • Hali hitaji kuni na mkaa
  • Hutunza mazingira

Mtambo wa kufua umeme kwa upepo


Makambako-Njombe

  • Huzalisha umeme wa nyumbani na kwa matumizi ya viwanda vidogo
  • Hutunza mazigira
  • Hakuna malipo ya kila mwezi

Jiko la Bio gas


Songea

  • Hupika vyakula vya aina zote
  • Halitoi moshi kabisa
  • Hutengenezwa kwa vyuma
  • Hutegemea kinyesi cha ng’ombe kuzalisha gesi

Jokofu la Asili(Pozeo Mkaa)


Songea

  • Hutumika kuhifadhi mbogamboga, matunda na vyakula.
  • Hujengwa kwa udongo/sementi, mkaa, majivu, fito/mbao na nyasi
  • Huhitaji maji ili kufanya kazi.

Kifaa cha kukuzia vifaranga vya kuku


Iringa

  • Hutumika kukuzia vifaranga baada ya kuvitenga na kuku wakubwa
  • Hujengwa kwa mbao na siling bodi au maboksi
  • Hutegemea taa ya chemli

Jiko sanifu(lenye bomba la kutolea moshi)


Mpanda

  • Lina faa kwa matumizi ya Taasisi kama shule n.k
  • Hujengwa kwa matofali, simenti, vyuma na bomba la moshi
  • Hupika haraka

Mashine ya kuchanganya mbegu na Dawa


Iringa

  • Huchanganya mbegu na Dawa kwa urahisi
  • Imetengenezwa kitaalam kwa kutumia vyuma
  • Haitumii umeme

Matangazo

  • Heri ya sikukuu ya Pasaka April 19, 2025
  • Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura May 01, 2025
  • Kila la Heri Kidato cha Sita 2025 May 05, 2025
  • KUITWA KWENYE USAHILI WA UBORESHAJI WA DAFTARI JIMBO LA KALENGA NA ISMANI December 06, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • "KILA KATA WEKENI MIKAKATI MAALUMU YA KUPUNGUZA HALI DUNI YA LISHE" - MHE. KHERI JAMES

    May 09, 2025
  • KAMPENI YA CHANJO YA POLIO AWAMU YA PILI YATOLEWA MEI 01, 2025

    May 08, 2025
  • MBOMIPA Wakabidhi Gari kwa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori

    May 08, 2025
  • IRINGA DC YAKABIDHI MWENGE WA UHURU KILOLO DC

    April 29, 2025
  • Tazama zote

Video

Makala kuhusu miundombinu ya elimu
video

Viungo vya haraka

  • FOMU YA USAJILI WA VIKUNDI
  • INGIA KWENYE MFUMO WA VIKUNDI VYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA
  • Salary slip

Viungo vinavyohusiana

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Rais-Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais -Utumishi na Utawala Bora
  • Sekretariati ya ajira
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti kuu ya takwimu huria
  • Tovuti Rasmi ya Rais

Idadi ya watembeleaji duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

https://bachelorthesiswritingservice.com

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Kijiji cha Ihemi

    Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa

    Simu ya mezani: 026-2702828/2702585

    Simu ya mkononi: 0757 364 994

    Barua pepe: ded@iringadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa