DC KESSY AKAGUA MIRADI NA KUZUNGUMZA NA BARAZA LA MAENDELEO LA TARAFA YA KIPONZELO NA ISIMANI
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Veronica Kessy amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo katika Tarafa ya Kiponzelo, Kalenga na Isimani.
Ziara hiyo ambayo imekuwa ya siku mbili tarehe 12-13/05.2023, Mhe. Kessy amepata fursa ya kuzungumza na Wajumbe wa Kamati za Maendeleo Tarafa ya Kalenga na Isimani kwa lengo la kujitambulisha na kusikiliza kero kutoka kwa wajumbe wa maeneo husika
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya walimu ya familia mbili (two in one) katika Shule ya Msingi Kihanga, ambapo Serikali imepeleka Kiasi cha Tsh. 50,000,000/- kwaajili ya Umaliziaji wa kazi hiyo, umaliziaji wa Zahanati ya Kijiji cha Mwambao, Kata ya Ulanda ambapo pia Serikali Imepeleka fedha kiasi cha Tsh. 50,000,000/- za umaliziaji na ujenzi wa miundombinu ya vyoo, umaliziaji wa jengo la nyumba ya walimu katika shule ya Msingi Mlambalasi ambapo vilevile Serikali imepeleka kiasi cha Tsh. 50,000,000/- kwa ajili ya kazi hiyo, ujezi wa uzio na matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Kipera iliyopo Kata ya Nzuhi. Hii ni Shule Jumuishi ambayo ina watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali yaani wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa ngozi, wenye ulemavu wa viungo, usonji na ulemavu wa akili. Katika shule hii Serikali imepeleka kiasi cha Tsh. 30,000,000/- kwaajili ya ujenzi wa uzio na matundu ya vyoo na kazi imeshaanza, umaliziaji wa nyumba ya Walimu katika shule ya Msingi Mikong’wi ambapo kazi ipo katika hatua ya umaliziaji. Hapa Serikali imetoa kiasi cha Tsh. 25,000,000/- na kazi inaendelea, umaliziaji wa jengo la Zahanati katika Kijiji cha Holo ambapo Serikali imepeleka Fedha Zaidi ya Tsh. 51,000,000/- ili kufanya umaliziaji wa upande mmoja wa Zahanati ambao utaanza kutumika kutolea huduma kwa wananchi. Miradi hii yote imeanza kufanyika katika Mwaka wa Fedha 2022/2023.
Aidha, Mhe. Kessy alipata fursa ya kuwatembelea wanakikundi cha ufugaji wa mbuzi katika kijiji cha Makatapola Kata ya Izazi, ambao Serikali imewawezesha kuanzisha mradi huo ikiwa na lengo la uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji na Serikali kupitia ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira kwa awamu ya kwanza imetumia Zaidi ya Tsh. Milioni 188 kwenye kuwezesha vikundi.
Mh. Kessy amewasisitiza wananchi kutumia miradi hii kama fursa na kwamba wanatakiwa kuitunza na kuilinda ili iweze kudumu kwa vizazi vijavyo.
Kwa upande wao, wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi wametoa pongezi zao za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutoa fedha nyingi za miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa