RC – Iringa atoa maazimio ili kuleta tija ya Program Shirikishi Jumuishi ya UVIKO -19.
Na. (Anton Ramadhan -Iringa DC)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Queen Sendiga ametoa maazimio ya kimkoa katika kuhakikisha zoezi Mpango Jumuishi Shirkikishi kuhusu chanjo ya UVIKO -19 ambayo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa zoezi la utoaji chanjo hiyo lilianza Agosti 4 mwaka wa 2021.
Mh.Sendika alitoa maazimio hayo wakati wa kikao cha Afya cha Mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo Septemba 28 mwaka huu wa 2021 lengo kuu la kikao hiko ni kuongeza elimu Jumuishi na Shirikisha kwa Jamii ili elimu na umuhimu wa chanjo na madhra ya UVIKO -19 iwapo hautapata chnjo hiyo.
Amesema ni wakati sasa kila mtaalam awe na taarifa sahihi juu ya suala zima la chanjo ili kuondoa hofu kwa jamii pindi inahitaji kufahamu kwa kina kuhusu suala zima la chanjo.
“Mwananchi hatokuwa na Imani iwapo mtaalam anaemtegemea kumuelimisha juu ya suala zima la chanjo ya UVIKO -19 akawa hana majibu au maelezo ya kina ya kumtoa shaka mwananchi huyo kwani hofu kubwa iliyotanda ilisababishwa na wananchi kutopata taarifa sahihi kutoka kwa watu au wataaalam sahihi”alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Afya,Uatawi wa Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bi.Catherine Sungura alisema kwa kufahamu umuhimu wa kuhabarisha Umma tayari Wizara hiyo imeingia mkataba na redio za ndani katika mikoa 26 ili kuwezesha kufikika kwa taarifa sahihi hususani maeneo ya vijijini.
“Tunatambua sio wananchi wote wanaweza kuwa na Luninga (Television) hivyo pamoja na kutumia vyombo na teknolojia mbalimbali za kufikisha elimu hiyo kipaumbele kimetolewa kwa redio za ndani”alisema Bi.Sungura.
Naye Dkt.Alexander May ambaye aliiwakilisha Ofisi ya Rais TAMISEMI alisema mpaka sasa Mkoa wa Iringa ulikuwa uko nyuma katika suala zima la chanjo na hali hii ilitokana na sababu mbalimbali na tayari mkatkati wa kukabiliana na hili umeshatekelewa ikiwa ni pamoja na kuongeza vituo vya utoaji chanjo hiyo ambapo kwa sasa Mkoa una vituo 231.
“Kila zahanati,vituo vya kutolea huduma za afya hospitali zinazoongozwa na kusimamiwa na taasisi za dini na hata huduma ya mkoba sasa inapatikana kupitia wataalam waliopewa mafunzo ya utoaji wa huduma hiyo”alisema
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa