Maafisa Ugani wanolewa kwenda kuboresha Utendaji kazi.
Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa-DC
Akizungumza ufunguzi wa kikao hiko kilichofanyika leo katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo, Mkurugenzi Mtendaji Wakili Bashir Muhoja amewakumbusha Maafisa ugani kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kutimiza lengo la Serikali la kutoa huduma kwa wananchi kwa haraka na ubora.
Baada ya kufungua Kikao hiko Wakili Muhoja amewataka watumishi waendelee kusimamia mazao ya kimkakati ya Halmashauri ambayo ni Pamba, Parachichi,Kahawa na Alizeti katika maeneo wanayotoka ili wananchi waweze kunufaika na kilimo cha mazao hayo ya kimkakati.
Akiwasilisha mada ya lishe, Afisa lishe wa Wilaya Bi.Evaline Selemani amesema ni wakati sasa Maafisa Ugani kuwaeleza wananchi umuhimu wa kuhifadhi mazao ya chakula ili kuzuia kupata sumukuvu.
Bi. Selemani amesema iwapo wananchi watapata elimu watakuwa wamesaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza udumavu na hata saratani ambayo huweza kusababishwa na sumukuvu.
“Wananchi waelekezwe namna bora ya Uhifadhi wa Chakula kuanzia mazao yanapo kuwa yanatoka shambani kuvunwa hadi kufika nyumbani ili kuuvunja mnyororo huu wa kusambaa kwa sumukuvu”alisema na kuongeza
“Pia, wananchi wanapaswa kuyafahamu makundi makuu matano ya chakula na kula,sambamba na kuwa na mtindo bora wa maisha na kufanya mazoezi. Lakini pia wanapaswa kuzingatia umuhimu lishe kwa kipindi mama anapokuwa mjamzito, lishe ya mama anayenyonyesha na lishe ya mtoto mwenye umri wa chini ya miaka miwili”alisema.
Kikao hiko ni muendelezo wa vikao vya Idara ya Kilimo yenye lengo ya kutathmini utendaji na utekelezaji wa majukumu na maagizo mbalimbali ya Serikali yenye lengo la kuboresha sekta ya Kilimo.
Naye,Mkuu wa Idara ya Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji Bi.Lucy Nyalu akifunga kikao hiko amewataka Maafisa Ugani hao kwenda kutekeleza maagizo ya Mkurugenzi Mtendaji ambayo aliyatoa katika ufunguzi wa kikao hiko ambayo ni kusimamia kilimo cha mazao ya kikakati.
Aidha, Bi.Nyalu amewakumbusha kufuata kanuni,sheria na taratibu za Kiutumishi na suala zima la kuwapa kipaumbele wateja pindi wanapohitaji huduma kutoka kwao hasa kwa msimu huu wa kilimo ambao unaendeleo.
Wakati huo huo,Afisa Kilimo David Chilagane ametoa rai kwa Maafisa ugani kutoa kusimamia suala zima la pembejeo kwa kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kuingiza sokoni pembejeo ambazo hazitambuliki na nyingine zimeisha muda wake wa matumizi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa