Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imeingia makubaliano na kusaini mkataba wa kushirikiana kuendesha mradi wa Bomalang’ombe Village Company (BVC) ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa inamiliki hisa 50%, Kijiji cha Bomalang’ombe 22.5% na Kijiji cha Lyamko 22.5%.
Akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano baina vijiji hivyo yaliyofanyika katika ukumbi mdogo wa siasa ni kilimo Novemba 25, 2025, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Benjamin Sitta amesema mgogoro huo ni wa muda mrefu uliathiri uzalishaji mali wa kampuni inayojulikana kama bomalang’ombe village company BVC Kampuni iliyokuwa ikijishughulisha na uzalishaji wa nishati ya umeme, Kilimo, Ufugaji na usindikaji na kupelekea hasara kubwa kwa pande zote.
Vilevile Mhe. Sitta amesema makubaliano haya yanaenda kuleta manufaa makubwa sio tu kwa Halmashauri bali pia kwa vijiji husika.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Robert Masunya amesema kwenye vijiji hivyo kuna miradi zaidi ya minne kama uzalishaji wa umeme, uzalishaji miti ekari zaidi ya 400 ufugaji wa ngo’mbe na nguruwe hivyo kumalizika kwa mgogoro kutafanya miradi hiyo kuinuka na ku`fanya vizuri zaidi.
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa kijiji cha Bomalang’ombe na lyamko wamesema kumalizika kwa mgogoro huo kutafanya vijiji hivyo kunufaika ikiwa ni pamoja na ajira kwa wanawanchi wanaozunguka vijiji hivyo ambapo Mwenyekiti wa Kijiji cha Bomalang’ombe amemshukuru na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa jitihada zake hatimaye kufikia hatua ya makubaliano haya.








Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa