CMT Yashirikiana na Wananchi Kuchimba Mfereji Weru
Kamati ya Menejimenti ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Daktari Samwel Marwa leo Januari 22, 2024 imetembelea Shule ya Sekondari Weru ambayo imepata madhara ya kujaa kwa maji yanayosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Awali Kamati hiyo ilitembelea Januari 20, 2024 baada ya kupata taarifa juu ya madhara hayo, na kupanga mikakati nini kifanyike katika kudhibiti madhara hayo. Kati ya mikakati iliyowekwa ni kuchimba mfereji mkubwa ambao utadhibiti maji yanayotoka milimani na kuja katika viwanja vya shule hiyo.
Aidha, Kamati kwa kushirikiana na uongozi wa Kata, Kijiji, Kitongoji na wananchi kwa ujumla leo wamefanikiwa kufanya kazi hiyo ya kuchimba mfereji.
Vijiji vilivyoshiriki katika kazi hiyo ambavyo vinanufaika na ujenzi wa shule hiyo ni Kijiji cha Weru, Kibebe, Mwambao na Lupalama ‘B’.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa