Ahimiza matumizi sahihi ya mifumo mbalimbali kwa wa watumishi ili kuendana na kasi ya sasa ya Sayansi na teknolojia na hivyo kutoachwa nyuma hususani mfumo wa tathmini.
Katinu Tawala wa Wilaya ya Iringa Ndugu Bernard Urassa ametoa pongezi kwa walimu na wadhibiti ubora wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa ufaulu mzuri kufuatia matokeo ya Mtihani wa kidato cha Sita yaliyotoka hivi karibuni.
Ndugu Urassa amezungumza hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya mfumo wa tathmini uthibiti wa ubora kwa walimu yaliyofanyika katika ukumbi wa Sias ani Kilimo Julai 09, 2025.
Aidha Ndugu Urassa ametoa wito kwa watumishi kuhakikisha kuwa wanaendana na kasi ya mifumo mbalimbali katika zama hizi za sayansi na teknolojia na hivyo kutoachwa nyuma.
Kwa upande mwingine katibu wa CWT Wilaya ya Iringa ameunga mkono pongezi za katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa Ndugu Urassa na kuongeza kuwa hiyo ni kazi kubwa inayofanywa na walimu wanaojituma hadi usiku na hivyo kuomba kuwa kuna haja ya kuangalia upya maslahi ya walimu hawa ikiwemo kutokuwekewa makato kwenye nyumba wanazoishi ili kuwapa hamasa ya kujituma zaidi.
Mafunzo haya ya tathmini yameandaliwa na Idara ya Uthibiti Ubora ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambayo inatekeleza tathminiza jumla, ufuatiliaji na maalumu katika asasi 203 yaani shule za awali na msingi na sekondari.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa