Care WWF Aliance Yatoa Tuzo kwa Halmashauri
Care WWF Alliance wametoa tuzo kwa Halmashari ya Wilaya ya Iringa kwa kutoa ushirikiano mzuri wakati wanatekeleza miradi yao. Care wamemaliza mkataba wao wa miaka mitatu na Halmashari, wa kufanya miradi mbalimbali ya kuwakomboa wananchi na kuwapatia ujuzi katika vijji 21 vya Halmashari, ambapo ulianza 2019.
Akitoa taarifa fupi ya mafanikio tangu mradi uanze kwa Baraza la Madiwani, Meneja wa Mradi huo Dkt. Abubakary Kijoji amesema,” mafanikio mengi yamepatikana kutokana na ushirikiano mzuri wa ninyi viongozi wa Kata kwa kuwaeleza wananchi na kuelewa nini kitafanyika. Mafanikio hayo ni pamoja na kuweza kutoa mafuzo kwa wanawake jinsi ya kufanya ujasiriamali, kuwawezesha vijana namna ya kilimo bora chenye tija, kuanzisha AMCOS kwenye vikundi mbalimbali, kutoa mikopo kwenye vikundi vya Wajasiriamali, kutoa mafunzo ya lishe bora kwa jamii, kutoa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi, utoaji wa hati za kimila ambapo hati 6000 zimetolewa na hati 900 zipo kwenye mchakato, namna ya utunzaji wa vyanzo ya maji, namba bora ya kujiwekea akiba na hisa kwenye vikoba na mafunzo ya uandaaji wa mbegu”.
Aidha, Dkt. Kijoji ameendelea kusema kuwa, baadhi ya vijiji kufanya shughuli za mazingira na uhifadhi na ufugaji nyuki. Pia vikundi 41 vipo hai vinafanya uwekezaji katika kazi za utengenezaji wa batiki, sabuni na ukusanyaji wa mazao na kuyauza, na vikundi zaidi ya 11 vilipewa mkopo wa Milioni 153.
Care waliweza kutoa maoni yao juu ya nini kifanyike ili vikundi na elimu iliyotolewa isipotee na kuwaambia Baraza la Madiwani kuwa, waendelee kuwatambua Waganikazi na Walimu wa vikundi, kwa kuwajengea uwezo zaidi ya kilimo ili waweze kuwahudumia wakulima wengi zaidi, kuona uwezekano wa kuwa na bajeti maalumu ya mashamba darasa kupitia Waganikazi waliopo huko vijjini, kuimarisha jukwaa la mbegu, kuimarisha usimamizi wa matumizi bora ya ardhi na kuiweka jamii pamoja.
Wajumbe nao waliweza kutoa maoni yao kwa kuwaambia Care kuwa, elimu zaidi itolewa kwa wananchi juu ya miradi hii na faida zake, kwani elimu ikitolewa ya kutosha wananchi watajifunza na kuona umuhimu wa miradi hii.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Stephen Mhapa, amewashukuru sana Care kwa kuleta miradi hiyo kwenye Halmashauri na kuwaomba waendelee kuleta tena katika vijiji ambavyo havijafikiwa.
Kadhalika Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja amewashukuru Care na kuwapongeza kwa usimamizi mzuri tangu mwanzo wa mradi hadi unamalizika, na kwamba baadhi ya wananchi wameelewa umuhimu wa miradi hii, na kwamba wajumbe wameshuhudia kilichofanyika katika maeneo yao.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa