Baraza la Madiwani Kuwachukulia Hatua Watumishi Watovu wa Nidhamu
Baraza la Madiwani limeketi katika kikao chake cha Robo ya Nne na kutoa maazimia kwa kuwachukulia hatua watumishi watovu wa nidhamu.
Akitoa hotuba yake katika Baraza hilo lililoketi Agosti 12, 2023 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Stephen Mhapa amesema, “ni lazima tuwachukulie hatua watumishi ambao hawana nidhamu. Adhabu hizo ni muhimu ili kuweka heshima katika Utumishi wa Umma na kuondokana na kufanya kazi kwa mazoea”
Kati ya Watumishi watano waliochukuliwa hatua, watumishi watatu wamefutwa kazi na watumishi wawili wamekatwa mishahara yao kwa asilimia 15 kwa muda wa miaka mitatu.
Baraza hilo ambalo limefanyika kwa siku tatu mfululizo na kwamba Siku ya Kwanza ya tarehe 11/08/2023 ilikuwa ni kutoa taarifa mbalimbali za Madiwani hao kutoka sehemu zao za utawala. Siku ya Pili ya tarehe 12/08/2023 ilikuwa ni Baraza la Kawaida kwa Robo ya Nne pia kutoa maamuzi mbaimbali, na Siku ya Tatu 13/08/2023 ilikuwa ni Baraza Maalum la Kufunga Mwaka pia kufanya uchaguzi kwa ajili ya kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, kama kanuni zinavyoelekeza.. Uchaguzi ulifanyika na kwamba Diwani wa Kata ya Idodi Mheshimiwa Julius Modestus Mbuta aliweza kuchaguliwa na kuridhiwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri.
Pamoja na Mambo mengine Mheshimiwa Mhapa ameweza kutoa pongezi kwa Mkurugenzi na Wataalam wote kwa kazi nzuri ya maandalizi ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane). Sherehe hizo zilihitimiswa tarehe 08/08/2023, na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kushika nafasi ya Tatu Kitaifa, na kuwa mshindi wa Pili Kimkoa ikitanguliwa na Manispaa ya Iringa. Katika ushindi huo Mkulima Japhet Thomas Ngimbusi kutoka Kata ya Luhota Kijiji cha Ikuvilo amekuwa Mkulima Bora wa Kwanza Kimkoa na wa Pili Kitaifa, amezawadiwa kiasi cha Shilingi Milioni 6. Mfugaji Bora wa Ng’ombe wa Nyama Ndugu Matambile Mgemaa kutoka Kata ya Idodi Kijiji cha Tungamalenga amekuwa Mshindi wa Kwanza Kimkoa na kuzawadiwa kiasi cha Shilingi Milioni 2, hivyo kupelekea Halmashauri kupata Tuzo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa