DC IRINGA: MAFANIKIO YA UHIFADHI YAGUSE MAISHA YA WANANCHI
Mkuu Wa Wilaya ya Iringa Mhe. Benjamini Sitta amesema kuwa mafanikio ya jumuiya ya MBOMIPA yanatakiwa kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja na miradi isimamiwe ipasavyo ili kutoa matokeo Chanya.
Mhe. Ameyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka na uwasilishaji wa taarifa yam waka 2024/2025 ya maendeleo ya Jumuiya hiyo ya MBOMIPA. Mkutano huo umefanyika Desemba 19, 2025 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria Manispaa ya Iringa.
Amesema kuwa mafanikio ya uhifadhi yanaongezeka na yanatakiwa kugusa maisha ya mwananchi mmoja mmoja nasiyo kutumika kwenye shughuli zisizokuwa naa manufaa huku akiagiza miradi isimamiwe na kutoa matokeo yaliyo bora
Taarifa ya uwasilishwaji huo inaeleza kuwa, mapato ya jumuiya hiyo yameongezeka kutoka Milioni 64 mwaka 2022/2023 hadi milioni 700 mwaka 2024/2025 na kupelekea mgao wa fedha kwa vijiji kuongezeka kutoka Milioni 30 kufikia Milioni 258 na kusaidia kuboresha huduma za kijamii ikiwemo miundo mbinu , ajira kwa vijana , na afya kwa kutoa bima za afya kwa kaya 105.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa