Kamati ya Menejiment Yafanya Ziara
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Daktari Samwel Marwa ameongoza Kamati ya Menejimenti kufanya ziara kukagua miradi ya maendeleo kwa kipindi cha Robo ya Kwanza kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 tarehe 17/10/2022
Katika ziara hiyo Kamati imetembelea baadhi ya Kata za Halmashauri zikiwemo Kata ya Kihorogota katika Kijiji cha Mikongw’i kwenye mradi wa ujenzi wa vyoo matundu saba ya Zahanati.
Mradi huo wa vyoo vya Zahanati umekadiriwa kutumia kiasi cha Shilingi Milioni 28.4 ambapo kati ya hizo kiasi cha shilingi Milioni 4.2 ni nguvu za wananchi. Ujenzi ulianza tarehe 05/08/2022 na unategemewa kukamilika tarehe 05/11/2022 hadi sasa ujenzi umefikia 35/%, ujenzi unaendelea.
Kamati iliendelea na ziara yake hadi Kata ya Kising’a Kijiji cha Kinywang’anga kwenye mradi wa ujenzi wa Zahanti, ambapo mradi unakadiriwa kutumia kiasi cha Shilingi Milioni 50.
Ujenzi wa Zahanati hiyo ulianza mwezi Aprili 2022 na ulitegemewa kukamilika mwezi Agosti 2022, ambapo kutokana na changamoto zilizo nje ya uwezo, haukuweza kukamilika kwa wakati. Ujenzi umefikia 99% ambapo hatua ya ufungaji wa mabomba ya maji unaendelea.
Kamati pia imeendelea kufanya ziara katika Kata ya Kiwele Kijiji cha Kitapilimwa kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya na kukagua baadhi ya majengo ambayo yanaendelea na ujenzi, ambapo ni ujenzi wa wodi ya wazazi na upasuaji, jengo la kufulia nguo na kichomea taka. Majengo mengine ya OPD na maabara yalikwishakamilika, na yametumia kiasi cha Shilingi Milioni 250. Ujenzi umefikia 60% na ujenzi bado unaendelea.
Mwenyekiti ameendelea kuongoza Kamati na kwenda Kata ya Itunundu katika Hospitali ya Wilaya Igodikafu ambapo kuna ujenzi wa jengo la dharura lililotumia kiasi cha Shilingi Milioni 300 kwa fedha za UVIKO-19, nyumba ya mtumishi mbili kwa moja (2 in 1), ambapo zimetumika kiasi cha Shilingi Milioni 90, wodi ya upasuaji kwa wanawake na wodi ya upasuaji kwa wanaume, jengo la kuhifadhia maiti na jengo la upasuaji (Main Theatre), ambapo zimetumika kiasi cha Shilingi Milioni 800.
Kamati pia imefanya ziara katika Kata ya Mlenge Kijiji cha Magombwe ambapo kuna mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mlenge. Mradi huu umeletwa na Serikali kupitia progamu ya Secondary Education Quality Improvement Programme (SEQUIP) kwa fedha za Benki ya Dunia (World Bank), ambapo kiasi cha Shilingi Milioni 600 zimetolewa kukamilisha mradi huu, lakini awamu ya kwanza zimetolewa kiasi cha Shilingi Milioni 470 ili kuanza mradi. Katika kiasi hicho yamejengwa madarasa nane (8), maabara tatu (3), jengo la Utawala, Maktaba, chumba cha TEHAMA, vyoo vya wanafunzi wa kike na wa kiume matundu kumi na nane (18), vyoo vya Walimu.
Katika awamu hiyo ya fedha madarasa manne (4) yamekamilika kwa 100% ujenzi wote kwa ujumla umefikia 75%. Ujenzi bado unaendelea.
Mwenyekiti ametoa rai kwa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuongeza kasi ya ujenzi kwani majengo hayo yanategemewa kuanza kwa watoto wa Kidato cha Kwanza 2023. Kutokana na majengo mengine kutokamilika kwa wakati kiasi cha Shilingi 214.5 zinahitajika.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa