Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ni moja kati ya Wilaya mbili zilizoanzisha Mkoa wa Iringa Mwaka 1964. Wilaya ya pili ni Njombe, Mwaka 1970 Wilaya ilipunguza eneo lake kwa kuanzisha Halmashauri ya wilaya ya Mufindi na baadae mwaka 2006 ilianzishwa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo.
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa inapakana na Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa(Mkoa wa Dodoma) kwa upande wa kaskazini, Halmashauri ya Kilolo kwa upande wa Mashariki, Halmashauri ya wilaya ya Mufindi upande wa Kusini, Halmashauri ya wilaya ya Chunya(Mkoa wa Mbeya) kwa upande wa Magharibi na Halmashauri ya wilaya ya Manyoni kwa upande wa Kaskazini Magharibi.
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ina ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 20,413.98.
Makao Makuu ya Halmashauri yanapatikana katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa eneo la Gangilonga.
Katika utambulisho wa Kimataifa Halmashauri ya wilaya ya Iringa inapatikana katika latitudo 7.0' na 8.30' kusini mwa ikweta na katika longitudo 34.0' na 37.0' Mashariki mwa Greenwichi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa