Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Benjamin Sitta ametoa wito kwa Maafisa lishe na viongozi wa Idara zingine kukaa Pamoja, kuchakata na kuja na kanuni itakayowasaidia watu hasa akinamama wajawazito kupata lishe bora kwa uendelevu ili kupunguza utegemezi wa matumizi ya vidonge.
Mhe. Sitta ameyasema hayo wakati wa kikao cha tathmini ya Mkataba wa lishe kilichofanyika Agosti 12, 2025 katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo Iringa.
Aidha Mhe. Sitta ameongeza kuwa kitendo cha kuwa na utegemezi mkubwa wa vidonge kwa akinamama wajawazito Pamoja na changamoto zake ni Ushahidi kuwa lipo tatizo ambalo linahitaji majibu ya kiutafiti. Kwamba wakati mwingine matumizi ya vidonge hayazingatiwi kwa usahihi kutokana na changamoto za mabadiliko ya mama mjamzito lakini kukiwa na ulaji unaozingatika kanuni utapunguza changamoto nyingi za mjamzito wakati wa kujifungua.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Sitta ametoa pongezi kwa Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri, viongozi wa Idara na wadau wote wa masuala ya lishe kwa juhudi mbalimbali zilizopelekea kuwa na hali nzuri kwenye masuala ya lishe.
Kwa upande wake Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi. Aveline Selemani akisoma taarifa ya mpango wa utekelezaji wa afua za lishe amesema, mwaka 2025/2026 Halmashauri imepanga kutekeleza afua 28 kutoka Idara saba ambazo ni; Afya, Mifugo, Uvuvi, Kilimo, Maendeleo ya Jamii, Elimu Sekondari na Elimu Msingi kwa kushirikiana na UNICEF.
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo amba oni World Vision Tanzania, Care, CEFA, na ASF wanaotekeleza afua za lishe wamepunguza sana kiwango cha udumavu na wenyeviti wa vijiji kutoka vijiji 134 wamepatiwa mafunzo ya usimamizi wa masuala ya lishe ngazi ya jamii.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa