OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA
FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MISITU
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji (W)
S. L. P 108,
IRINGA
2022
UTANGULIZI
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ina eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 20,576, kati ya hizo, eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 10,718.5 sawa na asilimia 52 ya eneo lote la Halmashauri limetengwa kama eneo la Hifadhi ya Taifa ya wanyamapori ya Ruaha, Pori la Akiba la Lunda Mkwambi na mabwawa na eneo lenye kilometa za mraba 9857.5 ndilo lililobaki kwa matumizi anuwai ya binadamu ikiwemo hifadhi za misitu na wanyamapori (WMA) sawa na asilimia 48 ya eneo lote la Halmashauri. Wilaya ipo kati ya nyuzi za Latitudo 7 00o and 8 30o Kusini na Longitudo 34o na 37o Mashariki. Kwa ujumla, Wilaya ipo katika mwinuko kati ya meta 900 na 2000 juu ya usawa wa bahari. Aidha, Wilaya inapokea mvua kati ya mm 500 na 1000 na jotoridi kati ya 10 na 30 oC. Wilaya ya Iringa ni moja ya Wilaya zinazounda Mkoa wa Iringa. Halmashauri ina Tarafa 6, Kata 28 na Vijiji 134.
Eneo la Halmashauri limejaliwa kuwa na raslimali nyingi za misitu ya kupandwa na misitu ya asili. Misitu ya kupandwa iliyopo ni ile inayopandwa na taasisi au watu binafsi katika maeneo wanayomiliki. Kwa sasa, maeneo yenye mashamba ya miti ya kupandwa yanakadiriwa kufikia hekta 30,000 (Tarafa ya Kiponzelo Hekta 20,000, Tarafa ya Mlolo Hekta 8000 na Tarafa ya Kalenga Hekta 2000). Miti inayostawi ni mikaratusi (Eucalyptus) na misindano (Pines). Misitu ya asili iliyopo ni ile ya Miyombo ikiwa imechanganyika na aina nyingine za miti kama vile Acacia, Terminalia na Combretum. Maeneo yaliyohifadhiwa na yasiyohifadhiwa yanakadiriwa kufikia hekta 250,000 za misitu ya asili.
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pia ipo katika eneo la kimkakati la Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT) na ipo katika kitovu cha eneo la Ihemi Cluster. Eneo hili lina sifa ya kuwa na mvua za kutosha na hali ya hewa inayostawi mazao mengi ikiwepo misitu.
Fursa zilizopo za uwekezaji katika sekta ya misitu ni pamoja na:-
Sekta ya misitu katika Wilaya imepiga hatua kubwa katika kuletea maendeleo wananchi na kuingizia Serekali mapato. Yafuatayo ni mafanikio yaliyopo katika sekta hii:-
Uwekezaji katika sekta ya misitu utawezesha ukuaji wa sekta ya misitu katika maeneo yafuatayo:-
Sekta ya misitu inategemea sana mazingira rafiki ya ufanyaji biashara kwa kuwa inahitaji mitaji mikubwa na wakati mwingine inahitaji muda mrefu ili mwekezaji kupata manufaa yatokanayo na uwekezaji wake. Kwa mantiki hiyo, mchango wa serikali unahitajika kwa kiwango kikubwa ili kujenga uwezo wa kujiamini wa wawekezaji. Huduma zinazotolewa na Serikali kwa wadau wa misitu ni pamoja na:-
#KARIBU WILAYA YA IRINGA
#MISITU INALIPA
#WEKEZA SASA
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa