77 2023, Yafana Katika Kata ya Ilolompya
Katika kusherehekea Maadhimisho ya Kilele cha Sikukuu ya Sabasaba, wananchi wa Kata ya Ilolompya wameomba Kiwanja cha Sabasaba kuitwa jina la “Kiwanja cha Sabasaba cha Halima Dendego” ili kutoa heshima kwa kiwanja hicho, kwa sababu ni mara ya kwanza Mkuu wa Mkoa wa Iringa wa kwanza kukanyaga kiwanja hicho.
Tukio hilo limetokea Julai 10, 2023 katika Kuadhimisha Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Sabasaba, na kwamba ombi hili limetolewa na Diwani ya Kata ya Ilolompya kwa niaba ya wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego amesema kuwa, “nimefurahishwa na maandalizi ya Maadhimisho haya, kwani imefanya kuamsha ari ya wananchi kujitokeza kuonesha biadhaa zao na mambo mengi ya utamaduni”. Pia nimekubali uwanja huu uitwe Uwanja wa Sabasaba wa Halima Dendego”.
Pamoja na mambo mengine Mheshimiwa Dendego ametoa maagizo kwa Mkurugenzi kuwa, aanze maandalizi ya upimaji wa kiwanja hicho na kwamba ujenzi wa kiwanja uanze mara ifikapo Septemba 30.
“Uwanja huu ukijengwa utakuwa uwanja wa Maonesho ya Sabasaba na Nanenane kila mwaka. Kimkoa tutafanya maadhimisho haya katika viwanja hivi ili wananchi waje waoneshe bidhaa zao na kuongeza kipato”.
Akisoma taarifa fupi wakati wa Maadhimisho hayo Diwani wa Ilolompya Mheshimiwa Fundi Mihayo amesema, “pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika maeonesho hayo, kuna changamoto ambazo haziishi kama, ugomvi kati ya wakulima na wafugaji na kuhitaji suluhu ya kudumu, umeme wa uhakika, mitandao (minara), vyombo vya fedha (benki) na usafiri” ni changamoto kubwa kwa Tarafa ya Pawaga”.
Pia wananchi wamomba kijiji cha Isele kuwa Lango la kuingilia Hifadhi ya Ruaha kwa ajili ya kuendeleza utalii, na kuongeza utalii wa utamaduni (ngoma na vyakula vya asili) katika Tarafa ya Pawaga.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Veronica Kessy amesema kuwa, changamoto zote zilizowasilishwa zimepokelewa na baadhi yake zimeanza kufanyiwa kazi.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W), Bi. Lucy Nyallu amewashukuru wananchi wa Kata ya Ilolompya kwa kuandaa maadhimisho hayo wakiongozwa na Mhe. Diwani pamoja na Wadau mbalimbali. Pia ameahidi kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Katika Kilele cha Maadhimisho hayo, Mheshimiwa Dendego ameweza kushuhudia fainali za michezo mbalimbali ikiwepo ngoma za asili na kandanda. Mechi ilikuwa kati ya Kata ya Mlowa Kijiji cha Malinzangana Kata ya Ilolompya kijiji cha Magozi, ambapo kijiji cha Magozi kiliibuka mshindi na kupata zawadi ya kiasi cha Shilingi Milioni Moja na Laki Tano (Tsh. 1,500,000/-).
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa