IDARA YA ELIMU YA MSINGI
0 UTANGULIZI:
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa inasimamia utoaji wa elimu katika ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi na Elimu ya Watu Wazima na Idara ina vitengo vinne. Aidha yapo madarasa ya awali 113 na shule za msingi 149, madarasa ya Elimu ya Watu Wazima….na vituo vya Ufundi Stadi 2
Katika usimamizi na utekelezaji wa Elimu ya Msingi yapo baadhi ya mafanikio, changamoto na athali za changamoto hizo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kama ifuatavyo:-
MAJUKUMU YA IDARA:
Kusimamia uandikishaji katika
Kusimamia utoaji wa Elimu bora.
Kujenga uwezo wa utawala bora, usimamizi na ufuatiliaji katika Elimu.
Kusimamia na kuratibu masuala mtambuka.
Kufafanua na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo, Sheria na
Elimu ya awali.
Elimu ya Msingi.
Elimu Maalumu.
Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya mfumo Rasmi.
Ukimwi na VVU.
Elimu ya mazingira.
Usawa wa Kijinsia katika Elimu.
kanuni zinazoongoza utoaji wa Elimu na mafunzo ya Ufundi.
Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Elimu.
Kuhimiza udhibiti wa nidhamu ya walimu na wanafunzi.
Kusimamia maendeleo ya taaluma na michezo.
Kukusanya, kuratibu na kuchambua takwimu za Elimu kwa ajili ya Mipango ya Maendeleo katika ngazi ya shule, Halmashauri, Mkoa na Taifa.
Kusimamia wajibu na haki za walimu.
MAFANIKIO YA ELIMU YA MSINGI
1.Elimu ya Msingi
Idadi ya Shule za Msingi imeongezeka kutoka shule 118 mwaka 2006 kufikia shule za msingi 146 mwaka 2014.
2 Ikama ya walimu na idadi ya wanafunzi
Idadi ya walimu imeongezeka kutoka walimu 1226 mwaka 2006 kufikia walimu 1358 mwaka 2014 sawa na ongezeko la uwiano wa 1:45. Mchanganuo wa idadi ya wanafunzi pamoja na mahitaji, waliopo na upungufu wa walimu ni kama ilivyooneshwa hapo chini.
Ikama ya walimu na idadi ya wanafunzi
IDADI YA WANAFUNZI
|
IKAMA YA WALIMU
|
||||||
|
WAV
|
WAS
|
JUMLA
|
MAHITAJI
|
WALIOPO
|
UPUNGUFU
|
UWIANO
|
AWALI
|
4050
|
4040
|
8090
|
404
|
127
|
277
|
1:64
|
MSINGI
|
29370
|
29544
|
58914
|
1473
|
1358
|
115
|
1:43
|
NB: Uwiano unaohitajika ni 1:40 (yaani mwalimu 1 kwa wanafunzi 40 kwa elimu ya msingi na 1:20 kwa elimu ya awali.)
3 Uandikishaji wa wanafunzi
Uandikishaji wa wanafunzi wenye umri wa kuanza darasa la kwanza umeongezeka kutoka 52.9% mwaka 2005/2006 hadi 99.1% mwaka 2013/2014 kama inavyooneshwa kwenye jedwali lifuatalo:
HALI HALISI YA UANDIKISHAJI KWA MUDA MIAKA 10 MFULULIZO
MWAKA
|
WALIOTEGEMEWA
KUANDIKISHWA |
WALIOANDIKISHWA
|
ASILIMIA (%) YA UANDIKISHAJI
|
||||||
WAV
|
WAS
|
JUMLA
|
WAV
|
WAS
|
JUMLA
|
WAV
|
WAS
|
JML
|
|
2005
|
10,000
|
11,000
|
21000
|
5641
|
5469
|
11110
|
56,41
|
49.7
|
52.9
|
2006
|
4500
|
4886
|
9386
|
4419
|
4385
|
8804
|
98.2
|
89.7
|
93.7
|
2007
|
4500
|
4884
|
9364
|
4695
|
4699
|
9394
|
104.3
|
96.2
|
100.3
|
2008
|
5000
|
3692
|
8692
|
4195
|
4133
|
8328
|
82.6
|
103.5
|
95.8
|
2009
|
4500
|
4500
|
9000
|
4450
|
3990
|
8440
|
98.8
|
88.6
|
93.7
|
2010
|
4700
|
4750
|
9450
|
4818
|
4518
|
9336
|
102.5
|
94.94
|
96.7
|
2011
|
4956
|
4522
|
9478
|
4645
|
4695
|
9340
|
93.7
|
103.8
|
98.75
|
2012
|
4789
|
4661
|
9450
|
4748
|
4668
|
9416
|
99.1
|
100
|
99,5
|
2013
|
4022
|
4192
|
8214
|
3971
|
4172
|
8143
|
98.7
|
99.5
|
99.1
|
2014
|
4689
|
4881
|
9570
|
4856
|
4618
|
9474
|
99.2
|
99.5
|
99.8
|
NB: Tofauti katika idadi ya wanafunzi waliotegemewa kuandikishwa na walioandikishwa inatokana na sababu ya kuhama na kuhamia kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
4 Elimu Maalum
Wilaya ya Iringa ni kati ya Wilaya chache zenye shule maalum. Shule ya Msingi Kipera iliyopo kata ya Nzihi ilianzishwa mwaka 1976 kama shule ya kawaida. Mwaka 2013/2014 shule hii ilianzisha kitengo cha Elimu maalum ikiwa na wanafunzi wenye ulemavu wa aina mbili uziwi na wasioona ambapo hadi sasa idara imepokea wanafunzi 10 wasiosikia na 12 wasioona.
Miundombinu ya shule ya watoto wenye ulemavu (Kipera) imeboreshwa kwa kiasi kikubwa hadi kufikia 80% mwaka 2013/2014)
5 Miundombinu ya shule
Idadi ya vyumba vya madarasa imeongezeka kutoka vyumba 986 mwaka 2005/2006 kufikia vyumba 1238 mwaka 2013/2014 ongezeko hili ni sawa na asilimia 20.
Matundu ya vyoo yameongezeka kutoka matundu 1326 mwaka 2005/2006 hadi 1824 mwaka 2013/20014 ongozeko hili ni sawa na asilimia 28. Nyumba za walimu zimeongezeka kutoka nyumba 398 mwaka 2005/2006 kufikia nyumba 611 mwaka 2013/2014 na madawati kwa mwaka 2013/2014 ni 18490 upungufu 10967
0 MATOKEO YA MITIHANI YA TAIFA YA DARASA LA
IV NA VII
1 Matokeo ya Mtihani wa darasa la iv (2011-2013)
Tathmini ya mtihani wa Taifa wa darasa la IV kwa miaka 3 mfululizo kuanzia mwaka 2011` hadi 2013.
MWAKA
|
WALIOFANYA |
KIWANGO CHA UFAULU
|
% |
|||||||||||||
IDADI YA WANAFUNZI WALIOFAULU
|
||||||||||||||||
DARAJA ‘A’
|
DARAJA ‘B’
|
DARAJA ‘C’
|
JUMLA (A+B+C)
|
|||||||||||||
WV
|
WS
|
JML
|
WV
|
WS
|
JML
|
WV
|
WS
|
JML
|
WV
|
WS
|
JML
|
WV
|
WS
|
JML
|
||
2011
|
3769
|
3908
|
7697
|
03
|
01
|
04
|
189
|
212
|
401
|
1154
|
1346
|
2500
|
1346
|
1559
|
2905
|
37.7
|
2012
|
3488
|
3769
|
7257
|
0
|
0
|
0
|
54
|
56
|
110
|
633
|
636
|
1269
|
691
|
688
|
1379
|
19
|
2013
|
3339
|
3833
|
7172
|
06
|
09
|
15
|
93
|
113
|
206
|
591
|
688
|
1279
|
690
|
810
|
1500
|
20.9
|
2 MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA VII (2004 2013)
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ilikuwa na jumla ya wanafunzi 6,403 waliofanya mtihani wa Taifa mwaka 2013. Wanafunzi waliochaguliwa kuendelea na Kidato cha kwanza ni wale waliopata alama 100 - 250 ambao jumla yao ni 3,982 (Wavulana 1916 na Wasichana 2,066) sawa na 62.2%. Wanafunzi ambao hawakupata nafasi kuendelea na masomo ni 2,421 (Wavulana 1,148 na Wasichana 1,273) sawa na 38.6% jumla ya shule 138 kati ya 146 zilizokuwa na watahiniwa.
Idadi ya wanafunzi wa darasa la VII waliofanya, waliofaulu, waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza na kiwango cha ufaulu kuanzia mwaka 2002 hadi 2013
HALI HALISI YA UFAULU KWA MIAKA 10 MFULULIZO
|
|
WALIOSAJILIWA
|
WALIOFANYA
|
WALIOFAULU
|
ASILIMIA
|
||||||
N/O
|
MWAKA
|
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
ME
|
KE
|
JML
|
%
|
1
|
2004
|
4061
|
4061
|
8122
|
3958
|
4335
|
8293
|
1708
|
1469
|
3177
|
38.31
|
2
|
2005
|
3818
|
4172
|
7990
|
3358
|
4129
|
7487
|
2130
|
1819
|
3949
|
52.74
|
3
|
2006
|
3016
|
3136
|
6152
|
2965
|
3114
|
6079
|
2179
|
2072
|
4251
|
69.93
|
4
|
2007
|
3443
|
3626
|
7029
|
3265
|
3478
|
6743
|
2435
|
2255
|
4690
|
69.55
|
5
|
2008
|
4273
|
4411
|
8684
|
4231
|
4372
|
8603
|
2346
|
2350
|
4696
|
54.5
|
6
|
2009
|
4388
|
4367
|
8775
|
3931
|
4065
|
7996
|
1823
|
1580
|
3403
|
42.56
|
7
|
2010
|
3042
|
3038
|
6080
|
2984
|
3005
|
5989
|
1730
|
1449
|
3179
|
53.09
|
8
|
2011
|
4541
|
4752
|
9293
|
4370
|
4820
|
9190
|
2922
|
2354
|
5276
|
57.4
|
9
|
2012
|
3403
|
3643
|
7046
|
3350
|
3628
|
6978
|
2466
|
2760
|
5226
|
74.69
|
10
|
2013
|
3111
|
3377
|
6488
|
3064
|
3339
|
6403
|
1916
|
2066
|
3982
|
62.19
|
3 Changamoto zinazoathiri maendeleo ya taaluma
Ufaulu wa mtihani kwa watahiniwa wanaomaliza elimu ya msingi una kabiliana na changamoto mbalimbali kama zifuatazo:
Upungufu mkubwa wa walimu
Upungufu mkubwa wa nyumba za walimu
Kukosekana kwa chakula cha asubuhi/mchana kwa baadhi ya shule
Ukosefu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia
Ukosefu wa madarasa na walimu wa awali katika baadhi ya shule za msingi
0 MIKAKATI YA KUINUA UBORA WA ELIMU - 2014
Kuongeza idadi ya udahili wa walimu wa fani mbalimbali
Wanafunzi kuwa na chakula cha mchana shuleni
Kusogeza huduma za elimu pale inapostahili
Walimu kuimarisha usimamizi, Kuimarisha mazingira
Kuimarisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia
Kuwa na uwiano wa 1:1 wa vitabu kwa wanafunzi
Kuwa na walimu mahiri wa KKK katika kila shule
Kuwa na elimu ya kutosha juu ya matumizi ya OMR.
Kupunguza kero za walimu kuangalia haki na wajibu wa walimu
Kuwa na mafunzo kabilishi juu ya mitaala.
Kwa kutumia walimu mahili katika mafunzo yatolewe kwa walimu wengine
Kuwawezesha walimu kwa kuwa na ukaguzi wa ndani
Kuwawezesha wakaguzi kukagua shule nyingi kwa mwaka
Kuhamasisha jamii kuwa shule ni mali yao
Kuwa na mashamba darasa shuleni ili kupata chakula.
Kuhamasisha watu wenye uwezo wa kuchangia chakula shuleni.
Kuelimisha jamii kuwa shule ni mali yao.
Kuelimisha jamii pia kuwa wao pia ni moja ya jamii ya pale waliopo.
Kuwajengea uwezo wa masomo walimu wakuu na walimu
Kuboresha utaratibu wa kushughulikia masuala ya walimu.
KITENGO CHA ELIMU YA WATU WAZIMA
Idadi ya vituo/madarasa ya MEMKWA ni 19
(i) idadi ya wanafuzi wote wa MEMKWA 2014
KUANDIKA
|
WAVULANA
|
WASICHANA
|
JUMLA
|
KUNDIRIKA LA I
|
99
|
108
|
209
|
KUNDIRIKA LA II
|
62
|
57
|
119
|
JUMLA KUU
|
161
|
137
|
326
|
(ii) taarifa ya matokeo ya mtihani kwa wanafunzi wa MEMKWA waliofanya mtihani mwaka 2013
Wanafunzi wa MEMKWA kundirika la I waliofanya mtihani wa darasa IV mwaka 2012
WAV
|
WAS
|
JUML
|
87
|
72
|
152
|
Waliofaulu na kuingia darasa la V (mfumo rasmi)
WAV
|
WAS
|
JUML
|
74
|
50
|
124
|
Wanafunzi wa MEMKWA kundirika la II, waliofanya mtihani wa darasa VII – 2012
WAV
|
WAS
|
JUML
|
32
|
38
|
70
|
Wanafunzi wa MEMKWA kundirika la II waliofaulu na kujiunga kidato cha kwanza 2014
WAV
|
WAS
|
JUML
|
15
|
25
|
40
|
|
|
|
B: MUKEJA
Idadi ya vituo/madarasa ya MUKEJA yaliyopo katika Halmashauri ya Iringa ni 66 yaliyohai mpaka sasa hivi ni 35
Idadi ya wanakisomo waliopo katika madarasa
Walio katika madarasa ya K.K.K
ME 304
KE 693
JUMLA 997
Shughuli za ugani (SU)
ME 162
KE 329
JUMLA 491
JUMLA ya wanakisomo kwa madarasa yote ni
ME 833
KE 1655
JUMLA 2488
C: Idadi ya madarasa/mduara kwa kila aina ya programu
Darasa KCM
|
KCK
|
|
|||||
K.K. K
|
SU
|
UMALI
|
UMALI
|
SU
|
UST
|
Elimu masafa
|
JUMLA
|
8
|
6
|
8
|
27
|
15
|
2
|
-
|
66
|
K.K.K – Kusoma, kuandika na kuhesabu
SU – Shughuli za ugani (kilimo, ufugani n.k)
UMALI Shughuli za uzalishaji mali (mfano: ujaliamali, vikoba n.k)
UST – Ufundi stadi (uselemala, ushonaji n.k)
E: IDADI YA VITUO VYA MTAALA MPYA NA FANI ZAKE
Tanangozi (sayansikimu)
Kibena (sayansikimu)
Tungamalenga (kilimo)
Kilichohai na kinatoa huduma ni kituo cha Tanangozi
F: IDADI YA VYUO VYA UFUNDI STADI VYA SERIKALI NI VIWILI
Tanangozi
Kalenga
Idadi ya vituo vya ufundi stadi usinyo vya serikali ni 14 (binafsi na mashirika ya dini)
Fani zinazofundishwa vituo vya serikali (Tanangozi)
Sayansikimu
Wanaume
|
Wanawake
|
Jumla
|
-
|
7
|
7
|
Useremala
Wanaume
|
Wanawake
|
Jumla
|
10
|
-
|
10
|
Uashi
Wanaume
|
Wanawake
|
Jumla
|
7
|
-
|
7
|
Jumla ni 24
Idadi ya wanafunzi wanaosomo elimu masafa(Distance learining) ni 4 wapo katika kituo cha Ifunda shule ya msingi
MAFANIKIO
Wanafunzi wa ufundi stadi waliofaulu kuanzia 2012 hadi 2013 ni 33
Wanafunzi wa MEMKWA waliofaulu kuanzia 2010 hadi 2012 wavulana ni 67 na wasichana 60 jumla ni 127
Wananchi kupitia madarasa ya Elimu ya Watu Wazima wanakisomo 133 wameweza kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.
Idara ya Elimu imeweza kusambaza viti 20,200 katika kipindi cha 2013 katika shule za Msingi
Wananchi mbalimbali wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu na wale wanaohitaji kujiendeleza wamehamasishwa kujiunga na mfumo wa elimu masafa (odl) kupitia sekondari 12 walihitimu elimu ya sekondari kupitia kituo cha sekondari Mseke.
CHANGAMOTO NA UTATUZI
Baadhi ya walimu kutokuwa na ari ya kufundisha
Idara ya elimu wilaya, waratibu, walimu wakuu tunafanya vikao vya kielimu na kubaini changamoto na namna ya kuzitatua kwa wakati
Malipo ya honoralia kutokutoka kwa wakati
Idara inalipa honoralia kulingana na upatikanaji wa fedha
Mtaala wa ufundi stadi bado haujaboreshwa ili uweze kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia
Kutoa ushauri kwa mamlaka zinazohusika ili utatuzi wa tatizo hilo uzingatiwe
Vituo vya ufundi havina na vyombo vya kutosha
Kutafuta wahisani watakaoweza kusaidia ununuzi wa vyombo hivyo
KITENGO CHAUTAMADUNI NA MICHEZO
KAZI ZA KITENGO / MAJUKUMU
Kukuza na kuendeleza Utamaduni wa Mtanzania
Kusimamia sera zinazohusiana na shughuli za Utamaduni kama Sera ya Utamaduni, Sera ya Michezo, Sera ya Vijana n.k.
Kukuza, kusimamia na kuhimiza matumizi ya Lugha ya Kiswahili na kusimamia maendeleo yake.
Kukuza na kuendeleza Mila na Desturi nzuri kwa jamii
Kuhimiza nidhamu na uwajibikaji kwa jamii
Kusimamia maendeleo ya shughuli za sanaa na wasanii.
Kusimamia maendeleo ya michezo yote
Kusimamia maendeleo ya shughuli za vijana
Kuhimiza moyo wa uzalendo wa Taifa letu.
Kuratibu na kusimamia vyama vya michezo katika wilaya
Kuratibu shughuli za Mwenge wa Uhuru.
VIKUNDI VYA SANAA:
Halmashauri ya wilaya ya Iringa ina jumla ya vikundi vya Sanaa 80 kati ya hivyo vikundi 40, vimesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Vikundi hivyo vinajishughulisha na fani za Ngoma, Ngoma za Asili, Maigizo, Kwaya, Muziki wa kizazi kipya, Muziki wa Asili, Ngonjera, Mashairi, Utambaji wa hadithi
na Majigambo.
VYA MICHEZO:
Katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa tuna jumla ya Vilabu vya Mpira wa miguu 60 kati ya hivyo jumla ya Vilabu 16 vimesajiliwa. Pia kuna chama cha mpira wa miguu kimoja.
VIKUNDI VYA VIJANA:
Halmashauri ina jumla ya vikundi vya vijana 180 ambavyo vinajishughulisha na shughuli mbalimbali za maendeleo kama vile, kilimo, ufugaji, ufugaji nyuki, ufyatuaji wa tofali, utengenezaji wa vigae na biashara ndogondogo. Jumla ya vijana 1360 wanafanya shughuli hizo.
CHANGAMOTO:
Vikundi vingi vya sanaa, sanaa zao hazipo kibiashara kwa kukosa stadi za ujuzi
Ukosefu wa fedha wa kuendesha mafunzo ya sanaa kwa wasanii
Uongozi wa Vilabu kutokuwa makini
Uhaba wa walimu wa michezo mbalimbali
Ukosefu wa mitaji kwa vijana
Ukosefu wa elimu ya Ujasiliamali kwa vijana.
MIKAKATI YA UTEKELEZAJI:
Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tutaandaa Semina za Ujasiliamali kwa vijana
Mafunzo ya Stadi za ujuzi zitatolewa.
Mafunzo kwa walimu wa michezo yameanza kutolewa na yataendelea kutolewa.
Halmashauri inatenga fedha kwa ajili ya kuwakopesha vijana pia kwa kushirikiana na Asasi zisizo za Kiserikali zinaendelea kutoa mikopo.
MAONI NA USHAURI
Mambo yafuatayo hayanabudi kufanyika ili kuwezesha hali ya ufaulu wa wanafunzi kuwa mzuri kwa kuzingatia nafasi za wadau wote ambao ni:
Wanafunzi, walimu, wazazi / walezi/jamii na serikali kila kundi litimize wajibu wake katika kutekeleza majukumu ya elimu ili kufanya elimu kuwa bora zaidi
HITIMISHO:
Ufaulu katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2013 umepanda katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na kufikia malengo ya BRN. Ufaulu huu umepelekea Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kushika nafasi ya 3 kimkoa. Idara ya Elimu msingi imeweka lengo la kuongeza ufaulu kufikia asilimia 100 kwa mwaka 2014 kwa kujiwekea mikakati madhubuti ya usimamizi na uendeshaji wa elimu kwa shule za msingi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa