Halmashauri inatekeleza miradi ya maji katika vijiji 10 chini ya “Program” ya Maji (Rural Water Supply and Sanitation Programme – RWSSP). Vijiji vifuatavyo vimechaguliwa; Igangidung’u, Malinzanga, Kikombwe, Mfyome, Itengulinyi- Lumuli, Isupilo na Weru.
Vijiji vya Izazi na Migoli vimeingizwa baada ya vijiji vya Chamundindi na Ikengeza kujengewa mradi wa maji wa Ismani kwa ufadhili wa Serikali ya Italia.
Ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Igangidung’u umekamilika kwa 100% na miradi ya maji mingine 7 wakandarasi wanaendelea na ujenzi ambapo Utekelezaji wake upo katika hatua kama ifuatavyo;
Mradi wa Maji wa Mtiririko katika kijiji cha Malinzanga hatua iliyofikiwa ni kama ifuatavyo;
- Ujenzi wa Mtego wa Maji (Intake) umekamilika
- Ujenzi wa vituo 26 vya kuchotea Maji umekemilika
- Ujenzi wa Tanki la kuifadhia Maji la ardhini lenye ujazo wa lita 150,000 umekamilika
- Ujenzi wa Ofisi kwa ajili ya Jumuiya ya watumiaji Maji umekamilika
- Ujenzi wa birika la kunyweshea mifugo umekamilika
- Uchimbaji wa mtaro kwa ajili ya kulaza mabomba umbali wa kilometa 23 umekamilika
- Kazi ya ununuzi wa bomba inaendelea
Kwa wastani utekelezaji wa Mradi huu wa kijiji cha Malinzanga.
Mradi wa Maji wa Kupampu wa kijiji cha Kikombwe hatua iliyofikiwa ni kama ifuatavyo;
- Ujenzi wa Mtego wa Maji (Intake) umekamilika
- Ujenzi wa Tanki dogo lenye lita 10,000 (SampTank) la kuhifadhia Maji baada ya kuvutwa na mashine kutoka kwenye Mtego wa Maji umekamilika.
- Ujenzi wa Tanki la kuhifadhia Maji la ardhini lenye ujazo wa lita 150,000 umekamilika
- Ujenzi wa nyumba ya kuifadhia pampu (Pump House) umekamilika
- Ujenzi wa vituo 15 vya kuchotea Maji umekamilika.
- Uchimbaji wa mtaro kwa ajili ya kulazia mabomba kilometa 16 umekamilika
- Ujenzi wa birika la kunyweshea mifugo umekamilika
- Ujenzi wa Ofisi kwa ajili ya Jumuiya ya Watumiaji Maji umekamilika
Mradi wa Maji wa kupampu katika kijiji cha Mfyome shughuli zilizofanyika ni;
- Ujenzi wa Ofisi kwa ajili ya Jumuiya ya watumiaji Maji umekamilika
- Uchimbaji Mtaro na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 12 umekamilika
- Ujenzi wa vituo 17 vya kuchotea Maji umekamilika
- Uchimbaji wa visima virefu 2 umekamilika na Maji yamepatikana
Kwa wastani utekelezaji wa Mradi huu wa Maji katika kijiji cha Mfyome umefikia 90%.
Mradi wa Maji wa Mtiririko katika vijiji vya Itengulinyi, Isupilo na Lumuli ambao unajulikana kwa jina la Isupilo “Grouped Scheme” umetekelezwa kwa;
- Ujenzi wa Ofisi kwa ajili ya Jumuiya ya watumiaji Maji umekamilika
- Ujenzi wa intake unaendelea
- Uchimbaji mtaro na ulazaji mabomba unaendelea
- Ujenzi wa matanki ya kuhifadhia maji unaedelea
Kwa wastani utekelezaji wa Mradi huu wa Maji katika vijiji vya Itengulinyi, Isupilo na Lumuli.
Mradi wa Maji wa Mtiririko katika kijiji cha Weru shughuli zilizofanyika ni kama ifuatavyo;
- Ujenzi wa mitego miwili (2) ya Maji (Intake) umekamilika
- Ujenzi wa matanki mawili (2) ya kuhifadhia Maji ya ardhini moja lenye Ujazo wa lita 50,000 na lingine lita 25,000 umekamilika.
- Ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea Maji umekamilika.
- Ujenzi wa Ofisi kwa ajili ya Jumuiya ya Watumiaji Maji umekamilika
- Uchimbaji mtaro na ulazaji mabomba unaedelea
- Ujenzi wa intake unaendelea
- Ujenzi wa matank ya maji umekamilika.
Kwa wastani utekelezaji wa Mradi wa Maji wa kijiji cha Weru umefikia 85%. Mradi wa Maji wa Mtiririko wa kijiji cha Malagosi unaofadhiliwa na wastaafu wawili Raia wa Canada Bob & Hellen bado unaendelea na shughuli zilizofanyika ni kama ifuatavyo.
- Ujenzi wa Tanki la kuhifadhia Maji la ardhini lenye ujazo wa lita 50,000 umekamilika.
- Ujenzi wa Mtego wa Maji (Intake) umekamilika
Kwa wastani utekelezaji wa Mradi wa Maji wa kijiji cha Malagosi umefikia 60%. Mradi wa Maji wa Mtiririko wa kijiji cha Ihomasa unaofadhiliwa na kanisa la Anglicani Dayosisi ya Ruaha kupitia shirika la “Emmanuel International” bado unaendelea na shughuli zilizofanyika ni Ujenzi wa Mtego wa Maji (Intake) ambayo imekamilika
Kwa wastani utekelezaji wa Mradi huu wa Maji katika kijiji cha Ihomasa umefikia 40%.
Uchimbaji wa visima viwili (2) katika kijiji cha Mtera, Makatapora na Kinyali unaofadhiliwa na shirika la UNICEF umekamilika na Maji yamepatikana. Mradi wa maji wa Ismani bado unaendelea na ukarabati chini ya ufadhili wa Serikali ya Italia.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa