Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James ametoa wito kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuwaandaa wananchi ili waweze kunufaika na miradi mikubwa ya kimkakati ambayo inatekelezwa kwenye eneo lao.
Mhe. Kheri James amezungumza hayo alipokuwa kwenye ziara ya kuongea na watumishi wa makao makuu katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa yaliyopo Ihemi mapema Julai 18, 2025.
Miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ni Pamoja na upelekaji wa umeme vijijini ambapo kwa Wilaya ya Iringa vijiji vyote tayari vimeshafikiwa na umeme nah atua iliyopo ni ujazilizi kwenye vitongoji, ujenzi wa Barabara ya Iringa – Msembe (Ruaha National Park), skimu ya umwagiliaji Tarafa ya Pawaga wa zaidi ya Bilioni 54, na miradi mingine ya utoaji huduma kama elimu na afya.
“Ukiachilia mbali miradi ya utoaji huduma, hii miradi mikubwa miwili inatafsiri dhamira ya kweli ya ni namna gani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amedhamiria kuona maisha ya watu wa Iringa yanabadilika, Uchumi wa watu wa Iringa unabadilika, watu wanabadilika na ustawi wao unakua kutokana na uwekezaji mkubwa unaokwenda kufanyika”
Aidha Mhe. Kheri amewakumbusha watumishi kuhakikisha kuwa fedha zinazolewa kwa ajili ya miradi zinatumika vizuri na kuhakikisha matokeo yaliyokusudiwa yanaonekana katika utekelezaji wa miradi husika.
Kwa upande wa ukusanyaji wa mapato, Mkuu wa Mkoa amewataka watumishi wa Iringa DC kuwa wabunifu kubuni vyanzo vya mapato na kuongeza juhudi katika ukusanyaji ikiwa ni Pamoja na kuona uwezekano wa kuwa na stendi zinazofanya kazi kuongeza mapato na kuangiza kufanyika kwa kikao na wadau ili stendi ya Migoli ianze kufanya kazi.
Kwa upande wao watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wamemshukuru na kumpongeza Mhe. Kheri James kwa kuaminiwa na kuteuliwa na Mhe. Rais kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na kuahidi kutekeleza kwa vitendo ushauri na maelekezo yaliyotolewa.
#Iringa Imara Tutaijenga kwa Umoja na Uwajibikaji.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa