Baraza la Watoto Wilaya Lazinduliwa
Hatimaye Baraza la Watoto limezinduliwa katika Halmashauri limezinduliwa ikiwa na lengo la kuwaleta watoto pamoja, kujadili matatizo yao na kuwajengea uwezo na ujasiri katika kila jambo.
Baraza hilo limezinduliwa Juni 10, 2024 katika Ukumbi wa Kanisa la Anglikana na kuchagua uongozi mpya baada ya uongozi wa awali kuisha muda wake.
Katika Hotuba yake ya ufunguzi wa uzinduzi wa Baraza hilo Mgeni Rasmi Mheshimiwa Stephen Mhapa ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri amesema, ameshukuru sana viongozi wa Mashirika kwa kuwezesha Baraza hili liundwe, na kushukuru uongozi wa Baraza uliopita kwa kuongoza vizuri katika kutekeleza majukumu yao.
“Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata akiwa Mzee”, Mheshimiwa Mhapa amenukuu maneno hayo kutoka katika Biblia Takatifu na kuwahusia wazazi watimize wajibu wao.
Naye Padre Emilyo Kindole ambaye ni Mlezi wa Baraza aliweza kutoa mafunzo mafupi kwa watoto na kuwahusia wazazi/walezi wasiwaumize wala kuwadhalilisha au kuwafanyia ukatili watoto. Pia amewaambia watoto kuwa wanapofanyiwa ukatili wanapaswa kusema kwa polisi, Mwenyekiti wa Mtaa, Afisa Maendeleo au kwa mtu anayemuamini ili aweze kupata msaada.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo Wilaya Bi. Saumu Kweka amewashukuru Wadau kwa kuandaa Baraza hilo na kusema kuwa, “Watoto mmeletwa hapa ili mjengewe uwezo wa kuwatetea watoto wenzenu. Hivyo mmechaguliwa ninyi ili muwe mfano na kuwaongoza watoto wenzenu kwenye kila jambo”.
Kupitia Baraza hilo, watoto walifanya uchaguzi wa uongozi na kupata Mwenyekiti Angel Robert Ng’anguli kutoka Kata ya Ulanda wa Shule ya Sekondari Kalenga Kidato cha Kwanza na Makamu wake Emanuel Nwenzi kutoka Kata yaa Migoli wa Shule ya Msingi Mtera Darasa la VI, Pia Katibu Natalia Sanga wa Kata ya Kihorogota wa Shule ya Msingi Isimani Darasa VII na Makamu wake Elisha Mfume wa Kata ya Itunundu wa Shule ya Sekondari Pawaga Kidato cha II, Kadhali Mtunza Hazina Jackline Mtove wa Kata ya Ifunda Shule ya Sekondari Lyandembela Kidato III na Makamu wake Resmida Mhangala wa Kata ya Maguliwa Shule ya Msingi Maguliwa Darasa la VII.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa