“Bendera ya Ushindi Ipo Mikononi mwa Walimu” – Dkt. Mutahabwa
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ni miongoni mwa Halmashauri zilizochaguliwa katika kuwajengea uwezo walimuu wa masomo ya Sayansi na Hisabati, ambapo kwa Halmashauri hiyo shule Tisa zimeweza kuchaguliwa na kushiriki mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yalitolewa na Wahadhiri kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania ambayo yalifanyika Januari 30, 2024 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria Tawi la Iringa, ambapo yaliongozwa na Kamishina wa Elimu Tanzania Dkt. Lyabwene Mutahabwa na kutoa Kauli Mbiu hiyo ya “Bendera ya Ushindi Ipo Mikononi mwa Walimu”.
Lengo la Mafunzo hayo ilikuwa ni kuwajengea Walimu uwezo na ubunifu na mafunzo ya Awali (Orientation) na kufundisha kwa vitendo kwa kutumia vifaa vya kwenye mazingira yanayowazunguka ili wanafunzi waweze kuwaelewa na kupenda masomo. Mafunzo hayo yalipewa jina la Connected Learning for Secondary Schools STEM Teacher’s Capacity Builng (CL4STEM).
Aprili 29 – 30, 2024 Dkt. Edephonce Nfuka akiwa na Wataalamu wengine aliongoza ziara ya kutembelea walimu katika shule zote Tisa zilizoshiriki mafunzo hayo na kufanya tathimini kwa kile walichojifunza kama wanafunzi waweze kupenda masomo ya Sayansi.
Siku ya Kwanza Aprili 29, 2024 ziara ilianza katika shule za Sekondari Mgama iliyopo katika Kata ya Mgama, Tanangozi iliyopo katika Kata ya Mseke, Lipuli iliyopo katika Kata ya Kalenga na Bread of Life iliyopo katika Kata ya Kiwele.
Dkt. Nfuka ameweza kuona wanafunzi wakipenda masomo hayo kwa kuingia darasani wakati Mwalimu akiwa anafundisha, na kuona wanafunzi wanavyoshirikishwa katika ujifunzaji.
Aidha Dkt. Nfuka aliweza kuonana na Walimu wa masomo hayo na kujifunza juu ya changamoto na mafanikio waliyopata baada ya kufanya mapinduzi katika masomo hayo.
Walimu wameweza kutoa changamoto na mafanikio ambayo ilionesha mafanikio ni makubwa zaidi kuliko changamoto. Kwamba Mwalimu anaweza kutumia zana kutoka katika mazingira yanayowazunguka kuliko hapo awali, na pia wanafunzi wamebadilika sana kwa kupenda na kuyafurahia masomo hayo.
Siku ya Pili ambayo ilikuwa ni Aprili 30, 2024, ziara iliendelea katika Shule za Sekondari za Kibena Kata ya Ifunda, St. Mary’s, Lumuli Kata ya Lumuli, Shule ya Ufundi Ifunda na Shule ya Sekondari Lyandeembele Kata ya Ifunda.
Huko Dkt. Nfuka aliweza kujionea Walimu walivyofurahishwa na mafunzo waliyopata, na walimu wanaweza kushirikisha wanafunzi katika ufundishaji na ujifunzaji, pia ameweza kusisitiza walimu kutumia program hii na njia mbalimbali kwa ajili ya kujifunza zaidi.
Dkt. Nfuka amefurahishwa na mapokeo ya Walimu na Wanafunzi kwani Serikali itaweza kutafuta mbinu nzuri zaidi za kuwewezesha Walimu.
Naye Afisa Taaluma wa Halmashauri Bi. Tina Sanga amewaambia walimu wasiache kutumia mbinu hizi kwani ni muhimu sana kwa uboreshaji wa taaluma, pia imemfanya mwalimu ajivunie kuwepo darasani kufundisha kifua mbele kwani mwanafunzi anamuelewa zaidi na hatimaye kuleta mabadiliko katika elimu.
Baadhi ya Walimu wamesema “katika mafunzo tuliyojengewa uwezo, tumeweza kujifunza zaidi ya kile tulichokuwa nacho, hii imetusaidia kuongeza ubunifu na kumshirikisha mwanafunzi kila hatua katika ujifunzaji, na kwamba mwanafunzi anelewa kwa haraka na kulipenda somo”.
Kadhalika Walimu wametoa maombi kwa Serikali kuwa, mafunzo kama hayo yawe yanatokea mara kwa mara, kwani inasaidia kuwakumbusha taaluma zao na kuwafanya wanafunzi wawepo muda wote wa vipindi.
Pia wameomba kuongezewa vifaa vya kisasa zaidi ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, japo kwa sasa wamweza kutumia vishikwambi, kompyuta, na simu vinavyowasaidia kutufuta mbinu zaidi za ufundishaji.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa