Benki Kuu ya Tanzania Yatoa Elimu ya Mikopo
Wataalam kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imefanya ziara kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa lengo la kutoa elimu kwa watumishi juu ya kuchukua mikopo kutoka kwenye Taasisi mbalimbali za kifedha.
Wataalam hao ni Meneja wa Uendeshaji Bi. Graceana Erasto Bemeye na Meneja Msaidizi Kitengo cha Benki Bi. Sweetlet Mushi, ambao wametokea Benki Kuu Tawi la Mbeya, wamewaasa watumishi pindi wanapotaka kuchukua mkopo kutoka kwenye Taasisi za Kifedha basi ni muhimu wajue mambo mbalimbali juu ya Taasisi husika.
“Benki Kuu inashauri watumishi tukope kwenye Taasisi za kifedha ambazo zimesajiliwa na zina Leseni halali kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Hii itasaidia pale ambapo utapata tatizo katika mkopo wako kuwachukulia hatua za kisheria, kwani Taasisi ikikosea masharti iliyopewa na Benki Kuu huweza kufutiwa Leseni na kufungiwa huduma”.
Pamoja na mambo mengine Wawezeshaji wamesema, kila Taasisi ya Fedha lazima iwe na dawati la kutatua migogoro kati yao na mteja, na kwamba mgogoro unapowasilishwa katika dawati hilo, ni lazima utatuliwe ndani ya siku 14, kama utakuwa bado basi huongezwa siku saba. Ikishindikana hapo mteja anaweza kuwaandikia Benki Kuu na kuwasilisha mgogoro wake na Taasisi husika.
Wawezeshaji wamesisitiza kuwa, baada ya hii elimu wnaanchi/watumishi wawe makini zaidi wakati wa kwenda kukopa kwenye Taasisi yoyote ya kifedha, na kuongeza kuwa, kusoma mkataba wa ukopeshaji ni muhimu sana kabla ya kusaini mkataba huo.
Pia imesisitizwa mtumishi kulinda sana namba ya usajiri wa ajira (Cheki Namba) ikiwa na nywila au neno siri (Password) ya akanti ya benki.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa