AFISA ELIMU SEKONDARI IRINGA DC ATEMBELEA NA KUKAGUA MAANDALIZI NA MAPOKEZI YA KIDATO CHA KWANZA 2025
Atembelea Shule mpya zilizojengwa kwa Mradi wa SEQUIP awamu ya tatu ambazo tayari zimeshaanza kupokea wanafunzi kwa kidato cha kwanza 2025
Afisa Elimu Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi Alice Nkwera ametembelea na kukagua shughuli za maandalizi ya mapokezi ya kidato cha kwanza 2025 katika shule mbalimbali Januari 13, 2025 wakati ambao mhula mpya wa masomo unaanza.
Akizungumza akiwa shule ya mpya ya sekondari Ugwachanya Bi. Nkwera ameishukuru na kuipongeza Serikali chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa shule mpya tano kiasi cha Bilioni 2.9. Shule hizo ni Pamoja na Ugwachanya Sekondari, Kimambe Sekondari, Lukuvi Sekondari na Kimande Sekondari na Magunga Sekondari ambazo mwaka huu 2025 zinapokea wanafuzi wa kuanza kidato cha kwanza.
“Namshukuru sana Mhe. Rais wetu Mama Samia ametuwezesha kutuletea hizi shule, atoto wamepunguziwa umbali, natumai Ugwachanya na shule zingine zitafanya vizuri sana. Amesema Bi Nkwera.
Aidha baadhi ya shule zinaendelea na ukamilishaji wa miundombinu kwenye maeneo yaliyokuwa bado kukamilishwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa shule zote zinakuwa na uwezo wa kupokea wanafunzi bila kikwazo chochote.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa