IDARA YA MAJI
Eng. LUCAS MADAHA
MKUU WA IDARA YA MAJI
MAELEZO YA IDARA:
Idara ya Maji ni moja kati ya Idara zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Idara ya Maji ina jumla ya wataalam 14 wahandisi 3 na mafundi sanifu 11, Pia Idara ina watumishi wengine karani 1, Mtunza Ofisi 1, Walinzi 2, Wahudumu 2, na madereva 2, Idara ina gari moja na pikipiki 3 ambazo hutumika kufanikisha ufanyaji kazi wa kila siku.
SHUGHURI ZA IDARA
Shughuri kuu zinazofanywa na Idara ya Maji ni kutoa huduma ya ushauri wa kitaalamu juu ya matumizi ya maji, Kuunda na kusimamia Jumuiya za watumiaji maji.
MIRADI YA MAJI ILIYOTEKELEZWA NA INAYOTEKELEZWANA IDARA
Miradi ya Maji ya vijiji 10 yenye thamani ya bilioni 7 iliyopo chini ya Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira- RWSSP.
AINA ZA MIRADI NA HALI YA UPATIKANAJI WA MAJI KATIKA HALMASHAURI YA IRINGA
Na |
AINA YA MRADI |
IDADI |
1
|
Miradi ya maji ya mtiririko na mfumo wa bomba
|
16 |
2
|
Miradi ya maji ya visima inayosukumwa na mashine za diseli
|
3 |
3
|
Miradi ya maji mito inayosukumwa na mashine za diseli
|
2 |
4
|
Miradi inayosukumwa na umumu wa TANESCO
|
2 |
5
|
Miradi ya maji ya visima virefu inayosukumwa na umeme wa nguvu za jua
|
41 |
6
|
Miradi ya maji ya chemche inayosukumwa na umeme wa nguvu za jua
|
1 |
7
|
Miradi ya maji ya visima virefu inayosukumwa na pampu za mkono
|
100 |
8
|
Miradi ya maji ya visima vvifupi inayosukumwa na pampu za mkono
|
67 |
Hali ya upatikanaji wa maji katika halmashauri nzima ya Iringa ni 69.7%, idara inaendelea na juhudi mbalimbali ikiwa ni kuwashirikisha wadau katika kusaidia kuongeza hali hii ya upatikanaji wa huduma ya maji kufikia 85% ifikapo mwaka 2020.
CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI IDARA
PICHA MBALIMBALI ZA MIRADI
Tanki la maji la Mradi wa Malinzanga Mtego wa maji Mradi wa Malinzanga
Kituo cha maji Mradi wa Maji ya kisima Mashine ya kuchuja maji na kutoa maji safi na kinachosukumwa na nguvu ya umeme jua salama inayotumia nguvu ya umeme jua katika shule ya msingi Katenge kituo cha afya Kimande
Ujenzi wa tanki la juu la maji lenye ujazo wa Uwekaji wa mfumo wa umeme jua na lita 150,000 la Mradi wa maji Migoli Mtera uchimbaji mitaro na uwekaji mtandao wa maji ukiendelea
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa