Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ndg. Robert Masunya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kutokomeza Ukatilidhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ngazi ya Halmashauri ametoa wito kwa wajumbe wa kamati na wadau wengine kuwa mabalozi wazuri kwenye jamii wanakotoka juu ya kutokomeza ukatili.
“Tutoke hapa tukatimize majukumu yetu kwenye vikao mbalimbali za vijiji, kata na wale wa vyombo... wote tukiondoka kwa Pamoja, tukaenda kuelimisha jamii tukawa mabalozi wazuri kwenye jamii zetu maana yeke tuna uhakika wale ambao wana taaluma za Habari wakaelimisha vizuri jamii zetu, wale wanaoishi ndani ya jamii wakaelimisha na kuchukua hatua tuna uhakika tunakwenda kutokomeza ukatili wa wanawake na Watoto”. amesema Ndg. Masunya
Ameyasema hayo alipokuwa kwenye kikao maalumu cha robo cha kuzindua mpangokazi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa awamu ya pili (MTAKUWWA II) ngazi ya Halmashauri kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo Novemba 21, 2025.
Katika kikao hicho taarifa za kutoka maeneo mbalimbali ya utendaji zimewasilishwa na kujadiliwa kwa kina ili kupata ushauri na hatua stahiki juu ya kutokomeza ukatili kwenye jamii
Kwa upande wake katibu wa kameti ambaye ni Afisa Ustawi (W) Bi. Gladness Amulike amepata fursa ya kuwasilisha mhutasari wa Mpango kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA II) 2024/2025 – 2028/2029 kwa wajumbe ili kupata uelewa wa Pamoja.








Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa