Changamoto Kutoka Kwenye Kata Zifanyiwe Kazi
“Nawaagiza Mkurugenzi na Watalaam wote kuwa, changamoto zote zilizowasilishwa na Madiwani zifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo, kwani uchaguzi wa Serikali za Mitaa umekaribia, ili kusiwe na manung’uniko kwa wananchi”.
Kauli hii imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Stephen Mhapa alipokuwa anatoa hotuba katika Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa Robo ya Kwanza Julai – Sepemba 2023/2024, ambapo ni muendelezo wa Mkutano huo tangu Desemba 07 na kuhitimisha Desemba 08, 2023.
Mheshimiwa Mhapa pia aliwakaribisha Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA), ili waje waeleze mpango kazi wao katika kuimarisha barabara za Halmashauri. Ndugu Barnabas Jabir ambaye ni Meneja wa TARURA aliweza kueleza mpango uliopo katika kutengeneza na kukarabati barabara mbalimbali za Halmashauri na kufafanua kuwa, wanahitaji ushirikiano wa wananchi kwenye maeneo husika ili kazi ifanyike kwa urahisi, na kusisitiza kuwa, wananchi wajitahidi kusafisha mitaro na mifereje ili maji ya mvua yasiache njia yake.
Mheshimiwa Mhapa pia aweza kuwakaribisha Mamlaka ya Maji Safi na Salama vijijini (RUWASA), naye Ndugu Exaud Humbo ambaye ni Meneja wa RUWASA aliweza kutoa ufafanuzi juu ya mpango wa utengenezaji na uboreshaji wa miundombinu ya maji katika Kata za Halmashauri, na kwamba miradi mingi imeanza na ipo katika utekelezaji.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa