IDARA YA MAZINGIRA NA USAFISHAJI
Idara ya Usafishaji na Mazingira ina vitengo viwili ambavyo ni Kitengo cha Usafishaji na Kitengo cha Mazingira.
Idara ya Usafishaji na Mazingira ina jumla ya wataalamu wanne (04), ambapo Mkuu wa Idara mmoja (01) na Maafisa Mazingira watatu (03).
SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA IDARA YA MAZINGIRA
Kusimamia usafi wa majengo, maeneo ya wazi, barabara na mifereji.
Utunzaji, uchambuaji na usafirishaji wa taka
Uchambuaji, utupaji taka na uendeshaji wa dampo la kisasa (Sanitary Landfill)
Udhibiti wa uchafuzi wa mazingira, ardhi, maji, hewa na sauti.
Utunzaji na upendezeshaji mazingira (Beautification):- kupanda miti, majani na maua (greening), kukatia miti na majani (pruning)
Upimaji na ufuatiliaji wa tathmini za athari za kimazingira na kijamii (Environmental Impact Assessment- EIA), katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Kutoa elimu ya mabadiliko ya tabianchi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa