KITUO CHA AFYA MAHUNINGA KUZINDULIWA JANUARI 20, 2026
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, Desemba 18, 2025 amefanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa Kituo cha Afya Mahuninga kilichopo Kata ya Mahuninga, kwa lengo la kujionea hatua za ukamilishaji wa mradi huo.
Katika ziara hiyo, Mhe. Kheri James amewashukuru wananchi wa Mahuninga kwa uvumilivu wao kwa kipindi chote walichokuwa wakifuata huduma za afya umbali mrefu, huku akiwahakikishia kuwa ndoto ya kuwa na kituo cha afya cha karibu imetimia.
Aidha, ameagiza vifaa kufikishwa mara moja, akisisitiza kuwa ndani ya siku saba vifaa vyote viwe vimefungwa na ujenzi kukamilika rasmi ifikapo Januari 10, 2026, na huduma za afya kuanza kutolewa Januari 20, 2026.
Pia amewaomba wananchi kutunza na kulinda miundombinu yote iliyojengwa katika kituo hicho ili idumu na kuendelea kuwahudumia kwa muda mrefu.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa