Madiwani walidhia na kupitisha rasimu ya Mpango wa Mapato na Matumizi ya 65,896,915,013.32 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa –DC)
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Iringa jana Februari 10 limeridhia na kupitisha rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka fedha 2022/2023 ambapo Halmashauri inatarajia kutumia Bilioni 65.896 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za uendeshaji na miradi.
Taarifa hiyo ilisomwa na Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw.Wapa Mpwehwe kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji kwa Baraza la Waheshiwa Madiwani ambapo wajumbe walijadili taarifa hiyo na kuipitisha.
Pamoja na kuipitisha rasimu hiyo ya Mpango wa Bajeti walishauri maboresho mbalimbali kuhusu namna ya kuongeza vyanzo vya mapato ili kuwezesha Halmashauri kukusanya na kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato.
Akichangia hoja Diwani wa Kata ya Ilolompya Mh. Fundi Mihayo alianza kwa kuipongeza serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mh. Samia Suluhu Hassain kwa kupunguza na kuondoa kero kubwa ya vyumba vya madarasa kupitia mradi wa No.5441 TCPR.
“Tunamshukuru sana kwa kweli imepunguza changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa kwa mwaka huu wa masomo 2022 hususani kwa shule za msingi ambapo baadhi ya watoto wamekuwa wakitembea umbali mrefu, na yeye ameliona hilo na kutoa fedha za kujenga shule shikizi”alisema.
Aidha,Waheshimiwa Madiwani wametoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji na Watumishi wote kwa ujumla kwa kufanya kazi nzuri husasani Idara ya Ujenzi ambapo walisema pamoja na upungufu wa Wahandisi bado wameweza kusimamia kazi na kutoa ushauri kwa wakati kwa mafundi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa